Alhamdulillah neno "vunja jungu" limetokomea ndani ya manispaa ya morogoro kwa takriban miaka 4 sasa.
---------------------------------------
Kama tunavyofahamu kuwa inapokaribia mwezi wa ramadhan kawaida huwa kunakuwa na matangazo ya madisco na taarab ,katika matangazo hayo huwa linaandikwa neno vunja jungu.
Hii kwa mazoea kuwa mwezi wa tawba umefika hivyo watu wanakumbushwa wamalizie yale maasi kabla mwezi kuingia,au kwa lugha nyingine kuwa ni wito kwa waislaam kufanya maasi kabla ramadhan kuingia.
Na pia zinapokaribia sikukuu zetu za eid huwa matangazo kama haya yanaonekana mitaanai "disco baab kubwa la eid alhajj au eid el fitr"
Hii ni kudhalilisha dini yetu na kuikashif.
Nani wakulamiwa?
Wakulaumiwa ni manispaa idara ya matangazo ambayo inatoa ruhusa hio,kwani huruhusiwi kutoa tangazo lolote bila kuomba kibali manispaa na kulipia.
Wapili kulaumiwa ni waislam wenyewe kukaa kimya bila kudai haki yao.
Kwanini Manispaa ya morogoro imefanikiwa?
Hii ni baada ya waislam kulalamika na kuomba haki yao.
Zipi njia za kufanya ili kuipata haki hio?
Kwanza kabisa tufahamu kuwa nchi yetu si ya kiislaam na inatawalia kisheria na kanuni.
Na pia nchi yetu inadaiwa kuwa haina dini bali inaheshimu dini zote.
Pia kuifahamisha serikali kwa njia ya mdomo na maandishi kuwa hilo jambo ni tusi kwenye dini yetu hivyo kuomba msaada wa serikali kutatua tatizo hilo.
Zifuatazo ni njia sahihi za kuomba haki hizo.
1.Kuunda kamati itakayofuatilia Jambo hilo na kuhusisha taasisi za kiislam zilizopo katika eneo husika,au kuhusisha mtu mmoja mmoja kutoka kila taasisi (bakwata msiwasahau sometimes wanasave :). )
2.Kuwafahamisha wailsam juu ya qadhia hio ili waiunge mkono.
3.Kuiomba serikali (mkurugenzi wa manispaa) isaidie kupiga marufuku jambo hilo na mumfahamishe kwa njia nzuri kuwa jambo hilo ni kukashifiwa kwa dini ya kiislam.
4.Majadiliano yote yawe kwa maandishi na msikubli kujibiwa na midomo lazima kwa maandishi.na kopi ziende kwa rpc na mkuu wa mkoa.
5.Kukumbushia kila wakati majibu hayo kwani kiuzoefu hua yanachelewa sana inaweza kuchukua zaidi ya mwaka.
6.kufanya kazi hio kwa ikhlaas na kuwa na subra kwa yatakayojitokeza.
7.Kuacha kutumia jazba bila kutoa elimu ya jambo hilo kwa serikali.
Nini chakufanya baada ya kupata haki hio?
Kila inapokaribia mwezi wa ramadhan au eid niwajib kuikimbusha serikali kwa barua kuwa ramadhan au eid zinakaribia hivyo kuwakumbusha wale wote wanaokuja kuchukua kibali cha madisco wasihusishe miezi au sikukuu zetu.
Baada ya hapo kila muislam atakae ona tangazo baso ahakikishe analiondoa kwa mkono wake.
Na ushindi unatoka kwa Allah pekee
4 comments:
Inshaallah
Vizuri kwa kuepukika
Asanteni kwa mchango wenu@anonymous & Hussein
Vizuri,asante kwa kutujulisha admin.
Post a Comment