SWALAH - 2 - Kusisitizwa Kwake na Malipo yake
Swalah hakika ni jambo muhimu na tukufu katika Uislamu, na uthibitisho wake ni kama ufuatao:
Swalah Ni Nguzo Ya Dini:
Hadiyth ndefu inayotoa maelezo yafuatayo:
عن
معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه (( ...ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ
وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال: ((
رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ
الجِهادُ))
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ ٌ
Kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu 'anhu) ((…Tena akasema: Je, nikwambie kilele cha hilo
jambo; nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa?)) Nikasema: Ndio ewe
Mjumbe wa Allaah. Akasema: ((Kilele chake ni Uislamu, nguzo yake ni
Swalah na sehemu yake ya juu kabisa ni Jihaad)) [At-Tirmidhiy na Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hivyo inapoanguka nguzo huanguka kile kilichojengewa nacho nayo ina maana ni dini yake mtu kwani bila ya kuswali ni kama kafiri kama tutakavyoelezea katika mada zitakazofuatia kuhusu hukmu ya mwenye kuacha Swalah.
Jambo La Kwanza Kuulizwa Mja Siku Ya Qiyaamah
((إن أول ما يحاسب به العبد يوم القيامة من عمله الصلاة ، فإن صلحت فقد أفلح وأنجح وإن فسدت فقد خاب وخسر)) التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ)
((Kitu
cha kwanza atakachohesabiwa nacho mja Siku ya Qiyaamah katika amali
zake ni Swalah, ikitengenea atakuwa amefuzu na amefanikiwa, na
ikiharibika atakuwa ameshapita patupu na amehasirika….)) [At-Tirmidhy na amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]
Bila shaka ni jambo la kumtia khofu kubwa Muislamu kupata hasara siku ya Qiyaamah kwa kuacha tu kuswali.
Wasiya Wa Mwisho Wa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Kwa Ummah Wake
Katika khutbah zake za mwisho aliwausia sana Swalah akisema:
((...الصلاة الصلاة و ما ملكت أيمانكم)) أحمد وصححه الألباني
((…Swalah, Swalah na waliomiliki mikono yenu ya kuume)) [Ahmad na ameipa daraja ya Swahiyh Shaykh Al-Albaaniy]
'Ibaadah Pekee Iliyofaradhiwa Katika Mbingu Ya Saba
Fardhi
ya nguzo ya Swalah ni ibaadah pekee aliyoipokea Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) mbingu ya saba alipokwenda safari ya Israa
Wal-Mi'raaj. Nazo zilikuwa asili yake ni Swalah khamsini kisha
zikapunguzwa hadi zikafika tano. Hivyo thawabu zake ni khamsiyn katika mizani ingawa ni tano katika kuzitekeleza.
Sifa Ya Mwanzo Na Ya Mwisho Ya Waja Watakaofuzu
Jinsi
Swalah ilivyokuwa ni muhimu na tukufu, Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
Ameanza kutaja Swalah kwa waja Wake watakaofuzu na kupata Pepo ya
Firdaws kwa kutekeleza na kudumisha Swalah.
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ ﴿1﴾ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ﴿2﴾ وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ ﴿3﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ ﴿4﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿5﴾ إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿6﴾ فَمَنِ ابْتَغَى وَرَاء ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿7﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿8﴾ وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿9﴾ أُوْلَئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ ﴿10﴾ الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿11﴾
1. Hakika wamefanikiwa Waumini,
2. Ambao ni wanyenyekevu katika Swalah zao,
3. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi
4. Na ambao wanatoa Zakaah
5. Na ambao wanazilinda tupu zao
6. Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa
7. Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.
8. Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao
9. Na ambao Swalah zao wanazihifadhi
10. Hao ndio warithi
11. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo.
[Al-Muuminuun: 1-11]
Kwa
hiyo, nani basi miongoni mwa Muumini asiyetaka kuipata Pepo ya juu
kabisa karibu na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa
sababu tu ya kuacha Swalah? Ibaadah ambayo hata dakika kumi haifiki
kuitekeleza?
No comments:
Post a Comment