Tuesday, December 25, 2012

~~MADHARA YA SIMU ZA MCHINA

~~MADHARA YA SIMU ZA MCHINA
(KENYA, UGANDA ZAPIGWA
MARUFUKU)~~
A/Alleykum, Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa
simu nyingi za kichina hazina viwango
vya FCC , hivyo kwa kuwa nyingi
hutengenezwa kupitia viwanda vidogo
vidogo huingizwa nchini kwa njia ya
magendo. Utafiti huu unaweza kudhibitika kwa
yafuatayo. 1. Simu nyingi hazina majina halisi,
nyingi zina chip inaitwa MTK, Spedrum,
Infineon ambazo ni chip nyepesi sana
ambazo hazihimili kiwango cha umeme
kwa siku nyingi, ndio maana simu
nyingi uganda wakati wa kuwashwa Utakuta simu inaitwa nokla, samsung,
ipone, ilimradi tu iweze kushaabihiana
na original. 2. Simu hivi zina madini hatari sana
ambayo yanaitwa li-ione ambayo
yanatengeneza muwako ambao
unaweza kuunguza au kutumika
kutengeneza mabomu. Madini hayo
huwekwa kwenye batery ya kichina ambazo sio imara kwani
zimetengenezwa kwa kuzungushia
karatasi nyepesi. 3. Viwango vya spika sio sahii kwani
vinaweza kumfanya mtu awe kiziwi
akitumia simu hizi kwa muda mrefu. 4. kwa kuwa simu nyingi zina vioo vya
touch sceen, au shika shika vioo hivi
huharibika mara kwa mara hivyo
mafundi wengi wanaotumia dawa ya
kubandua kioo na kubandika
huungua mfumo wa uvutaji hewa kwani dawa hii (soldering Paste)mafuta
haya yanasumu kali. 5. Utafiti unaonyesha Tanzania inatumia
kiasi kikubwa cha fedha za kigeni
kuagiza bidhaa mbovu za simu,
ambazo hudumu muda mfupi. 6. Simu hizi zimeongeza mianya ya
rushwa upande wa TRA na TBS kwani
ndio wanaoruhusu bidhaa hii mbovu
mbovu. 7. Imeyakatisha tamaa makampuni
makubwa yanayolipa kodi kama vile
Samsung, Nokia, Siemens, Iphone ,Sony
Ericsson kwani simu nyingi zimeigwa
kwa kutumia ujuzi wa kampuni hizi. 8. Mafundi walipa kodi na wenye vipaji
wameanza kupotea kwani kazi hii
imeonekana kudharaulika, kwa kuwa
ukitengeneza simu hizi unatengeneza
ugomvi na wateja wako kwani kila siku
matatizo hayaishi. 9. Simu hizi zinaongeza wizi wa
mitandao kwa kuwa nyingi zina chip
ambazo hazitambuliki kimataifa hivyo
kuziingiza kwenye mtandao wa
kudhibiti vyombo hivi kuwa mgumu,
kwani no. zinazotambulika ni MSID na ICCID au PIN au product Code No.
Namalizia kwa kusema basi kama
hatuwezi tuige mfano wa Kenya na
Uganda wamezipiga marufuku.....sh
ukraan Wrote by Akhiy

je mnachukuliaje suala hli ambalo tetesi zilizopo ni kwamba tanzania
nako watazifungia japo ni muda kdogo umepita,toa MAONI YAKO

No comments: