Tuesday, December 25, 2012

HAKI LIVE: Vyakula vya kuongeza NGUVU ZA KIUME kwa uwezo wa ALLAH inshaallah,,pata TIBA HIYO IKIWA NI SEHEMU YA KWANZA(part one)

HAKI LIVE: Vyakula vya kuongeza NGUVU ZA KIUME kwa uwezo wa ALLAH inshaallah,,pata TIBA HIYO IKIWA NI SEHEMU YA KWANZA(part one)

~~MADHARA YA SIMU ZA MCHINA

~~MADHARA YA SIMU ZA MCHINA
(KENYA, UGANDA ZAPIGWA
MARUFUKU)~~
A/Alleykum, Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa
simu nyingi za kichina hazina viwango
vya FCC , hivyo kwa kuwa nyingi
hutengenezwa kupitia viwanda vidogo
vidogo huingizwa nchini kwa njia ya
magendo. Utafiti huu unaweza kudhibitika kwa
yafuatayo. 1. Simu nyingi hazina majina halisi,
nyingi zina chip inaitwa MTK, Spedrum,
Infineon ambazo ni chip nyepesi sana
ambazo hazihimili kiwango cha umeme
kwa siku nyingi, ndio maana simu
nyingi uganda wakati wa kuwashwa Utakuta simu inaitwa nokla, samsung,
ipone, ilimradi tu iweze kushaabihiana
na original. 2. Simu hivi zina madini hatari sana
ambayo yanaitwa li-ione ambayo
yanatengeneza muwako ambao
unaweza kuunguza au kutumika
kutengeneza mabomu. Madini hayo
huwekwa kwenye batery ya kichina ambazo sio imara kwani
zimetengenezwa kwa kuzungushia
karatasi nyepesi. 3. Viwango vya spika sio sahii kwani
vinaweza kumfanya mtu awe kiziwi
akitumia simu hizi kwa muda mrefu. 4. kwa kuwa simu nyingi zina vioo vya
touch sceen, au shika shika vioo hivi
huharibika mara kwa mara hivyo
mafundi wengi wanaotumia dawa ya
kubandua kioo na kubandika
huungua mfumo wa uvutaji hewa kwani dawa hii (soldering Paste)mafuta
haya yanasumu kali. 5. Utafiti unaonyesha Tanzania inatumia
kiasi kikubwa cha fedha za kigeni
kuagiza bidhaa mbovu za simu,
ambazo hudumu muda mfupi. 6. Simu hizi zimeongeza mianya ya
rushwa upande wa TRA na TBS kwani
ndio wanaoruhusu bidhaa hii mbovu
mbovu. 7. Imeyakatisha tamaa makampuni
makubwa yanayolipa kodi kama vile
Samsung, Nokia, Siemens, Iphone ,Sony
Ericsson kwani simu nyingi zimeigwa
kwa kutumia ujuzi wa kampuni hizi. 8. Mafundi walipa kodi na wenye vipaji
wameanza kupotea kwani kazi hii
imeonekana kudharaulika, kwa kuwa
ukitengeneza simu hizi unatengeneza
ugomvi na wateja wako kwani kila siku
matatizo hayaishi. 9. Simu hizi zinaongeza wizi wa
mitandao kwa kuwa nyingi zina chip
ambazo hazitambuliki kimataifa hivyo
kuziingiza kwenye mtandao wa
kudhibiti vyombo hivi kuwa mgumu,
kwani no. zinazotambulika ni MSID na ICCID au PIN au product Code No.
Namalizia kwa kusema basi kama
hatuwezi tuige mfano wa Kenya na
Uganda wamezipiga marufuku.....sh
ukraan Wrote by Akhiy

je mnachukuliaje suala hli ambalo tetesi zilizopo ni kwamba tanzania
nako watazifungia japo ni muda kdogo umepita,toa MAONI YAKO

Vyakula vya kuongeza NGUVU ZA KIUME kwa uwezo wa ALLAH inshaallah,,pata TIBA HIYO IKIWA NI SEHEMU YA KWANZA(part one)

Assalaam alaykum,ama baada ya salamu ningependa kumshukuru Allah kwa
kunijaalia afya na kunipa uwezo wa kuweza kukutana nanyikatika makala
hii.Leo ninaongelea tatizo ambalo linawakabili wanaume weng siku hizi
,suala la kupungukiwa na nguvu za kiume ikiwa ni tatizo linaloweza
kusababishwa na upigaji wa punyeto ama utumiaji wa vyakula vyenye
kemikali nyingi,kutokana na hayo imesabisha ongezeko la wanaume wenye
matatizo hayo bila kupata ufumbuzi na kuishia kupata tiba za kienyeji
ambazo husababisha madhara na kuishia kujuta ,kwa maana hyo
ningewashauri ku2mia vyakula vifuatavyo ili kuweza kuikabili hali hyo
ya upungufu wa nguvu za kiume,...VYAKULA VYENYE KUONGEZA NGUVU ZA
KIUME:-


.1.PILIPILI-Pilipili
unaweza kula hvyo hvyo au kuchanganya kwenye chakula inasaidia sana
.
2.TIKITIKI MAJI-Tikitiki maji unaweza
kulila kama tunda au kukamua juis yake ni zuri xana

.3.PARACHICHI-Parachichi ni tunda rahisi sana kupatikana japo kuna
misimu ambayo huuzwa ghali lakini linasaidia xana katika kuongeza
nguvu za kiume
.
4.CHOKOLATE-Chocolate wengi wa wanaume huidharau na kuona kama
wanawake na watoto ndio pekee wanaostahiki kula bila ya kufahamu kuwa
ina faida kwao,hivyo inapendeza kupata japo kwa wiki mara tatu

.5.MAJI YA KUNYWA-inapendeza kunywa maji mengi kwa siku
na mtu ajitahidi anywe hata zaidi ya lita tanao kama walivyoshauri
wataalam wa mambo hayo. . . .itaendelea inshaallah kwa mawali coment
hapo na utasaidika . .. . .
NB.Epuka
kufanya zinaa na usithubutu kwani ALLAH aliyetukuka amekataza katika
Quran kwa kusema -.na wala msiikaribie zinaa.-

Monday, December 3, 2012

Friday, November 16, 2012

BMW cars......picha za magari ya BMW

maoni yako kuhusu magari hayo umeyapenda..epuka picha za ajab ajabu
chukua hzo uweke kwenye wallpaper yako

Tuesday, November 13, 2012

ISLAMIC WALLPAPERS/PATA BURE PICHA ZA KIISLAM

Kama umezipenda basi endelea kufuatilia hapa au toa maoni yako

PICHA ZA PIKIPIKI/xr pictures

umeipenda hyo,bs endelea kufuatilia

TIZAMA PICHA MBALIMBALI HAPA

write somethng

Faida za Ndizi.tunda rahisi sana kupatikana,songa nayo

Habari zenu,wazima wapenzi wafuatiliaji wa blog hii leo nimewaandalia
kwa uchache tu faida za tunda ambalo linaloitwa NDIZI.Tunda hilo ni
tunda rahisi sana kupatikana ni tunda linalolimwa sana mkoani
kilimanjaro,kagera,mbeya na maeneo mengine ya Tanzania.Tunda hili
linafaida nyingi japo limekuwa likipuuzwa na baadhi ya watu na
miongoni mwa faida za ndizi ni kama vile,kutibu magonjwa ya
moyo,saratani ya figo,kukosa choo na magonjwa ya moyo ,nawashauri sana
kutumia tunda hilo kwani wataalam wa masuala ya matunda wameshauri
sana watu kutumia tunda hilo.Jitahidi sana kuwa mnatumia tunda hilo
basi jitahidini hata mtumie mara tatu kwa wiki.Asanteni kwa kufuatilia
na mungu akijaalia katika makala ijayo ntawaletea faida za tangawizi

Sunday, November 11, 2012

Niwaomba radhi kwa yaliyotokea

---------Assallam alaykum,ndugu zangu blog imekuwa kimya kdogo kutokana na
sababu fulani fulani huku viewers wakiongezeka kwa wingi ila
inshaallah tutaendelea kuwapa makala ila msihofu kwa hilo ndugu zangu inshaallah

Thursday, October 25, 2012

Tumshukuru Allah kwa kutuwezesha kufika hapa leo tunataraji kuswali inshaallah

Assalaam alaykum,ninamshukuru Allah,ama baada ya kumshukuru Allah
ningependa nafasi hii niit kuwatakia EID EL HAJJ kwani tayari jua
limeshazama na hvyo kukichwa tutaswali inshaallah,allah atufikishe

Friday, July 20, 2012

Yah.kula daku mwezi huu wa Ramadhan,Daku unaweza kula saa yote hadi inapoingia...

Daku unaweza kula saa yote hadi inapoingia Alfajiri. Hii ni kutoka na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((..وَكُلُواْ وَاشْرَبُواْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّواْ الصِّيَامَ إِلَى الَّليْلِ...))

((…Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku…)) [Al-Baqarah: 187]

Hivyo, unaruhusiwa kula daku hadi Alfajiri ndipo unapoanza kufunga. Na hata Muadhini akiadhini na kama una tonge au fundo la maji mdomoni usiliteme, kamilisha kulimeza kisha ndio uanze kufunga. Haya yamethibiti katika Sunnah kama inavyoonyesha Hadiyth ifuatayo:

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: كان لرسول الله صلى الله عليه وسلم مؤذنان:
بلال وابن أم مكتوم .فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((إن بلال يؤذن بليل
فكلوا واشربوا حتى يؤذن ابن أم مكتوم)) متق عليه

Kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na waadhini wawili; Bilaal na Ibn Ummi Maktuum. Akasema: ((Hakika Bilaal anaadhini usiku (adhana ya mwanzo), basi kuleni na mnywe hadi aadhini Ibn Ummi Maktuum)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na Allaah Anajua zaidi

Kujihifadhi ni Miongoni mwa sifa Alizozitaja za mwanamke na si tu kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan

Kujihifadhi ni Miongoni mwa sifa Alizozitaja za Mwanamke Allaah
(Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu
zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe
shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume
zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa
waume zao, au kaka zao, au... wana wa kaka zao, au wana wa dada zao,
au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi
wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo
yaliyokhusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo
waliyoyaficha. Na tubuni nyote kwa Allah enyi Waumini, ili mpate
kufanikiwa.

Hivyo ni vyema kujisitiri wakati wote ma si tuu mwezi wa Ramadhan au siku ya ijumaa kama wafanyavyo baadh ya akina mama na akina dada

Fadhila za kuswali jamaa alfajiri na kumsabihi All mpaka jua lichomoze hasa mwezi huu Mtukufu wa RAMADHANI

عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنه قال (( من صلى الفجر في جماعة ثم قعد يذكر الله حتى تطلع الشمس ثم صلى ركعتين كانت له كأجر حجة وعمرة تامة تامة تامة) ) أخرج الترمذي صححه الألباني .

Imetoka kwa Anas kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Alfajiri katika Jama'ah kisha akakaa anamkumbuka Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) [Imetolewa na At-Tirmidhiy na kaisahihisha Al-Albaaniy]

Pindi ukifanya hivyo kwa mwezi mzima utakuwa umechuma thawabu za Hajj na 'Umrah mwezi mzima. Hizo ni fadhila za siku za kawaida, seuze ukifanya mwezi mtukufu huu wa Ramadhaan? Jitahidi ndugu Muislamu kadiri uwezavyo kuchuma hizi thawabu kubwa ambazo zingelikukalifu mali, tabu za safari na mashaka ya kufika Makkah kutekeleza ibada hizo. Lakini kwa Rahma ya Allaah Ametujaalia tuweze kuzichuma tukiwa majumbani mwetu tena kwa wepesi kabisa. Wanaume thawabu zitazidi ikiwa watatekeleza wakiwa misikitini. Wanawake wanazipata fadhila hizo hata wakiswali majumbani mwao. Hata hivyo, pamoja na ujira wote huu, tusisahau kuwa fadhila hizo hazivunji wala hazifuti fardh ya kwenda Hajj kwa mwenye uwezo, asije mtu akadhani kufanya hayo kutakuwa kumetengua wajiibu wake wa kuhiji au kufanya 'Umrah.

Saturday, July 7, 2012

Alhamdulillah neno "vunja jungu" limetokomea...ambalo hutokea kabla ya mwezi wa Ramadhani kwa kuingza watu madisko

Alhamdulillah neno "vunja jungu" limetokomea ndani ya manispaa ya morogoro kwa takriban miaka 4 sasa.
---------------------------------------
Kama tunavyofahamu kuwa inapokaribia mwezi wa ramadhan kawaida huwa kunakuwa na matangazo ya madisco na taarab ,katika matangazo hayo huwa linaandikwa neno vunja jungu.
Hii kwa mazoea kuwa mwezi wa tawba umefika hivyo watu wanakumbushwa wamalizie yale maasi kabla mwezi kuingia,au kwa lugha nyingine kuwa ni wito kwa waislaam kufanya maasi kabla ramadhan kuingia.

Na pia zinapokaribia sikukuu zetu za eid huwa matangazo kama haya yanaonekana mitaanai "disco baab kubwa la eid alhajj au eid el fitr"

Hii ni kudhalilisha dini yetu na kuikashif.

Nani wakulamiwa?

Wakulaumiwa ni manispaa idara ya matangazo ambayo inatoa ruhusa hio,kwani huruhusiwi kutoa tangazo lolote bila kuomba kibali manispaa na kulipia.

Wapili kulaumiwa ni waislam wenyewe kukaa kimya bila kudai haki yao.

Kwanini Manispaa ya morogoro imefanikiwa?

Hii ni baada ya waislam kulalamika na kuomba haki yao.

Zipi njia za kufanya ili kuipata haki hio?

Kwanza kabisa tufahamu kuwa nchi yetu si ya kiislaam na inatawalia kisheria na kanuni.

Na pia nchi yetu inadaiwa kuwa haina dini bali inaheshimu dini zote.

Pia kuifahamisha serikali kwa njia ya mdomo na maandishi kuwa hilo jambo ni tusi kwenye dini yetu hivyo kuomba msaada wa serikali kutatua tatizo hilo.

Zifuatazo ni njia sahihi za kuomba haki hizo.

1.Kuunda kamati itakayofuatilia Jambo hilo na kuhusisha taasisi za kiislam zilizopo katika eneo husika,au kuhusisha mtu mmoja mmoja kutoka kila taasisi (bakwata msiwasahau sometimes wanasave :). )

2.Kuwafahamisha wailsam juu ya qadhia hio ili waiunge mkono.

3.Kuiomba serikali (mkurugenzi wa manispaa) isaidie kupiga marufuku jambo hilo na mumfahamishe kwa njia nzuri kuwa jambo hilo ni kukashifiwa kwa dini ya kiislam.

4.Majadiliano yote yawe kwa maandishi na msikubli kujibiwa na midomo lazima kwa maandishi.na kopi ziende kwa rpc na mkuu wa mkoa.

5.Kukumbushia kila wakati majibu hayo kwani kiuzoefu hua yanachelewa sana inaweza kuchukua zaidi ya mwaka.

6.kufanya kazi hio kwa ikhlaas na kuwa na subra kwa yatakayojitokeza.

7.Kuacha kutumia jazba bila kutoa elimu ya jambo hilo kwa serikali.

Nini chakufanya baada ya kupata haki hio?

Kila inapokaribia mwezi wa ramadhan au eid niwajib kuikimbusha serikali kwa barua kuwa ramadhan au eid zinakaribia hivyo kuwakumbusha wale wote wanaokuja kuchukua kibali cha madisco wasihusishe miezi au sikukuu zetu.

Baada ya hapo kila muislam atakae ona tangazo baso ahakikishe analiondoa kwa mkono wake.

Na ushindi unatoka kwa Allah pekee

Darsa la maandalizi ya mwezi wa Ramadhani

ASSALAAMU 'ALAYKUM WARAHMATULLAAHI WABARAKAATUH

DARASA LA MAANDALIZI YA MWEZI WA RAMADHANI.

Ndg zangu ktk imaan ktk darasa letu la sehemu ya kwanza tuliangalia baadhi ya mambo kama nguzo za funga,masharti yake,sunnah zake nk:

Ktl sehemu hii ya pili tutaangalia maaswi ya viungo vyote vya mwili ambavyo vinampelekea mja ktk kuiharibu funga yake.

MAASWI YA VIUNGO.

Maswi ya viungo ni maaswi yote ya tumbo. mfano:- kula riba,kunywa kila chenye kulewesha,kula mali ya mayatima,na kila kile ambacho amekiharamisha juu m/mungu juu yake miongoni mwa vyenye kuliwa na kunywewa,na hakika amemlaani m/mungu na mtume wake mwenye kula riba na kila mwenye kusababisha juu ya kula kwake,

na amemlaani m/mungu mwenye kunywa pombe na kila mwenye kusababisha kunywa kwake mpaka mpikaji,muuzaji,mbebaji nk.

Ktk post zijazo in shaa allaah tutaangalia kiungo kimoja kimoja pamoja na maaswi yake ili tuwe navyo makini visije vikawa ni sababu ya kuharibu funga zetu. wallaahu a'alam.

Kwanini tunafunga SWAUMU,soma kwa faida

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ)) (( أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ وَأَن تَصُومُواْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ)) ((شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن
شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ))

((Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa Swawm, kama waliyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah))(([Mfunge] siku maalumu za kuhisabika. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakayefanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua)) ((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini katika mwezi huu na afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Allaah Anakutakieni yaliyo mepesi wala Hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Allaah kwa kuwa Amekuongoeni ili mpate kushukuru))

Monday, June 25, 2012

MANUFAA KATIKA NDOA

MANUFAA KATIKA NDOA

1. Kupata kizazi ambacho kwanza kitasaidia katika ujengaji wa
jamii, pili kueneza jinsia ya watu wa kila kabila au mataifa mbali
mbali, na kubwa zaidi ni kuongeza idadi ya kizazi cha jamii ya
kiislamu.

2. Kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) na Mtume Wake
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kueneza idadi ya
wafuasi wa dini ya Kiislamu.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika
hadithi sahihi:

"Oeni wake wema muwapendao na wataowapatia kizazi chema, kwani siku
ya Qiyaamah nitajivunia ukubwa wa umati wangu." [Ahmad]

3. Kupata baraka za mtoto mwema ambaye atakayemsomea dua mzee
wake (atakapofariki). Maneno haya yamethibitishwa na Hadiyth maarufu
inayosema kuwa:

"Binaadamu anapokufa, basi 'amali zake nzuri hukatika au
humalizika, isipokuwa mambo matatu makuu nayo ni: Sadaka yenye
kuendelea, Elimu yenye kunufaisha na Mtoto mwema atakayemuombea
du'aa mzee/wazee wake." [Riyadhus-Swaalihiyn]

Faida nyenginezo zipatikanazo katika ndoa ni:

4. Kinga kutokana na Shaytwaan katika mambo yanayopelekea au
yanokaribisha tendo la zinaa.

5. Utulivu wa akili na moyo na kuwa na urafiki ambao hupelekea
mapenzi na huruma baina ya mume na mke.

6. Kunganisha kwa Familia za pande mbili za ukeni na uumeni.

7. Kusaidiana katika kazi za nyumba (sio kumuachia mke kazi zote
za ndani ya nyumba). Hii ni tabia ambayo ingalipo kwa baadhi ya akina
baba. Kwa vile tabia hii imekuzwa na utamaduni wetu wa tunakotoka,
kinyume kabisa na maamrisho ya dini yetu ya Kiislamu yanavyotuagiza.

8. Kuelimishana majukumu ya kifamilia. Pia kuweka bidii na kuwa
tayari kuihami na kuitunza familia. Na vile vile kuishughulikia na
kuitimizia mahitaji yake yakiwa ama ya (kimwili, kimavazi, kisiha,
kimawazo na kiroho) na kustahamiliana pale panapotokea kutoelewana.

Wabillahi Towfiq

Sunday, June 24, 2012

Umuhimu wa kusalimiana

Ninamshukuru mwenyenzi mungu(s.w) kama anavyostahiki kushukuriwa sala na salama zimfikie mtume wake Muhamad (s.a.w) pamoja na maswahaba wake na wote wanaofata njia zake

Ndugu zangu waislamu, kusalimiana ni jambo ambalo lipo katika kila
jamii tena lilikuwepo kabla ya hata kuja Uislamu. Ulipokuja Uislamu
haukuliondoa bali ulileta matamshi yake maalumu kwa Waislamu
kusalimiana, matamshi ambayo kama yalivyothibiti katika Hadithi ni
yale yale waliyosalimiana baba yetu Aadam ('Alayhis Salaam) na
Malaika wa Ar-Rahmaan kama yalivyothibiti katika Hadithi:

"Allaah Amemuumba Aadam kwa sura yake urefu wake alikuwa dhiraa
sitini, Alipomuumba Alimwambia: Nenda ukawasalimie kikundi kile pale
miongoni mwa Malaika waliokaa na usikilize watachokuitikia nacho;
kwani hayo maamkizi watayokuitikia nayo ndio maamkizi yako na ya
vizazi vyako; Aadam akawaamkia kwa kusema: Assalaamu 'Alaykum;

Kwa nini mtume alikuwa akifunga mwezi Rajab na Shaaban kuliko miezi mingine ??soma hapa

Assalaam Alaykum
Naihusia Nafsi yangu pamoja na kuwahusia Ndugu
Zangu Waislamu Katika Kumcha Mwenyezi Mungu.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mwezi huu wa Shaabani Ni miongoni Mwa
Miezi Mitukufu wala Tusichoke kwa Kufanya Mema pamoja na Kuomba
Msamaha
kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ili kupata Maghafira toka toka Mola
(S.W.T)
Ndugu zangu Waislamu
Tuzidishe Kufunga katika Mwezi huu Mtukufu kiasi
Tutakavyoweza pamoja na Kuzidisha Kheri.
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga sana katika Mwezi huu wa Shaabani.

Ndugu zangu Katika Imaani. Katika mwezi huu wa Shaabani Mtume
(S.A.W)
Alikuwa Akifanya Ibaada Sana.
Siku moja bwana Usama bin Zaid Mola Amwilie Radhi. Alimuliza Mtume (
S.A.W)
Akasema Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu Mbona Sijakuona Unafunga Katika
Miezi Mingine kama Unavyofunga Katika mwezi huu wa Shaabani?
Mtume (S.A.W)
Akajibu Akasema Huu ni Mwezi Ulio baina ya mwezi wa Rajab na
Ramadhani.
Ni watu Wengi Hughafirika Nao. na huu ni Mwezi Ambao Amali za Waja
HUpelekwa
Kwa Mwenyezi Mungu. Basi napenda Zipelekwe Amali Zangu nikiwa
Nimefunga.

Ndugu Zangu Waislsmu Tujitahidi Nasi Tufanye Ibaada Kwa kufuata
mwendo
wa Kipenzi Chetu Mtume Muhammad (S.A.W)
Ndugu zangu Katika Imaani Tuzidishe Ibaada pamoja na Toba kwa Allah
(S.W.T)
Katika Mwezi huu Mtukufu na Hakuna Njia Ya Mkato ya Kwenda Peponi ila
ni
Kwa Kazi ngumu kujitolea katika njia za kheri.
Ndugu Zangu katika Imaani
Tumtii Mwnyezi Mungu na Mtume wake ili Tupate Kurehemewa.

ALHADITH
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga hata tukafikiria kwamba Hatafungua na
Alikuwa Alikuwa Akifungua hata Tukadhani Hatofunga tena.
Sikumuona Mtume Akitimiza Kufunga Ispokuwa Mwezi wa Ramadhani. na
Sikumuona Mtume Pia Kuzidisha Kufunga Saumu ila katika Mwezi wa
Shabaani-kasma Bibi Aisha.

Wabillahi Toufq

Tuzidishe kumcha Allah mwezi huu wa Shaabani

Assalaam Alaykum
Naihusia Nafsi yangu pamoja na kuwahusia Ndugu
Zangu Waislamu Katika Kumcha Mwenyezi Mungu.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mwezi huu wa Shaabani Ni miongoni Mwa
Miezi Mitukufu wala Tusichoke kwa Kufanya Mema pamoja na Kuomba Msamaha
kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ili kupata Maghafira toka toka Mola (S.W.T)
Ndugu zangu Waislamu
Tuzidishe Kufunga katika Mwezi huu Mtukufu kiasi
Tutakavyoweza pamoja na Kuzidisha Kheri.
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga sana katika Mwezi huu wa Shaabani.

Ndugu zangu Katika Imaani. Katika mwezi huu wa Shaabani Mtume (S.A.W)
Alikuwa Akifanya Ibaada Sana.
Siku moja bwana Usama bin Zaid Mola Amwilie Radhi. Alimuliza Mtume ( S.A.W)
Akasema Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu Mbona Sijakuona Unafunga Katika Miezi Mingine kama Unavyofunga Katika mwezi huu wa Shaabani?
Mtume (S.A.W)
Akajibu Akasema Huu ni Mwezi Ulio baina ya mwezi wa Rajab na Ramadhani.
Ni watu Wengi Hughafirika Nao. na huu ni Mwezi Ambao Amali za Waja HUpelekwa
Kwa Mwenyezi Mungu. Basi napenda Zipelekwe Amali Zangu nikiwa Nimefunga.

Ndugu Zangu Waislsmu Tujitahidi Nasi Tufanye Ibaada Kwa kufuata mwendo
wa Kipenzi Chetu Mtume Muhammad (S.A.W)
Ndugu zangu Katika Imaani Tuzidishe Ibaada pamoja na Toba kwa Allah (S.W.T)
Katika Mwezi huu Mtukufu na Hakuna Njia Ya Mkato ya Kwenda Peponi ila ni
Kwa Kazi ngumu kujitolea katika njia za kheri.
Ndugu Zangu katika Imaani
Tumtii Mwnyezi Mungu na Mtume wake ili Tupate Kurehemewa.

ALHADITH
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga hata tukafikiria kwamba Hatafungua na Alikuwa Alikuwa Akifungua hata Tukadhani Hatofunga tena.
Sikumuona Mtume Akitimiza Kufunga Ispokuwa Mwezi wa Ramadhani. na
Sikumuona Mtume Pia Kuzidisha Kufunga Saumu ila katika Mwezi wa Shabaani-kasma Bibi Aisha.

Wabillahi Toufiq

Tuzidishe kumcha Allah mwezi huu wa Shaabani

Assalaam Alaykum
Naihusia Nafsi yangu pamoja na kuwahusia Ndugu
Zangu Waislamu Katika Kumcha Mwenyezi Mungu.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mwezi huu wa Shaabani Ni miongoni Mwa
Miezi Mitukufu wala Tusichoke kwa Kufanya Mema pamoja na Kuomba Msamaha
kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ili kupata Maghafira toka toka Mola (S.W.T)
Ndugu zangu Waislamu
Tuzidishe Kufunga katika Mwezi huu Mtukufu kiasi
Tutakavyoweza pamoja na Kuzidisha Kheri.
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga sana katika Mwezi huu wa Shaabani.

Ndugu zangu Katika Imaani. Katika mwezi huu wa Shaabani Mtume (S.A.W)
Alikuwa Akifanya Ibaada Sana.
Siku moja bwana Usama bin Zaid Mola Amwilie Radhi. Alimuliza Mtume ( S.A.W)
Akasema Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu Mbona Sijakuona Unafunga Katika Miezi Mingine kama Unavyofunga Katika mwezi huu wa Shaabani?
Mtume (S.A.W)
Akajibu Akasema Huu ni Mwezi Ulio baina ya mwezi wa Rajab na Ramadhani.
Ni watu Wengi Hughafirika Nao. na huu ni Mwezi Ambao Amali za Waja HUpelekwa
Kwa Mwenyezi Mungu. Basi napenda Zipelekwe Amali Zangu nikiwa Nimefunga.

Ndugu Zangu Waislsmu Tujitahidi Nasi Tufanye Ibaada Kwa kufuata mwendo
wa Kipenzi Chetu Mtume Muhammad (S.A.W)
Ndugu zangu Katika Imaani Tuzidishe Ibaada pamoja na Toba kwa Allah (S.W.T)
Katika Mwezi huu Mtukufu na Hakuna Njia Ya Mkato ya Kwenda Peponi ila ni
Kwa Kazi ngumu kujitolea katika njia za kheri.
Ndugu Zangu katika Imaani
Tumtii Mwnyezi Mungu na Mtume wake ili Tupate Kurehemewa.

ALHADITH
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga hata tukafikiria kwamba Hatafungua na Alikuwa Alikuwa Akifungua hata Tukadhani Hatofunga tena.
Sikumuona Mtume Akitimiza Kufunga Ispokuwa Mwezi wa Ramadhani. na
Sikumuona Mtume Pia Kuzidisha Kufunga Saumu ila katika Mwezi wa Shabaani-kasma Bibi Aisha.

Wabillahi Toufiq

Thursday, June 14, 2012

KUMTEGEMEA MWENYEEZI MUNGU SUBHAANAHU WA TA'ALA:

KUMTEGEMEA MWENYEEZI MUNGU SUBHAANAHU WA TA'ALA:
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
A/Alleykum,
Kumpenda Mwenyeezi mungu na Mtume wake ni miongoni mwa mambo ya IMANI
ya Lazima, Mtu hawi Muislaam mwenye Imani mpaka atangulize mapenzi ya
Mwenyeezi mungu na mtume wake mbele ya kitu alichonacho, kiwe ni
mali,mtoto,mzazi, au watu woote, kama alivyotueleza Mtume wetu...''Na
kadri ya mapenzi ndio unapatikana UTIIFU na kufuata amri za Allah s.w.
na Mtume wake''.
Na hakika himaya ya kutafuta cha kutosheleza au kutaka utajiri vyote
vipo katika milki ya Mwenyeezi mungu, na kama alivyosema Mtume swalla
allaahu 'alayhi wa sallam ''Isiwapelekee nyinyi uzito wa kupata riziki
mkaingia katika kumuasi Mwenyeezi mungu, hazitapatikana zilizoko kwa
mwenyeezi mungu ila kwa Twaa yake'' , na hadith nyingine imepokewa
toka kwa omar bin khatwab r.a. akisema nimemsikia Mtume swalla allaahu
'alayhi wa sallam akisema ''Lau hakika nyinyi mungalikuwa mnamtegemea
Mwenyeezi mungu haki ya kumtegemea angeliwaruzuku nyinyi kama
anavyowaruzuku ndege, wanatoka asubuhi wakiwa na njaa na wanarudi
jioni wakiwa wameshiba''. Kutokana na hadithi hii inatuonyesha
TUMTEGEMEE ALLAH SUBHAANAHU WA TA'ALA Kikweli na Allah atatupa
tunalolitaka, Na aya nyingi zimekuja za kumtegemea Allah, mfano katika
suratil Huud:123...''Ni vya Mwenyeezi mungu vilivyofichika mbinguni na
ardhini na mambo yote yanarejeshwa kwake na hakuna Mola mwenye
kughafilika na mnayoyatenda''.
Pia katika suratil shuaraa:217..."Na umtegemee Mola wako mwenye nguvu
mwenye Rehema''.
Na suratil Ahzaab:3..''Na umtegemee Mwenyeezi mungu na Mwenyeezi Mungu
atosha kuwa Mlinzi''.
Na Mtume swalla allaahu 'alayhi wa sallam ameeleza kuhusu kumtegemea
Allah s.w. katika hadith aliyoipokea Abu hurarya r.a...''wataingia
peponi watu nyoyo zao ni mfano wa nyoyo za ndege''(muslim), maana yake
wanaomtegemea Mwenyeezi Mungu kwa kuwa nyoyo zao ni laini.
Hakika Allah subhaanahu wa ta'ala amewaahidi wenye kumtegemea watapata
malipo makubwa, Na hakuna kufaulu wala kupata furaha ila kwa kumuabudu
ALLAH subhaanahu wa ta'ala na kumuomba Msaada kwake yeye ndiyo mwenye
kuabudiwa kiukweli, na yeye anastahiki kuombwa msaada pekee yake.
...Inshaalah Allah s.w. atujaalie tuwe wenye KUMTEGEMEA yeye peke
yake, na tusimshirikishe na chochote.
Atujaalie ni Wenye kusikia pamoja na kufuata na atuepushe na Batili,
Na atupe Mema ya ulimwenguni na Akhera...AMIIN:

"MAMBO 10 YA KUZINGATIA KWA MMEO"

"MAMBO 10 YA KUZINGATIA KWA MMEO"

1. Unyenyekee kwake kwa Kukinai.
2. Umsikilize Mmeo na Kumtii.
3. Na uangalie Maeneo ya Macho yake na Pua yake. Yaan macho yake
yasione au Kuangalia yanayochukiza kwako mfano kaenda kizini karudi
kakukuta hujakoga nguo chafu unanuka Moshi na Mikojo ya Watoto. 4.
Hivyo basi Macho ya Mumeo yasione Au Kuangalia Yanayochukiza kwako na
wala mapua yake Yasinuse ila Harufu Nzuri kutoka Kwako.
5. Angalia sana wakati wake wa kulala Mumeo na Umpe chakula chake.
6. Kwani hakika Mbabaiko wa njaa Unaunguza na Kunaghadhibisha.
7. Chunga Mali yake na Ulinde heshima yake na Watoto wake.
8. Na matumizi ya Mali yawe Mazuri na katika kuishi Nae Upange vizuri
Maisha.
9. Usimuasi kwa Jambo lolote na Usitoe Siri Zake Mumeo nje.
10. Kwani wewe Ukikengeuka na Amri yake Utapandisha Shuki na Hasira
katika kifua chake. Na ukitoa siri Zake hutosalimika kwa kumvunjia
ahadi yake. Kisha ole wako na kufurahi hali yakuwa Mmeo hana Raha. Na
kukasirika hali ya kuwa mmeo Amefurahi!
Pia kuwa Kwake mfanyakazi nae Atakuwa ni Mtumwa wako asiyetamani
kukukosa.
Assalaam Alaykum

Photo attachment:
http://www.facebook.com/photo.php?fbid=221488311305869&set=o.229408227128973&type=1

ADABU NA SABABU ZA KUJIBIWA DUA:

ADABU NA SABABU ZA KUJIBIWA DUA:

Baadhi ya waislamu wengi hudhani dua waziombazo ni ndogo ndio maana
hawajibiwi na hudhani kuna dua kubwa kubwa ambazo mashekh huzificha
kwa ajili yao tu.
Napenda kukuzindua kuwa Allah (s.w) hujibu dua yeyote ile iwapo
itapitia misingi maalum ambayao kwayo M/Mungu hujibu dua.Misingi hiyo
ni kama ifuatayo:-
1. Mwombaji lazima awe na ikhilaswi (unyenyekevu wakati wa kuomba dua)
2.Mwombaji lazima amwombe M/Mungu peeke bila ya kumshilikisha na chochote
3.Kuhudhurisha moyo katika kuomba dua
4. Mwombaji asiwe na sharaka na haraka ya kujibiwa dua yake (awe na subra)
5.Mwombaji lazima ayatambue madhambi yake na kuomba msamaha kwayo
pamoja na kuzitambua neema na kumshukuru M/Mungu kwazo
6.Kurejesha ulichodhulumu na kutubia na kula chakula ambacho ndani
yake hakuna haramu
7.Kuwa na udhu kabla ya dua kama hilo ni jepesi kwako
8.Kuelekea Qibla wakati wa kuomba kama inawezekana
9.Kuanza kwa kumsifu M/Mungu kwa sifa zake na kumswalia Mtume (s.a.w)
mwanzo na mwisho wa dua.
10.Mwombaji lazima awe ni mwenye kuamrisha mema na kukataza mabaya
11.Maombi yasiwe ya maovu au kukata udugu
Inshallah tukizingatia hayo na mengine mengi mazuri yaliyofundishwa
katika uislamu na imaani dua zetu zitajibiwa.

Mwenyezi Mungu anasema tujitolee nafsi zetu kwa ajili yake

Mwenyezi Mungu anasema
Na ktk ishara zake Mwenyezi Mungu (kuonyesha hisani yake) amekuumbieni
kutokana na nafsi zenu wanawake ili mpate UTULIVU kwao. Na akaweka
baina yenu mapenzi na huruma kwa hakika katika haya kuna alama kwa
watu wanaotafakari. Wewe vipi umempata mke halafu unautafuta utulivu
kwenye bao? Au unaupata utulivu kwenye kusoma magazeti yalio jaa:-
1. Habari ýa vita
2. Habari za maafa
Umepotea ndugu khazina ya utulivu anayo mkeo
Funguka

Na watu wanafanya mambo kwa kujiona wao ni wabora sana hebu soma hapa kwa maelezo zaidi

اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ
سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن
ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ
أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ
إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ
يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

"Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Aliye hai, Msimamiaji wa
mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee
vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele
yake bila ya idhini Yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma
yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi Wake, ila kwa
atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala
haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye Aliye juu, na ndiye Mkuu."

Al-Baqarah – 255

JE MNAJUA MAANA YA KUMSENGENYA MTU?? soma hapa kwa maelezo zaidi

عَنْ أَبِى هُرَيْرَةَ رَضِىَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُوْلَ اللهِ صَلَّى
اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم قَالَ:أَتَدْرُوْنَ مَاالْغِيبَةُ؟قَالُوا:اللهُ
وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ:قَالَ ذِكْرُكَ أَخَاكَ
بِمَايَكْرَهُ.قَالَ:أَفَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِى أَخِى
مَاأَقُوْلُ.قَالَ:إِنْ كَانَ فِيْهِ مَاتَقُوْلُ فَقَدِ
اُغْتَبْتَهُ,وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيْهِ فَقَدْ بَهَتَّهُ)أَخْرَجَهُ
مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abii huraira Radhwi za M/mungu ziwe juu yake,Amesema Mtume
wa M/mungu rehma na amani ziwe juu yake.
Hivi mnamjua msengenyaji?,wakajibu maswahaba "M/mungu na mtume wake
ndio wenye kujua"
Akasema Mtume,kusengenya ni kumtaja ndugu yako wakati hayupo kwa yale
yanayo mkera.maswahaba wakauliza, "Jee ikiwa yale tunayomzungumzia ni
ya kweli?" akasema tena mtume "hata ikiwa mnayomzungumzia ni ya
kweli mtakuwa mmemsengenya,na hata kama mnayomzungumzia hana basi
utakuwa umemsengemya.
Imepokelewa na imamu muslim

UMUHIMU WA KUTOA KWA AJILI YA ALLAH

‫Imetoka kwa Abu Hurairjq رضي الله عنه amesema: Mtume صلى الله عليه
وآله وسلم amesema: ((Kila 'amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara
kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba hadi Atakavyo
Allaah…)). [Ahmad].

Na hii ndio maana Anasema Allaah سبحانه وتعالى katika Aayah nyingine
kuwa mtu anapotoa mali yake kwa ajili Yake ni kama mfano amemkopesha
Allaah سبحانه وتعالى mkopo mzuri ambao malipo yake ni kuzidishiwa
zaidi ya hiyo mali aliyoitoa, kisha juu yake ni kupata ujira mwema
kutoka kwa Mola wake Mtukufu. Ni muhimu kujua kuwa Yeye Mwenyewe
Allaah سبحانه وتعالى Ndiye Anayeturuzuku hiyo mali, kisha Anatutaka
tumkopeshe katika hicho alichotupa ili Atulipe zaidi ya Aliyoturuzuku
kabla. Basi nani atakayesita kutoa mkopo kumkopesha Mola wake kwa
kutegemea malipo kama hayo?

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

((مَن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضاً حَسَناً فَيُضَاعِفَهُ لَهُ
وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ))

((Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mwema, ili Amrudishie
maradufu, na apate malipo ya ukarimu)) [Al-Hadiyd: 11]

Kutoa mali kwa fiy Sabili-Allaah ni jambo lenye kutaka kuazimiwa
kikweli kwani hakuna asiyependa kumiliki mali. Na wakati wa kutoa mali
shaytwaan husimama haraka kumtia wasiwasi binaadamu asitoe mali yake.
Unapofika wakati huo basi ndugu Muislamu kumbuka kuwa thawabu zake ni
nyingi mno na nzito mbele ya Allaah na ndio maana tunaona kwamba
Allaah سبحانه وتعالى Ametanguliza mali kabla ya nafsi katika kuhimiza
kufanya jihaad fiy Sabiyli-Allaah:

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَى تِجَارَةٍ
تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ))

((تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ
بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ
تَعْلَمُونَ))

((يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن
تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ
ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))

((Enyi mlioamini! Nikuonyesheni biashara itakayokuokoeni na adhabu
iliyo chungu?))

((Muaminini Allaah na Mtume Wake, na piganeni Jihaad katika Njia ya
Allaah kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi
mnajua))

((Atakusameheni dhambi zenu, na Atakutieni katika Mabustani yapitiwayo
na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele.
Huko ndio kufuzu kukubwa)) [Asw-Swaff: 10-12].

Vile vile:

((إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ
ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي
سَبِيلِ اللَّهِ أُوْلَئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ))

((Hakika Waumini ni wale walio muamini Allaah na Mtume Wake tena
wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihaad katika Njia ya Allaah kwa
mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli)) [Al-Hujuraat: 15].

Kama tunavyoona katika Aayah hizo za juu kwamba Allaah Anatupa nguvu
kutoa mali fiy Sabili-Allaah kwa kutuhakikishia kuwa kutoa ni kufanya
biashara Naye ambayo matokeo yake ni kupata faida nyingi na juu ya
hivyo ni kupata maghfira kutoka Kwake:

((إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ
وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ
تِجَارَةً لَّن تَبُورَ))

((لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ
غَفُورٌ شَكُور))

((Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalah, na
wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika Tulivyowaruzuku, hao hutaraji
biashara isiyododa [isiyoanguka]))
((Ili Yeye Awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na Awazidishie kutokana na
fadhila Zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani))
[Faatwir: 29-30]

"Enyi watu! Mcheni Mola wenu, hakika mtetemeko wa...

"Enyi watu! Mcheni Mola wenu, hakika mtetemeko wa...
To: UTAMU WA NDOA <229408227128973@groups.facebook.com>

Hassan Kibari posted in UTAMU WA NDOA

"Enyi watu! Mcheni Mola wenu, hakika mtetemeko wa Kiama ni jambo kubwa
kabisa. Siku mtakapokiaona hicho kiama kila mwanamke anyonyeshaye
atamsahau amnyonyeshaye na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake (kabla
ya wakati) tena kwa uchungu.Utawaona watu wamelewa hali ya kuwa
hawakulewa. Lakini ni adhabu ya Mwenyezi Mungu tu hiyo iliyo kali
kabisa" (22:1-2).
Siku hii nzito kabisa Allah subuhana wataalah ameipa majina mengi
katika Quran mimi nitayataja machache:-
1. YA UMUL-QIAMA- Siku ya kiama
2.ASSAA - Saa
3.AL-WAQIA -Tukio la uhakika
4.AL-HAAQA - Tukio la kushitukiza
5.AL-QARIA - Msiba wenye kugonga nyoyo
6.ASWAAKHA - Sauti kali yenye kuumiza nyoyo za wanadamu
7.ATWAMMATUL-KUBRA- Balaa iliyo kubwa kabisa
8. YA UMUDDIN - Siku ya malipo
9.YA UMUL-HISAAB - Siku ya kuhesabiwa
10. YA UMUL-JAMII - Siku ya kukusanywa
11. YA UMUL-TAGHAABUN - Siku ya khasara
12. YA UMUL-FASIL - siku ya hukumu
13. YA UMUL- ADHIIM - Siku iliyo nzito kabisa

Inshallah Allah (s.w) atunusuru.

Hassan Al-Basriy aliulizwa ameupata vp ucha Mungu...

Hassan Al-Basriy aliulizwa ameupata vp ucha Mungu...
To: UTAMU WA NDOA <229408227128973@groups.facebook.com>

Halima Al-Amin posted in UTAMU WA NDOA

Hassan Al-Basriy aliulizwa ameupata vp ucha Mungu na utulivu wa nafsi
yake? Akajibu kwa kusema:
1. NAJUA kila nifanyalo ALLAH ANANIONA. Hili hunifanya niogope kufanya maasia.
2. Sipapariki moyo kwani NAJUA RIZKI yangu hakuna atakaeichukua ALLAH
keshaniandikia.
3. NAJUA hakuna atakaenifanyia IBADA zangu lazima nifanye mwenyewe.
4. NAJUA ntakutana na KIFO wakati wowote hivyo lazima NIANDAE zawadi
zitumikazo akhera.
Jee sisi tunayazingatia haya??Funguka

SWALI: Je, Shirki ipo kwa Waislamu?

SWALI: Je, Shirki ipo kwa Waislamu?

JIBU: Ndio, ni masikitiko kuwa ipo tena nyingi'

DALILI KUTOKA QUR-AAN:(وما يؤمن أكثرهم بالله إلا وهم مشركون)

Na wengi katika wao hawamuamini Allaah pasina kuwa ni washirikina. (Yuwsuf: 106

DALILI KUTOKA HADIYTH :(لاتقوم الساعة حتى تلحق قبائل من أمتي بالمشركين
وحتى تعبد الأوثان )

Qiyaamah hakitosimama mpaka kutafika wakati watu wa baadhi ya makabila
katika ummah wangu wataungana na washirikina na hadi watakapoabudu
asiye Allaah!

ASSALAAM ALAYKUM SOMA KISA HIKI

ASSALAAM ALAYKUM

KISA:

Swahaba aliyeitwa Julaybiyb alijulikana sana kuwa alikuwa ni mtu duni
asiyemiliki mali na hakuwa ni mzuri kwa sura na umbo, na alikuwa ni
mtu wa kuchekesha watu. Kwa hivyo hakuna aliyetaka kumuozesha binti
yake. Mtume (S.A.W) alimuuliza Julaybib kama anataka kuoa, naye
akamjibu: "Ewe Mjumbe wa Allah, nani atakayekubali nimuoe mimi?

Sina nyumba wala mali wala chochote katika mapambo ya dunia".
Mtume (S.A.W) akamtuma mtu mmoja aende nyumba ya Answaariy fulani
ambao walikuwa ni familia yenye kujulikana kwa kabila lao maarufu
kubwa lenye kujulikana kwa heshima na wenye hali nzuri. Alipopiga
hodi, alifungua mlango mama wa binti huyo. Swahaba akamjulisha kuwa
ametumwa na Mtume kuleta posa kwa binti yake.

Mama huyo alifurahi sana kudhania kwamba Mtume (S.A.W) ndiye anayetaka
kumposa binti yake. Swahaba Alipomjulisha kuwa sio kwa ajili ya Mtume
(S.A.W) bali ni kwa ajili ya Julaybiyb, mama huyo alisema: "Nani?
Julaybib? Hapana! Hatumuozeshi yeye binti yetu!".

Mara yule binti alisikia mazungumzo hayo akaja kuuliza vizuri: "Nani
anayetaka kuniposa?" Mama mtu akamuelezea kuwa Mtume (S.A.W) amemtuma
mtu aje kumposa yeye kwa ajili ya Julaybiyb.

Binti huyo alimwambia mama yake: "Vipi mama unakataa amri ya Mtume
(S.A.W) Fuata amri yake kwani hakuna kitakachonidhuru". (Katika usemi
mmoja ni kwamba hapo hapo Aayah ifuatayo iliteremshwa [Ibnu Kathiyr
7:692-694]) na katika usemi mwingine aliwaambia wazazi wake:
"Hamkusikia kauli ya Allah (S.W)

(وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ
وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ
وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا)

(Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari
katika jambo, Allah na Mtume Wake Wanapokata shauri katika jambo lao.
Na mwenye kumuasi Allah na Mtume Wake basi hakika amepotea upotofu
ulio wazi)[Al-Ahzaab:36]

Ikabidi wamuozeshe binti yao kwa Julaybiyb. Kisha katika vita fulani
alitoka Mtume (S.AW) na Maswahaba miongoni mwao ni Julaybiyb na baada
ya ushindi wa vita hivyo, Mtume (S.A.W) aliwauliza Maswahaba kabla ya
kurudi: (Je, kuna mtu aliyekosekana?)
Wakataja baadhi ya Maswahaba waliokosekana kisha Mtume (S.A.W)
akawauliza tena wakasema: "Hakuna mtu mwingine aliyekosekana: Lakini
Mtume (S.A.W) akasema: (Lakini mimi naona kwamba Julaybiyb
amekosekana) yaani hayupo na sisi.

(Nendeni mkamtafute miongoni mwa waliouliwa). Wakaenda Maswahaba
kumtafuta wakamkuta ameuawa akiwa karibu yake makafiri saba ambao
aliwahi kuwaua yeye Julaybiyb. Maswahaba wakamjulisha Mtume (S.A.W)
ambaye alikwenda na kusimama karibu naye kisha akasema: (Ameua saba
kisha wakamuua. Yeye ni wangu na mimi ni wake).

Alisema hivyo mara mbili au tatu, kisha Mtume (S.A.W) akambeba kwa
mikono yake na kwenda kumzika. Na akamuombea Du'aa mke wake:

(الَّلهُمَّ، صَبَّ عَلَيْهَا [الخير] صَبَّا، وَلاَ تَجْعَل عَيْشَها كَدَّا)

(Ewe Allah, Mjaze kheri (nyingi) zilizojaa na Usimjaaliye maisha yake
kuwa ni ya shida [tabu na mashaka]

Imesemekana kwamba hakuweko mjane aliyekuwa ana maisha mema kama
maisha ya mke wa Julaybiy (R.A)

[Kisa kimesimuliwa na Imaam Ahmad Muslim na An-Nasaaiy]

Ndugu waislamu Kisa Hiki kimetufunza nini? wewe Binafsi. Funguka:

Wednesday, June 13, 2012

SWALI: Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah?



3:29pm Jun 10
SWALI: Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah?
JIBU: Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى.
(ذلك بأن الله هو الحق وأن مايدعون من دونه الباطل )

Hivi ni kwa sababu hakika Allaah ndiye wa kweli, na hakika wanachokiomba ni cha uongo. (Luqmaan: 30)

(من قال لا إله إلا الله وكفر بما يعبد من دون الله حرم ماله ودمه )

Atakayesema 'Laa ilaaha illa Allaah na akawapinga wanaoabudiwa wasio Allaah italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai(.

SWALI: Nini maana ya Tawhiyd katika sifa za Allaah SWA.?
JIBU: Kuthibitisha alivyojisifu Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى au alivyosifiwa na Mtume wake.

) ليس كمثله شيء وهو السميع البصير)

Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. (Ash-Shuwraa: 11)

(ينزل ربنا تبارك وتعالى في كل ليلة إلى السماء الدنيا)

Mola wetu Huteremka kila usiku katika mbingu ya dunia.

SWALI: Nini faida ya Tawhiyd kwa Muislamu?
JIBU: Kupata Hidaaya duniani na kuwa katika amani Akhera.

(الذين أمنوا ولم يلبسوا إيمانهم بظلم أولئك لهم الأمن وهم مهتدون )

Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakaopata amani na wao ndio walioongoka. (Al-An'aam: 82)

( حق العباد على الله أن لايعذب من لا يشرك به شيئ )

Haki ya mja kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى (Anayomfanyia) kuwa Hamuadhibu yule asiyemshirikisha Yeye na chochote.

View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.

Hakika Katika Jambo ambalo ni Muhimu kwa Mme...





Hakika Katika Jambo ambalo ni Muhimu kwa Mme kulichunga na kulilinda ni Kumchezea Chezea mke Wake na Haswa kabla ya Kumingilia,
Hili Linaathari kubwa sana Kati ya WanandoaWawili katika Mahusiano yao ya Kiroho
na Ya Kijinsi.
Katika Kufikia Kilele cha Raha ya Kiwiliwili kunahitaji kwa Mwanamme awe na
Diplomasia ili aweze Kumpa Mke wake Hamu na Matamanio ya Kweli,
na Ushiriki Mzuri ulio kamili na Mapenzi Yaliyokita.

Mke Akiwa Mwenye Hekima ANaweza Kwa Diplomasia aliyokuwa nayo ya
Mapambo yake na Usafi wa Kiwiliwili chake Kumvuta Mume wake na Kumtamanisha.
Hivyo basi kumhimiza katika kuwasiliana kwa Viwili wili vyao kwa Urahisi na Wepesi
Zaidi, Mahaba Siku Zote yanatimiza Furaha,


Pia tendo la kubusu lina Athari Muhimu sana katika Mapenzi ya Mdoa na Hukurubisha zile Hisia za Mapenzi na Mwisho na Mwisho Hupelekea Kugandana kwa Kiwiliwili,
Busu Nalo lina Umuhimu wake Busu nalo Linatakiwa Liwe katika Hali Nzuri lenye Kusisimua. na Hasa Linapokuwa ni
Mdomo kwa Mdomo Hali yakuwa Wanandoa Wanapokuwa Wamefumba Macho
Mawili na Kufungua kidogo kidogo Mara kwa mara.

Wakati huo wakati Huo Inapokuwa
Miili yao Imegandana na Pumzi Kubadilishana hali Zikiwa Moto moto, Ukianzia Kuvuta
Kwa ndani kabisa na Macho yenu yakiwa yanaangaliana kwa Huruma. Yote Haya
Huzipa Raha Nafsi za Wanandoa na ni Vitangulizi vizuri kwa Kutayarisha Mazingira
Mazuri ya Kuanza kwa Jimai.

Busu lilivyo na Umuhimu Hata Mtume S.A.W Alikuwa Akiwabusu Wake zake Na
Alikuwa haachi Kuwabusu Wake Zake Hata kama Amefunga Saumu.
Kwan Alikuwa Akiwabusu na Akiwakumbatia Wake zake Hali Yakuwa Amefunga"
(Bukhari na Muslim) Ummu Salama r.a Amesema Hakika Mtume wa Allah Alikuwa
Akiwabusu Wake zake Hali ya kuwa Amefunga


.


Hakika Katika Jambo ambalo ni Muhimu kwa Mme...

.


2:07am Jun 11
Hakika Katika Jambo ambalo ni Muhimu kwa Mme kulichunga na kulilinda ni Kumchezea Chezea mke Wake na Haswa kabla ya Kumingilia,
Hili Linaathari kubwa sana Kati ya WanandoaWawili katika Mahusiano yao ya Kiroho
na Ya Kijinsi.
Katika Kufikia Kilele cha Raha ya Kiwiliwili kunahitaji kwa Mwanamme awe na
Diplomasia ili aweze Kumpa Mke wake Hamu na Matamanio ya Kweli,
na Ushiriki Mzuri ulio kamili na Mapenzi Yaliyokita.

Mke Akiwa Mwenye Hekima ANaweza Kwa Diplomasia aliyokuwa nayo ya
Mapambo yake na Usafi wa Kiwiliwili chake Kumvuta Mume wake na Kumtamanisha.
Hivyo basi kumhimiza katika kuwasiliana kwa Viwili wili vyao kwa Urahisi na Wepesi
Zaidi, Mahaba Siku Zote yanatimiza Furaha,


Pia tendo la kubusu lina Athari Muhimu sana katika Mapenzi ya Mdoa na Hukurubisha zile Hisia za Mapenzi na Mwisho na Mwisho Hupelekea Kugandana kwa Kiwiliwili,
Busu Nalo lina Umuhimu wake Busu nalo Linatakiwa Liwe katika Hali Nzuri lenye Kusisimua. na Hasa Linapokuwa ni
Mdomo kwa Mdomo Hali yakuwa Wanandoa Wanapokuwa Wamefumba Macho
Mawili na Kufungua kidogo kidogo Mara kwa mara.

Wakati huo wakati Huo Inapokuwa
Miili yao Imegandana na Pumzi Kubadilishana hali Zikiwa Moto moto, Ukianzia Kuvuta
Kwa ndani kabisa na Macho yenu yakiwa yanaangaliana kwa Huruma. Yote Haya
Huzipa Raha Nafsi za Wanandoa na ni Vitangulizi vizuri kwa Kutayarisha Mazingira
Mazuri ya Kuanza kwa Jimai.

Busu lilivyo na Umuhimu Hata Mtume S.A.W Alikuwa Akiwabusu Wake zake Na
Alikuwa haachi Kuwabusu Wake Zake Hata kama Amefunga Saumu.
Kwan Alikuwa Akiwabusu na Akiwakumbatia Wake zake Hali Yakuwa Amefunga"
(Bukhari na Muslim) Ummu Salama r.a Amesema Hakika Mtume wa Allah Alikuwa
Akiwabusu Wake zake Hali ya kuwa Amefunga


.