Thursday, February 21, 2013

SWLLAH -3- Amri za mwanzo kwa mitume waliopita

SWALAH - 3 - Amri za Mwanzo Kwa Mitume Waliopita

Swalah ilikuwa ni amri ya kwanza hata kwa Mitume waliopita. Alipozaliwa Nabii 'Iysa (‘Alayhis Salaam) maneno ya mwanzo aliyotamka akiwa bado mtoto mchanga ni kuwa ameamrishwa Swalah:

فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا﴿27﴾يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا﴿28﴾فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا﴿29﴾قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا﴿30﴾وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا﴿31


27. Akaenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryam! Hakika umeleta kitu cha ajabu! 

28. Ewe dada yake Haaruun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. 

29. Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi? 

30. (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Allaah, Amenipa Kitabu, na Amenifanya Nabii 

31. Na Amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na Ameniusia Swalah na Zakaah maadamu ni hai.
[Maryam: 27-31]

Nabii Muusa pia alipoanza tu kupewa ujumbe, ujumbe huo ulikuwa ni ukumbusho wa Swalah

وَهَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَى﴿9﴾إِذْ رَأَى نَارًا فَقَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًالَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِقَبَسٍ أَوْ أَجِدُ عَلَى النَّارِ هُدًى﴿10﴾فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِي يَا مُوسَى﴿11﴾إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى﴿12﴾وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَى﴿13﴾إِنَّنِي أَنَا اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي﴿14

9. Na je! Imekufikia hadithi ya Muusa? 

10. Alipouona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto.

11. Basi alipoufikia akaitwa: Ewe Muusa! 

12. Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la Twuwaa. 

13. Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayofunuliwa. 

14. Hakika Mimi ndiye Allaah Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Swalah kwa ajili ya kunikumbuka Mimi.
[Twaahaa: 9-14]

Nabii Ismaa'iyl amesifiwa kwa kuamrisha watu wake Swalah

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِسْمَاعِيلَ إِنَّهُ كَانَ صَادِقَ الْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا﴿54﴾وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِ مَرْضِيًّا﴿55

54. Na mtaje katika Kitabu Ismaa'iyl. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.  

55. Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Swalah na Zakaa, na alikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa
[Maryam: 54-55]

Bila ya shaka ni ibada iliyo muhimu kupita zote kutokana na ishara kama hizo, na bila ya shaka umuhimu wake huo ni kwa ajili ya uhusiano wetu sisi waja na Mola wetu Mlezi Aliyetuumba kwa ajili ya kumuabudu Yeye pekee:

((وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُون))

((Nami Sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.)) [Adh-Dhaariyaat: 56]
 

No comments: