KUMTEGEMEA MWENYEEZI MUNGU SUBHAANAHU WA TA'ALA:
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
A/Alleykum,
Kumpenda Mwenyeezi mungu na Mtume wake ni miongoni mwa mambo ya IMANI
ya Lazima, Mtu hawi Muislaam mwenye Imani mpaka atangulize mapenzi ya
Mwenyeezi mungu na mtume wake mbele ya kitu alichonacho, kiwe ni
mali,mtoto,mzazi, au watu woote, kama alivyotueleza Mtume wetu...''Na
kadri ya mapenzi ndio unapatikana UTIIFU na kufuata amri za Allah s.w.
na Mtume wake''.
Na hakika himaya ya kutafuta cha kutosheleza au kutaka utajiri vyote
vipo katika milki ya Mwenyeezi mungu, na kama alivyosema Mtume swalla
allaahu 'alayhi wa sallam ''Isiwapelekee nyinyi uzito wa kupata riziki
mkaingia katika kumuasi Mwenyeezi mungu, hazitapatikana zilizoko kwa
mwenyeezi mungu ila kwa Twaa yake'' , na hadith nyingine imepokewa
toka kwa omar bin khatwab r.a. akisema nimemsikia Mtume swalla allaahu
'alayhi wa sallam akisema ''Lau hakika nyinyi mungalikuwa mnamtegemea
Mwenyeezi mungu haki ya kumtegemea angeliwaruzuku nyinyi kama
anavyowaruzuku ndege, wanatoka asubuhi wakiwa na njaa na wanarudi
jioni wakiwa wameshiba''. Kutokana na hadithi hii inatuonyesha
TUMTEGEMEE ALLAH SUBHAANAHU WA TA'ALA Kikweli na Allah atatupa
tunalolitaka, Na aya nyingi zimekuja za kumtegemea Allah, mfano katika
suratil Huud:123...''Ni vya Mwenyeezi mungu vilivyofichika mbinguni na
ardhini na mambo yote yanarejeshwa kwake na hakuna Mola mwenye
kughafilika na mnayoyatenda''.
Pia katika suratil shuaraa:217..."Na umtegemee Mola wako mwenye nguvu
mwenye Rehema''.
Na suratil Ahzaab:3..''Na umtegemee Mwenyeezi mungu na Mwenyeezi Mungu
atosha kuwa Mlinzi''.
Na Mtume swalla allaahu 'alayhi wa sallam ameeleza kuhusu kumtegemea
Allah s.w. katika hadith aliyoipokea Abu hurarya r.a...''wataingia
peponi watu nyoyo zao ni mfano wa nyoyo za ndege''(muslim), maana yake
wanaomtegemea Mwenyeezi Mungu kwa kuwa nyoyo zao ni laini.
Hakika Allah subhaanahu wa ta'ala amewaahidi wenye kumtegemea watapata
malipo makubwa, Na hakuna kufaulu wala kupata furaha ila kwa kumuabudu
ALLAH subhaanahu wa ta'ala na kumuomba Msaada kwake yeye ndiyo mwenye
kuabudiwa kiukweli, na yeye anastahiki kuombwa msaada pekee yake.
...Inshaalah Allah s.w. atujaalie tuwe wenye KUMTEGEMEA yeye peke
yake, na tusimshirikishe na chochote.
Atujaalie ni Wenye kusikia pamoja na kufuata na atuepushe na Batili,
Na atupe Mema ya ulimwenguni na Akhera...AMIIN:
No comments:
Post a Comment