Friday, May 17, 2013

PICHA ZA UCHI ZA WATANZANIA ZAZIDI KUSAMBAA MTANDAONI.. BONYEZA HAPA KUANGALIA

PICHA ZA UCHI ZA WATAMZANI
HI NI LAANA KWA WATANZANIA
MITANDAO YAGEUZWA UWANJA WA NGONGO

Kutokana na kukua kwa teknolojia siku za karibuni maadili yameonekana
kushuka kwa kiasi kikubwa kwan mitandao ming ya kijamii imekuwa
ikisambaza picha za ngono kwenye mitandao huku wakidai kuwa
wanafikisha ujumbe katika jamii, mitandao hyo imeonekana kuwa na
wapenz na wafuatiliaji weng sana kwa kuvutiwa na uchafu huo ambao
unaendelea kukua kila siku,

Sidhani kama unaielimisha au kuikosoa jamii kwa nafasi uliyoipata ya
kumiliki Blog au kumiliki website na kisha unatumia picha zenye
maadili mabovu kwa kudai kuwa unafikisha na kisha unajiita
Mwanaharakati wa kuondoa maovu, inakufaa ubadilike na kuacha tabia
hiyo mapema

Muogope Mola wako aliyekuumba

Thursday, February 21, 2013

Hukmu Ya Muziki Katika Qur-aan Na Sunnah - Ewe Upendaye Nyimbo Na Muziki, Haujafika Wakati Wa Kuogopa Adhabu Kali Za Allaah?


Hukmu Ya Muziki Katika Qur-aan Na Sunnah - Ewe Upendaye Nyimbo Na Muziki, Haujafika Wakati Wa Kuogopa Adhabu Kali Za Allaah?



Muziki ni haraam kutokana na dalili dhahiri tulizopewa katika Qur-aan na Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Baadhi wa watu katika Jamii yetu bado hawajatambua uharamu wa jambo hili, tunasikia wengi bado wanaimba taarabu au miziki mbalimbali, na mara kwa mara unapomnasihi nduguyo Muislamu kuacha maasi haya, jibu mara nyingi huwa: "Tena nyinyi mmezidi! Wapi inasema kuwa nyimbo haramu" Au wengine waliobobea katika maradhi haya hunena: "Mimi yote naweza kuacha lakini nyimbo utaniua", husema hivyo bila ya kujali amri ya makatazo ya Mola Mtukufu ambaye ni Muweza wa kuyaua masikio yake awe kiziwi na asiweze kusikia tena hizo nyimbo.
Inafika hadi Muislam hawezi kulala hadi alazwe kwa muziki, hawezi kula ila muziki uwe unapigwa, hawezi kufanya kazi za nyumbani bila muziki kufunguliwa, hawezi mtu kutembea bila kuwa na walkman au mp3 yake ikicheza, hawezi kufanya kazi akiwa kazini…hawezi kusafiri…hawezi hata kufanya mazoezi ya ndani bila kuwepo na muziki wa kumchochea na kumtia hamasa (kama wanavyoitakidi) ya lile analolifanya kwa wakati huo! ‘Alaa kulli haal, muziki umekuwa ni sehemu kiungo kikubwa cha maisha ya mwanaadam kwa wakati huu!
Hivyo tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kuwakumbusha ndugu zetu waepukane na haramu hii ili wajiokoe na ghadabu za Mola Mtukufu, ghadhabu kali ambazo zinafika kumgeuza mtu awe nyani au nguruwe kama tutakavyosoma katika hizi dalili za wazi wazi zenye uhakika.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ))

((Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha)) [Luqmaan: 6]

Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kuhusu Aayah hii "Naapa kwa Allaah hii inamaanisha ni kuimba" [At-Twabariy 20:127]

وعن ابن عباس قال عن آية: ((ومن الناس من يشتري لهو الحديث))، قال :الغناء وأشباهه إسناده صحيح - المحدث: الألباني

Na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) pia amesema kuhusu Aayah: ((Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi)) "Ni nyimbo na maneno ya yanayofanana (ya upuuzi)" [Isnaad Sahiyh kutoka kwa Shaykh Al-Albaaniy]
 
