Thursday, February 7, 2013

HUKUMU YA KUSHEREKEA VALENTINE DAY

Valentine (Siku Ya Wapendanao) Na Hukumu Ya Kuisherehekea
**********************************
Allaah سبحانه وتعالى Ametuchagulia dini ya Kiislamu ambayo ndio dini ya haki na Hatokubali dini yoyote nyingine kama Anavyosema:

((وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))

((Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasirika)) [Al-'Imraan:85]

Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ametuambia kuwa kutakua na makundi katika ummah wake ambao watawafuata maadui wa Allaah سبحانه وتعالىkatika desturi na mila zao kama ifuatavyo:

((ستتبعون سنن من كان قبلكم شبراً بشبر وذراعاً بذراع حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه)) قالوا: أتراهم اليهود والنصارى؟ قال: ((فمن إذن؟)) البخاري ومسلم

((Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Hivyo nani basi mwengine?)) Al-Bukhariy na Muslim

Maneno hayo aliyoyasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakika yamesadikika kwani tunaona jinsi gani Waislamu siku hizi wanavyoigiza mila, desturi na tabia za makafiri na kuzisherehekea kama mfano siku hii inayoitwa 'Valentine day' (Siku ya Wapendanao).

Na baya zaidi na la kusikitisha sana ni kwamba sherehe hizi zinaenezwa katika njia mbali mbali za mawasiliano kama kutumiana kadi, barua pepe (e-mail), salamu katika simu za mkono. Hakika fitna hii humfanya Muislamu aharibu 'Aqiydah (Iymaan) yake kwa kudhani kuwa anafanya jambo la kawaida na hali ni jambo lisilo katika sheria ya dini yetu bali ni shirki kubwa na upotofu wa kufuata wanayoamini makafiri.

No comments: