Friday, July 20, 2012

Kujihifadhi ni Miongoni mwa sifa Alizozitaja za mwanamke na si tu kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan

Kujihifadhi ni Miongoni mwa sifa Alizozitaja za Mwanamke Allaah
(Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu
zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe
shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume
zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa
waume zao, au kaka zao, au... wana wa kaka zao, au wana wa dada zao,
au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi
wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo
yaliyokhusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo
waliyoyaficha. Na tubuni nyote kwa Allah enyi Waumini, ili mpate
kufanikiwa.

Hivyo ni vyema kujisitiri wakati wote ma si tuu mwezi wa Ramadhan au siku ya ijumaa kama wafanyavyo baadh ya akina mama na akina dada

No comments: