Wednesday, June 13, 2012

Swalah Ya Safari:




11:38am Jun 12
Swalah Ya Safari:
Kwa vile Uislamu ndio njia pekee kamili na sahihi ya maisha, basi unawafikiria Waumini na hali zao katika mazingira tofauti. Na kwa vile safari zina mashaka, misukosuko na taabu, Uislamu unamsahilishia mambo msafiri upande wa Swalah na hata Funga. Hivyo ukiwa safarini swali Rakaa mbili badala ya Rakaa nne katika Swalah ya Adhuhuri, Alasiri na Ishaa. Ama Alfajiri na Magharibi hazipunguzwi. Allah Ametuambia:

Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Swalah"

(4: 101).

Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hii (kupunguza Swalah) ni neema ya Allaah kwenu, basi ipokeeni kwa shukrani" (Al-Bukhari).

Mtu akishatoka sehemu anayoishi kwa nia ya kuwa safarini (safari ianyokusudiwa hapa ni safari ya kheri inayoruhusiwa na Uislamu si safari ya maasiya na ufisadi) inakubidi ufupishe Swalah.

((Amehadithia 'Abdillahi bin 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) kuwa alisafiri na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu), 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) na 'Uthmaan (Radhiya Allaahu 'anhu) na kamwe hakuwaona kabisa kuswali zaidi ya Rakaa mbili zile Swalah za Rakaa nne ndani ya safari)) (Al-Bukhariy na Muslim).

Hamna umbali maalumu uliowekwa na Qur-aan au Sunnah. Kuna kauli nyingi na rai tofauti kutoka kwa Maulamaa kuhusu masafa, wengine wamesema ni maili 48 au kilomita 85 kutokana kwamba Ibn 'Umar na Ibn 'Abbaas walikuwa wakifupisha katika masafa hayo, na wengine wameonelea mwendo wa siku tatu kutokana na Hadiyth ya kuwa 'asisafiri mwanamke masafa ya siku tatu bila kuwa na Mahram wake', na wengine kutokana na kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali Rakaa mbili baada tu ya maili tatu. Ama kauli yenye nguvu ni kuwa pale popote panapojulikana katika ada ya jamii ni safari basi hupunguzwa Swalah, japo ni chini ya masafa yaliyotajwa. Na hapa haiangaliwi jinsi ya kusafiri iwe kwa mguu, mnyama, gari, treni, meli au ndege, kinachoangaliwa ni tendo la safari.


No comments: