Sunday, May 20, 2012

Adabu za kuvaa

Muislam analiona vazi kuwa limeamrishwa na Allah ktk kauli yake"Enyi
wanadamu chukueni pambo lenu mbele ya kila swala na kuleni na kunyweni
wala msivuke mpaka hakika yeye hawapendi wenye kuvuka
mipaka(al-A'raaf:31)pia ameonyesha neema "Enyi wanadamu hakika
tumeteremsha juu yenu vazi litakalo sitiri tupu zenu na vazi la
kujipamba na vazi la uchaji hilo ndilo bora"(al-A'raaf:26)
Ni juu ya kila muislamu kujilazimisha katika kuvaa kwake na adabu zifuatazo
1-Usivae hariri kwani amesimulia mtume(s.a.w),Msivae hariri kwani
hakika atakaye ivaa hariri duniani hataivaa huko akhera(Muslim)

2-Asirefushe nguo yake au suruali yake au kanzu iliyounganishwa na
kofia yake au shuka lake ya juu mpaka ikavuka fundo zake mbili za
miguu kutokana na kauli yake mtume(s.a.w)"Kilicho chini ya fundo mbili
ktk shuka hicho kitakuwa motoni"Na kauli yake "Kuteremsha shuka na
kanzu na kilemba,mwenye kuburuza hivyo hatamtazama Allah siku ya
kiyama(Abu Daud na Annasi)Na kauli yake:"Hatamtazama Allah mwenye
kuikokota nguo yake kwa kibri(Bukhari na Muslim)

3-Alipe kipaumbele vazi jeupe kuliko nyingne na aone kuvaa rangi aina
zote kunafaa kutokana na kauli yake mtume(s.a.w)
Vaeni nguo nyeupe kwani hzo ni safi na ni nzuri na wakafinini katika
hizo wafu wenu(Attirimidhy)

4-Arefushe muislam mwanamke vazi lake mpaka lifunike nyayo zake na
ateremshe mtandio wake juu ya kichwa chake mpaka afunike shingo na
kifua chake kutokana na kauli ya Allah"Ewe mtume waambie wake zako na
mabinti zako na wake zako na Waislam wateremshe shungi
zao(al-Ahzaab:59)

No comments: