4 – Nidhamu Zake
Tukiendelea katika mafunzo ya maamkizi ya Kiislamu na fadhila zake, tutazame nidhamu ya kuamkiana ilivyo. Tuangalie ni yupi aanze kutoa salaam? Wepi wanaofaa kutolewa salaam n.k.
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((يسلمالراكب على الماشي، والماشي على القاعد، والقليل على الكثير)) متفق عليه
وفي رواية للبخاري: ((والصغير على الكبير))
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aliyepanda (kipando) amsalimie anayetembea, anayetembea amsalimie aliyeketi na wachache wawasalimie walio wengi)) [Al-Bukhaariy na Muslim].
Na katika Riwaaya ya Al-Bukhaariy ((Mdogo amsalimie mkubwa))
Wajibu wa kumsalimia unayemjua na usiyemjua, nayo ni amali iliyo bora katika Uislamu:
عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما، أن رجلاً سأل رسول الله: أي الإسلام خير؟ قال: ((تُطْعِمُ الطَّعامَ، وتقرأُ السَّلام علـى مَنْ عَرَفْتَ ومَنْ لَـمْ تَعْرِفْ)) البخاري ومسلـم
Kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Amru bin Al-'Aasw (Radhiya Allaahu 'anhuma) amehadithia kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni amali gani katika Uislamu iliyo bora?" Akasema: ((Ni kulisha chakula na kumtolea salaam unayemjua na usiyemjua)) [Al-Bukhaariy na Muslim].
Aliye bora kabisa mbele ya Allaah ni mwenye kuanza na maamkizi, na maamkizi bora ni yale ya Kiislamu kama tulivyoona kwenye Hadiyth:
عن أبي أمامة الباهلي رضي الله عنه قال :قيل يا رسول الله صلى: رجلان يلتقيان أيهما يبدا بالسلام؟ قال: ((أَولاَهما بالله تعالى )) الترمذي حديث حسن
Kutoka kwa Abu Umaamah Al-Baahiliy (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: "Watu wawili wanapokutana ni yupi anayepaswa kuanza kutoa salaam?" Akajibu: ((Ni yule aliye mbora kwa Allaah) [At-Tirmidhiy: Hadiyth Hasan].
Inapendekezeka kurudia kutoa salaam kwa uliyekutana naye kipindi kifupi nyuma, kama vile umeingia sehemu ukatoka na kisha ukaingia tena, au mathalan kuna ukuta au mti au kizuizi chochote baina yao kimewakinga na kisha wakakutana tena, basi wanaweza kusalimiana tena kama tunavyoona katika Hadiyth ifuatayo:
عن أبي هريررة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم، قال: ((إذا لقي أحدكم أخاه، فليسلم عليه، فإن حالت بينهما شجرة، أو جدار، أو حجر، ثم لقيه، فليسلم عليه)) رواه أبو داود
Abu Hurayrah amesema kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mmoja wenu atakapokutana na nduguye amtolee salaam, iwapo watazuiwa na mti au ukuta au jiwe kisha akakutana naye basi amsalimie)) [Abu Daawuud].
Mapendekezo ya kutoa salaam unapofika katika majlisi (kikao) na pindi unapoachana na walioketi katika kikao hicho:
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إذا انتهى أحدكم إلى المجلس فليسلم، فإذا أراد أن يقوم فليسلم، فليست الأولى بأحق من الآخرة)) رواه أبو داود، والترمذي وقال: حديث حسن
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anapokomea mmoja wenu katika majlisi (kikao) atoe salaam, na atakapotaka kuondoka atoe salaam, kwani salaam ya kwanza si bora kuliko salaam ya pili)) [Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan].
Unaweza pia kumtolea salaam mwanamke ambaye ni Mahram wako na pia yule ambaye ni ajinabi (asiye Mahram wako) usipochelea fitna na wao (wanawake) wanaweza nao kutoa salaam kwa wanaume kwa sharti kama hilo:
عن سهل بن سعد رضي الله عنه قال: كانت فينا امرأة -وفي رواية: كانت لنا عجوز- تأخذ من أصول السلق فتطرحه في القدر، وتكركر حبات من شعير، فإذا صلينا الجمعة، وانصرفنا، نُسلم عليها، فتقدمه إلينا" - رواه البخاري
Kutoka kwa Sahl bin Sa'ad (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesimulia kuwa, "Kulikuwa na mwanamke" – na katika riwaaya nyingine imesema: "Kulikuwa kuna ajuza (mwanamke mwenye umri mkubwa) akichukua mizizi ya kiazisukari (cheupe) akitia sufuriani na akisaga nafaka za shayiri. Tunapomaliza kuswali Swalah ya Ijumaa na kutawanyika, tulikuwa tukimtolea salaam naye akituitikia"[Al-Bukhaariy].
وعن أم هانئ فاختة بنت أبي طالب رضي الله عنه قالت: أتيت النبي صلى الله عليه وسلم يوم الفتح وهو يغتسل، وفاطمة تستره بثوب، فسلمت، وذكرت الحديث - رواه مسلم
Ummu Haaniy Faakhitah bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Nilimuendea Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya Ukombozi wa Makkah naye anaoga na Faatwimah (binti yake) anamstiri kwa nguo, nikamtolea salaam…" akaendelea mpaka mwisho wa Hadiyth" [Muslim].
Hii ina uhusiano na Hadiyth ifuatayo:
عن أسماء بنت يزيد رضي الله عنه عنها أن رسول الله صلى الله عليه وسلم، مر في المسجد يومًا، وعصبة من النساء قعود، فألوى بيده بالتسليم. ((رواه الترمذي وقال: حديث حسن)).
Kutoka kwa Asmaa bin Yaziyd (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita msikitini siku moja kulikuwa na kundi la wanawake wameketi, akaashiria mkono wake kwa kutoa salaam" [At-Tirmidhiy na kasema Hadiyth Hasan].
Hali hii inachukuliwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alijumuisha baina ya kutamka na kuashiria na kinachotilia nguvu ni ile riwaaya ya Abu Daawuud inayosema "...akatutolea salaam" Kwa kuunganisha riwaya hizo mbili, tunapata pia faida ya kujua kuwa mtu anapoashiria ni bora afutilizie ile ishara yake kwa maneno; kama ni ishara ya kusalimia, basi na atoe salaam mdomoni mwake japo haitosikiwa na aliye/walio mbali.
Mafunzo Kutoka Katika Kisa Cha Swahaba:
No comments:
Post a Comment