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anamwambia Ibliys:


((وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُمْ بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِم بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِي الأَمْوَالِ وَالأَوْلادِ وَعِدْهُمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلاَّ غُرُورًا))

 
((Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na shaytwaan hawapi ahadi ila ya udanganyifu)) [Al-Israa: 64]
Hii inamaanisha ni nyimbo kama ilivyo rai ya Mujaahid katika Tafsiyr ya Ibn Kathiyr]
Vile vile Hadiyth zifuatazo zimedhihirisha uharamu wa nyimbo, ngoma na kila aina ya muziki:

عبدالله بن عمرو بن العاص عن رسول الله صلى الله عليه وسلم انه قال: ((إن الله حرم الخمر والميسر والكوبه وكل مسكر حرام ((إسناده صحيح و في رواية أحمد قال سفيان: قلت لعلي بن بذيمة: "ما الكوبة؟" قال: "الطبل"
Kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Amru ibnul 'Aasw kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ameharamisha pombe na kamari na kuubah na kila kilinacholewesha ni haram)) [Isnaad yake ni Sahiyh]
Na katika usimulizi mwingine kutoka kwa Imaam Ahmad, Sufyaan amesema: Nilimuliza 'Aliy ibn Budhaymah: "Nini Kuubah?" Akasema: "Ngoma".


 WENYE KUIMBA/KUSIKILIZA MUZIKI WATAGEUZWA KUWA NYANI NA NGURUWE
  
وقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((ليكونن من أمتي أقوام يستحلون الحر و الحرير و الخمر و المعازف، و لينزلن أقوام إلى جنب علم، يروح عليهم بسارحة لهم، يأتيهم لحاجة، فيقولون: ارجع إلينا غدا، فيبيتهم الله، ويضع العلم، ويمسخ آخرين قردة وخنازير إلى يوم القيامة ((رواه البخاري
Na akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Watakuweko watu katika Ummah wangu watakaojaribu kuhalilisha zinaa, uvaaji wa hariri, pombe na muziki. Baadhi ya watu watakuwa pembeni mwa mlima na mchungaji wao atawajia jioni na kuwaomba haja [fulani]. Watasema: "Rudi kesho". Allaah Atawaangamiza usiku, Atawaangushia milima kisha Atawabadilisha waliobakia wawe nyani na nguruwe na watabakia hivyo hadi siku ya Qiyaamah))[Al-Bukhaariy]


Hadiyth hii inatuthibitishia kuwa madhambi yote hayo yako sawa sawa uharamu wake,
kama vile zinaa na pombe ilivyo haramu, basi na muziki pia haramu sawa sawa. Sasa vipi Muislamu aone kuwa muziki sio maasi makubwa ya kujiepusha nayo?
 
Imaam Abu Haniyfah amesema: "Kuimba (nyimbo, ngoma) ni katika madhambi makubwa ambayo inatakiwa Muislamu kujiepusha nayo haraka"
 
Khofu zaidi imuingie Muislamu kuwa anaweza kupata adhabu ya kugeuzwa nyani au nguruwe kwa maasi haya kama tulivyoonywa katika Hadiyth ifuatayo:


 
وقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((ليشربن أقوام من أمتي الخمر يسمونها بغير اسمها يعزف على رؤوسهم بالمعازف والمغنيات ، يخسف الله بهم الأرض ويجعل منهم قردة وخنازير  ((قال الشيخ الألباني- رحمه الله تعالى- : صحيح

 
Na kasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Watu katika Ummah wangu watakunywa pombe wakiipa jina jengine lisilokuwa hilo, miziki itapigwa kwa ajili yao na watakuweko waimbaji wanawake. Allaah Atawadidimiza ardhini na Atawageuza wawe nyani na nguruwe)) [Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy ameipa daraja ya Sahiyh]



 GHADHABU ZA ALLAAH KUWAANGAMIZA WAFANYAO MAASI HAYA
 
 
Vile vile ghadhabu za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni kali mno za kuangamizwa pindi maasi haya yatakapodhihirika.


 عن عمر بن حصيل عن رسول الله صلى الله عليه وسلم انه قال: ((يكون فى امتى قذف ومسخ وخسف)): قيل يارسول الله ومتى ذلك قال: ((اذا ظهرت المعازف… )) اخرجه الترمذى وصححه العلامه الالبانى

 
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Kutatokea katika Ummah huu maafa ya kuteremshiwa mawe kutoka mbinguni, kugeuzwa maumbile ya binaadamu [kugeuzwa kufanywa nyani na nguruwe] na mididimizo [ya ardhi]. Ikaulizwa: Ewe Mjumbe wa Allaah, lini yatatokea hayo? Akasema: ((Itakapodhihirika muziki … )) [At-Trimidhy na ameipa daraja ya Sahiyh Shaykh Al-Albaaniy]

 
 TUSIKILIZE NA KUSOMA QUR-AAN

Muziki na nyimbo humjaza mtu mapenzi makubwa moyoni, zimshughulishe zaidi hadi asiwe na muda wa kusoma maneno ya Mola wake Mtukufu ambayo hiyo ndio inayopasa kuifanya iwe midomoni na moyoni mwetu daima kwa kusoma kwa sauti nzuri ya kupendeza (Tajwiyd) kama tulivyoamrishwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



 SAUTI ZA NYIMBO ZIMELAANIWA DUNIANI NA AKHERA

 قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((صوتان ملعونان فى الدنيا والاخره مزمار عند نعمه ورنه عند مصيبه ((البزار و صححه العلامه الالبانى

 Na kasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Sauti mbili maluuni [zilizolaaniwa] duniani na Akhera; mizumari katika furaha na kuombeleza katika misiba)) [Al-Baazaar – na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Sahiyh]
 

 NI SUNNAH KUZIBA MASIKIO UNAPOSIKIA MUZIKI BILA YA KUTAKA

 عن نافع أنه قال: سمع ابن عمر مزمارا، قال: فوضع أصبعيه على أذنيه، ونأى عن الطريق، وقال لي: يا نافع هل تسمع شيئا؟ قال: فقلت: لا! قال: فرفع أصبعيه من أذنيه، وقال: كنت مع النبي صلى الله عليه وسلم، فسمع مثل هذا! فصنع مثل هذا - حديث صحيح، صحيح أبي داوود وراجع السلسلة الصحيحة للألباني 
Kutoka kwa Naafi'i ambaye amesema, amesikia sauti ya muziki akaziba masikio yake kwa vidole vyake, kisha akamgeuza mnyama wake aliyempanda [arudi asiendelee kwenda sehemu hiyo iliyokuwa na muziki] akasema: "Ewe Naafi'i, umesikia kitu?" Akasema, nikajibu: "Hapana". Akaondosha vidole vyake masikioni mwake akasema: "[siku moja] Nilikuwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliposikia kama hivi [muziki] akafanya kama hivi [nilivyofanya mimi yaani kuziba masikio yake asisikie sauti ya mizumari] [Hadityh Swahiyh ya Abu Daawuud  na   Ikiwa katika Silsilatus-Swahiyha ya Shaykh Al-Albaaniy]

 

 
و قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((لا تصحب الملائكة رفقة فيها كلب ولا جرس ((مسلم
 
Na kasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Malaika hawafuatani na watu wenye mbwa na walio na kengele)) [Muslim]
 
Tanbihi: Ikiwa kengele tu inawakimbiza Malaika, seuze nyimbo, ngoma, mizumari na aina zote za muziki ambazo zinaamsha vishawishi na kuchochea hisia za binaadamu!


 MWENYE KUMPA MWENZIWE TAARIFA AU KUMPELEKA KWENYE MUZIKI ATABEBA DHAMBI ZAKE NA DHAMBI ZA MWENZIWE

Mara nyingi Waislamu wenye kufanya maasi haya wanasabisha wenzao kutumbukia pia katika maasi haya; kuna wanaoalika watu katika shughuli zenye maasi hayo (parties) zenye mchanganyiko wa wanawake na wanaume, wenye kupiga taarabu katika maharusi, na wengine wanaofika hadi kununua kanda (cassettes), CD au Video na kuwapa wenziwao kama zawadi.
 
Watambue wanaoanza kuwahusisha wenziwao na maasi haya kuwa watabeba madhambi yao na ya wenziwao pia na hizo dhambi ataendelea kupata mwenye kuanzisha kila yanaposambaa kwa maelfu ya watu! Ni mzigo mzito kiasi gani atakaoubeba mwenye kumhusisha mwenziwe na maasi haya?

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):


 
((إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي الْمَوْتَى وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ
وَكُلَّ شَيْءٍ أحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُبِينٍ))  
((Hakika Sisi Tunawafufua wafu, na Tunayaandika wanayoyatanguliza, na wanayoyaacha nyuma. Na kila kitu Tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha))
[Yaasiyn:12]
 
Pia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia:

 
((من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً ومن سن في الإسلام سنة سيئة كان عليه وزرها ووزر من عمل بها من بعده لا ينقص من أوزارهم شيئاً)) خرجه مسلم في صحيحه

((Atakayefanya kitendo chema katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao. Na atakayetenda kitendo kibaya katika Uislam atabeba (mzigo wa) dhambi zake na dhambi za yule atakayetenda wala hapungukiwi kitu katika (mzigo wa) dhambi hizo)) [Muslim]

 
TAHADHARI NDUGU MUISLAMU! BINAADAMU ATAFUFULIWA NA 'AMALI YAKE YA MWISHO


 Ikiwa ndugu yetu Muislamu ni mpenda muziki sana, basi tunakuomba utahadhari na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliyosema:

 

 
عن جابر بن عبدالله قَالَ : سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (( يُبْعَثُ كُلُّ عَبْدٍ عَلَى مَا مَاتَ عَلَيْه ((رواه مسلم

Kutoka kwa Jaabir bin 'Abdullaah ambaye amesema: "Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Kila mja atafufuliwa katika hali aliyofia nayo))[Muslim]
 
Je, ndugu Muislamu unayependa muziki, umetafakari vipi utakuwa mwisho wako?

Je, haikuingii khofu katika moyo wako kuwa huenda mwisho wako ukawa ni kuimba nyimbo badala ya kusema "Laa ilaaha Illa Allaah" neno ambalo ukilitaja mwisho wa maisha yako wakati wa kufa utaingia Peponi?

 
KISA CHA KWELI MTU ALIYEFARIKI AKIWA ANASIKILIZA NYIMBO


Katika moja ya nchi za Ghuba, Kijana mmoja aliyekuwa mpenzi wa nyimbo alikuwa haachi kusikiliza nyimbo katika gari lake. Kila alivyokuwa akikatazwa na wazazi wake na wenziwe waliokuwa wameongoka hakuwa akitaka kusikia nasaha hii. Siku ya ajali yake alitoka akiwa anaendesha gari yake na huku akisikiliza nyimbo ya Ummu Kulthuum 'Hal Ra-al-Hubbu Sukaara' (Je, hakuona mapenzi yanavyolewesha). Alipata maafa mabaya katika ajali hiyo ya gari na ukawa ndio mwisho wake. Kabla ya roho yake kutoka, walijaribu Maaskari wa usalama wa barabarani na waliokuweko kumlakinia (kumsemea atamke 'Laa ilaaha illa Allaah') lakini wapi! Kila akiambiwa aseme 'Laa ilaaha illa Allaah' alikuwa akitamka ''Hal Ra-al-Hubbu Sukaara" "Hal Ra-al-Hubbu Sukaara" na hayo ndio yakawa ni maneno yake ya mwisho akielekea kuonana na Mola wake Mtukufu, na ndio atakayofufuliwa nayo!



Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aturuzuku mwisho mwema na tunatumai kuwa ndugu zetu ambao bado wako katika maasi haya, watakaposoma dalili hizi, zitakuwa ni mazingatio kwako na kumkhofu Mola wao Mtukufu wajiepusha na uharamu huu na wabaki katika Radhi Zake Allaah

SWLLAH -3- Amri za mwanzo kwa mitume waliopita

SWALAH - 3 - Amri za Mwanzo Kwa Mitume Waliopita

Swalah ilikuwa ni amri ya kwanza hata kwa Mitume waliopita. Alipozaliwa Nabii 'Iysa (‘Alayhis Salaam) maneno ya mwanzo aliyotamka akiwa bado mtoto mchanga ni kuwa ameamrishwa Swalah:

فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا﴿27﴾يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا﴿28﴾فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا﴿29﴾قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا﴿30﴾وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا﴿31


27. Akaenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryam! Hakika umeleta kitu cha ajabu! 

28. Ewe dada yake Haaruun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. 

29. Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi? 

30. (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Allaah, Amenipa Kitabu, na Amenifanya Nabii 

31. Na Amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na Ameniusia Swalah na Zakaah maadamu ni hai.
[Maryam: 27-31]

Nabii Muusa pia alipoanza tu kupewa ujumbe, ujumbe huo ulikuwa ni ukumbusho wa Swalah

وَهَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَى﴿9﴾إِذْ رَأَى نَارًا فَقَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًالَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِقَبَسٍ أَوْ أَجِدُ عَلَى النَّارِ هُدًى﴿10﴾فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِي يَا مُوسَى﴿11﴾إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى﴿12﴾وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَى﴿13﴾إِنَّنِي أَنَا اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي﴿14

9. Na je! Imekufikia hadithi ya Muusa? 

10. Alipouona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto.

11. Basi alipoufikia akaitwa: Ewe Muusa! 

12. Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la Twuwaa. 

13. Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayofunuliwa. 

14. Hakika Mimi ndiye Allaah Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Swalah kwa ajili ya kunikumbuka Mimi.
[Twaahaa: 9-14]

Nabii Ismaa'iyl amesifiwa kwa kuamrisha watu wake Swalah

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِسْمَاعِيلَ إِنَّهُ كَانَ صَادِقَ الْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا﴿54﴾وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِ مَرْضِيًّا﴿55

54. Na mtaje katika Kitabu Ismaa'iyl. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.  

55. Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Swalah na Zakaa, na alikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa
[Maryam: 54-55]

Bila ya shaka ni ibada iliyo muhimu kupita zote kutokana na ishara kama hizo, na bila ya shaka umuhimu wake huo ni kwa ajili ya uhusiano wetu sisi waja na Mola wetu Mlezi Aliyetuumba kwa ajili ya kumuabudu Yeye pekee:

((وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُون))

((Nami Sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.)) [Adh-Dhaariyaat: 56]
 

SWALLAH - 2 - Kusisitizwa Kwake na Malipo YAKE

SWALAH - 2 - Kusisitizwa Kwake na Malipo yake


Swalah hakika ni jambo muhimu na tukufu katika Uislamu, na uthibitisho wake ni kama ufuatao:

Swalah Ni Nguzo Ya Dini:

Hadiyth ndefu inayotoa maelezo yafuatayo:

عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه (( ...ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال: (( رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ))
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ     ٌ
Kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu 'anhu) ((…Tena akasema: Je, nikwambie kilele cha hilo jambo; nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa?))  Nikasema: Ndio ewe Mjumbe wa Allaah.  Akasema:  ((Kilele chake ni Uislamu, nguzo yake ni Swalah na sehemu yake ya juu kabisa ni Jihaad)) [At-Tirmidhiy na Hadiyth Hasan Swahiyh]

Hivyo inapoanguka nguzo huanguka kile kilichojengewa nacho nayo ina maana ni dini yake mtu kwani bila ya kuswali ni kama kafiri kama tutakavyoelezea katika mada zitakazofuatia kuhusu hukmu ya mwenye kuacha Swalah.
    
Jambo La Kwanza Kuulizwa Mja Siku Ya Qiyaamah

((إن أول ما يحاسب به العبد يوم القيامة من عمله الصلاة ، فإن صلحت فقد أفلح وأنجح وإن فسدت فقد خاب وخسر))  التِّرْمِذِيُّ  وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ)
((Kitu cha kwanza atakachohesabiwa nacho mja Siku ya Qiyaamah katika amali zake ni Swalah, ikitengenea atakuwa amefuzu na amefanikiwa, na ikiharibika atakuwa ameshapita patupu na amehasirika….)) [At-Tirmidhy na amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

Bila shaka ni jambo la kumtia khofu kubwa Muislamu kupata hasara siku ya Qiyaamah kwa kuacha tu kuswali.    
  
Wasiya Wa Mwisho Wa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Kwa Ummah Wake

Katika khutbah zake za mwisho aliwausia sana Swalah akisema:

((...الصلاة الصلاة و ما ملكت أيمانكم))    أحمد وصححه الألباني

((…Swalah, Swalah na waliomiliki mikono yenu ya kuume)) [Ahmad na ameipa daraja ya Swahiyh Shaykh Al-Albaaniy]

'Ibaadah Pekee Iliyofaradhiwa Katika Mbingu Ya Saba

Fardhi ya nguzo ya Swalah ni ibaadah pekee aliyoipokea Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mbingu ya saba alipokwenda safari ya Israa Wal-Mi'raaj. Nazo zilikuwa asili yake ni Swalah khamsini kisha zikapunguzwa hadi zikafika tano. Hivyo thawabu zake ni khamsiyn katika mizani ingawa ni tano katika kuzitekeleza.

Sifa Ya Mwanzo Na Ya Mwisho Ya Waja Watakaofuzu

Jinsi Swalah ilivyokuwa ni muhimu na tukufu, Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameanza kutaja Swalah kwa waja Wake watakaofuzu na kupata Pepo ya Firdaws kwa kutekeleza na kudumisha Swalah.

  بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ  
قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ ﴿1 الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ﴿2 وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ ﴿3 وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ ﴿4 وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿5 إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿6 فَمَنِ ابْتَغَى وَرَاء ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿7 وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿8 وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿9 أُوْلَئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ ﴿10 الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿11

KWA JINA LA ALLAAH MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
1. Hakika wamefanikiwa Waumini, 
2. Ambao ni wanyenyekevu katika Swalah zao, 
3. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi
4. Na ambao wanatoa Zakaah
5. Na ambao wanazilinda tupu zao
6. Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa
7. Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka. 
8. Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao
9. Na ambao Swalah zao wanazihifadhi 
10. Hao ndio warithi
11. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo.
[Al-Muuminuun: 1-11]

Kwa hiyo, nani basi miongoni mwa Muumini asiyetaka kuipata Pepo ya juu kabisa karibu na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu tu ya kuacha Swalah? Ibaadah ambayo hata dakika kumi haifiki kuitekeleza?

SWALAH - 1 - Maana Ya Swalah Na Kuwajibika Kwake

e

SWALAH - 1 - Maana Ya Swalah Na Kuwajibika Kwake


 

Maana Ya Swalah Kilugha
 
Ni du'aa kama Anavyosema  Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
 ((خُذْمنْ أَمْوَلِهمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ و تُزَكِّيهِمْ بِهَا و صَلِّ عَلَيْهِمْ إِنَّ صلواتك سَكَنٌ لَّهُمْ وَ آللّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ))
((Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele ya Allaah) na uwaombee du’aa. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu na Allaah ni Mwenye kusikia Mwenye kujua)) [At-Tawbah: 103]
 Hadiyth ifuatayo inathibitisha pia maana hiyo:
 
عن أبي هريرة -رضي الله عنه- قال: قال رسول الله -صلى الله عليه وسلم: ((إذا دعي أحدكم فليجب فإن كان صائمًا فليصلِّ و إن كان مفطرًا فليطعم)) أخرجه مسلم         
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Akialikwa mmoja wenu aitike (mwaliko), ikiwa amefunga  (Swawm) awaswalie (yaani aombe (du'aa kwa waliomualika), akiwa hakufunga basi ale (chakula)))[Muslim]  [Inamaanisha awaombee du'aa ya maghfirah, baraka na kheri)
 
Swalah kutoka kwa Allaah ni sifa njema na kutoka kwa Malaika ni du'aa kama Anavyosema:
((إنَّ اللَّهَ وَ مَلاَئِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى آلنَّبِيِّ يَا أَيُّهَا آلَّذِينَءامَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَ سَلِّمُوا تَسْلِيمًا))
((Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabii. Enyi mlioamini! Mswalieni (muombeeni) na mumsalimu kwa salamu)) [Al-Ahzaab: 56]
Abu 'Alyah amesema: Swalah ya Allaah ni kumsifu mja kwa Malaika Wake na Swalah ya Malaika ni du'aa.
Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) amesema: "Wanawaswalia" maana wanawabarikia"  
Vile vile Swalah kutoka kwa Allaah ni Maghfirah (msamaha) au Baraka. Swalah kwa maana ya Maghfirah nikutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
 ((أُوْلئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَواتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَ رَحْمَةٌ وَ أُوْلئِكَ هُمُ آلْمُهْتَدُونَ))
((Hao juu yao zitakuwa maghfira zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka))[Al-Baqarah: 157]
Na kama ilivyosimuliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alisema:
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى آل أَبِي أَوْفَى
Allahumma Swalli ‘alaa Aali Abi AwfiyAkimaanisha ‘Ee Mola wangu wasamehe jamaa wa Abu Awfiy’.  
Hivyo hapa Swallah ina maana ya Maghfirah (msamaha).
 
 
 
Maana Swalah Kishari'ah
 
Ni kumuabudu Allaah kwa kauli na vitendo maalumu na khaswa (pekee) vinavyoanza na Takbiyr (Allaahu Akbar) na kumalizika na Tasliym (kutoa salam).
Na imeitwa Swalah kwa sababu inahusiana na du'aa katika kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) tunaposimama, tunaporukuu, tunaposujudu na tunapokaa, hivyo Swalah nzima ni du'aa.
 
 
Hukumu Ya Swalah
 
Swalah ni fardhi kwa kila Muislamu mwenye akili timamu, aliyebaleghe kutokana na dalili kutoka katika Qur-aan:
   ((وَمَا اُمِرُواْ إِلاَّ لِيَعْبُدُواْ آللّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ آلدِّينَ حُنَفَآءَوَ يُقِيمُواْ آلصَّلاَةَ وَ يُؤْتُواْ آلزَّكَاةَ وَ ذَلِكَ دِينُ آلْقَيِّمَةِ))
((Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Allaah kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Swalah, na watoe Zakaah. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti))[Al-Bayyinah: 5]
   ((إِنَّآلصَّلاَةَ كَانَتْ عَلَى آلْمُؤْمِنِينَ كِتابًا مَّوْقُوتًا))
((Kwani hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu)) [An-Nisaa: 103]
Ama katika Sunnah ni kauli yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomtuma Mu'aadh Bin Jabal (Radhiya Allaahu) kupeleka ujumbe Yemen kwa kumwambia: ((…na wafundishe kwamba Allaah Amewafaridhisha Swalah tano kila siku…)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]
Vile vile,
  عبدالله بن عمر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (( بُنِـيَ  الإِسْلاَمُ علـى خَمْسٍ: شَهادَةِ أنْ لا إِلٰهَ إلا الله وأنَّ مُـحَمَّداً رَسُولُ الله وإِقامِ الصَّلاَةِ وإِيتاءِ الزَّكاةِ وَحَجِّ البَـيْتِ وَصَوْمِ رَمَضَانَ)) البخاري
Kutoka kwa 'Abdullaah ibn 'Umar ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Uislamu umejengeka kwa matano; Kushuhudia (na kukiri kwa moyo)  kwamba hakuna Mola Apasaye kuabudiwa (kwa haki) isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allaah na kuswali (Swalah tano), kutoa Zakaah, kuhiji katika Nyumba (Makkah) na kufunga (mwezi wa) Ramadhaan)) [Al-Bukhaariy]
Kuna Aayah na Hadiyth nyingi zinazothibitisha kuwajibika kwa Swalah. Ama mwanamke mwenye hedhi na aliye katika nifaas hawawajibiki kuswali kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  
 
((Kwani sio kweli kwamba mwanamke anapokuwa katika hedhi haswali wala hafungi?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]