MAFUNGU (MAKUNDI) MATATU YA WAOMBAJI DUA NA MATOKEO YAKE.
Ndugu muislamu waomabaji dua wamegawanyika makundi matatu:
i/.Wapo ambao huomba na kujibiwa moja kwa moja
ii/. Wapo ambao huomba na hawajibiwi
iii/.Kundi la tatu limegawanyika sehemu kuumbi:
(a). Moja ni lile lisilofanikiwa kwenye maombi na hufanikiwa kwenye shiriki
(b). Pili ni lile ambalo halifanikiwi kwenye shiriki wala kwenye maombi
Kundi la kwanza hili ni la Wacha-Mungu ambao hawa dua zao hujibiwa haraka kutokana na Ucha-Mungu waliokuwa nao. Hawa M/Mungu hana hasira nao kwa hiyo huwapa waliombalo na Allah (s.w) huwapenda kwani wamemjua na kumpa haki yake sitahiki na wanaitwa Mawalii wa Allah.
" Bila shka rehema za Mwenyezi Mungu ziko karibu sana na wale waja wake wafanyao mema" (Aaraf:56).
Pia katika hadithi iliyopokelewa na Anas (r.a) anasimulia kuwa Mtume (s.a.w) alisema M/Mungu anasema kama mja wangu anisogeleapo kwa kiasi cha futi moja, mimi (Allah) namsongelea kiasi cha yadi moja na anaponisogelea kwa kiasi cha yadi moja mimi (Allah) namsongelea kwa kiasi cha mikono miwili iliyonyooshwa na anisogeleapo akiwa natembea nami (Allah) namsogelea nikiwa nakimbia (Bukhari) .
Kundi la pili ni lile ambalo halijibiwi hata liombe kwa vile limeghadhibikiwa na Allah kutokana na maasi wayatendayo. Ni kama ilivyo kwa mzazi hawezi kuwa na mapenzi na mtoto asiyekuwa mtiifu kwake.
Haya anayathibitisha Allah (s.w) katika kitabu chake kitukufu kuwa:
"Na atakayefanya ubaya, basi hawatalipwa wale wafanyao ubaya ila yale waliokuwa wakiyafanya" (Qasas: 84).
Pia katika surat Ruum Allah (s.w) anaendelea kusema kuwa:
"Anayekufuru madhara ya kufuru yake ni juu yake mwenyewe. Bila shaka yeye hawapendi makafiri" (Ruum:45).
Kundi la tatu ambalo limegawanyika katika sehemu mbili ufananuzi wake ni kama ifuatavyo:
Kundi lifanikiwalo kwenye kufru. Hapa shetani anawacheza shere tu yeye huwapelekea misukosuko nay eye mwenyewe huwaondolea pindi tu wafanyapo kufru ili kumridhisha yeye katika lengo la ke la kuwakufrisha wanadamu kama alivyochukuwa ahadi kwa Allah (s.w) pale alipofukuzwa katika rehhema zake. Mfano mtu aliyerogwa kuaguliwa kwa njia ya uchawi, hata kama uchawi utaondoka itakuwa ni haramu kwa vile uchawi ni amali ya shetani. Haiwezekani uaguliwe kwa njia ya uchawi ni lazima kuwe na makubaliano baina ya uchawi na kiaguzi ( Uchawi ni shetani na kiaguzi ni shetani). Siyo mapambano kama vile tiba ya Ruqya za kisheria (Quran) ndio maana yeyote aliyeaguliwa ucahwi kwa njia ucahwi lazima alazimishwe kuvaa hirizi, kutundika tarasimu na mengine kam hayo.
Katika kundi hili la tatu sehemu ya pili ni wale ambao hawafanikiwi kwa Allah nakwe4nye kufru, Ni kwamba M/Mungu hana ubia na wala shetani hatki ubia. Mwenye kumtegemea M/Mungu pekee Allah (s.w) atamkidhia haja zake lakini kwa mashariti ya kumtegemea yeye pekee. Hachanganywi na chochote katika utendaji wake na akichanganywa na chochote yeye hukaa pembeni. Kwani haki na batili havikai pamoja kama anavyo bainisha Allah (s.w) katika sulatu Baqarah.
"Basi anayemkataa shetani na akamwamini Mwenyezi Mungu, bila shaka yeye ameshikilia kishiko chenye nguvu kisicho vunjika, Na Menyezi Mungu ndiye asikiaye na mjuzi,.Mwenyezi Mungu ni mlinzi wa wale walioamini, lakini waliokufuru walinzi wao ni mashetani huwatoa katika mwangaza na huwaingiza kwenye giza.Hawo ndio watu wa motoni, humo wataka milele" (Baqarah:256-257).
Katika aya nyingine Allah (s.w) anabainisha kuwa shetani hana nguvu zozote za kukusaidia chochote.
" Nani huyo awezaye kuombea mbele ya Allah iba idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na yaliyo nyuma yao. Wala hawo viumbe (mashetani) hawalijui lolote katika yaliyo kwenye ilimu yake Allah ila kwa alipendalo yeye" (Baqarah :255),
Kati ya Allah na shetani, Allah ndiye mwenye mamlaka ya kweli, lakini shetani naye anajipa mamlaka kwa hiyo hawa hawakubaliani hata kidogo kila mmoja ana lake,.Basi ukimshika Allah shetanai anakususia na ukimshika shetan Allah anakususia.
Haiwezekani upatwe na misukusuko kasha utumie njia za kishirikina kuondosha na mara baada ya shetani kutumikia kwa lengo la kukufurisha ili uingie motoni mara unaonekana ukifunga ramadhani na kusali n akufanya mema mengine ambayo shetani hayapendi atakuona unamvurugia lengo lake hivyo hutafanikiwa katika yale uliyoyaomba kwa njia za kishirikina.
Vile vile leo uko kwa shetani kesho uko kwa Mwenyezi Mungu naye hakubali kukukidhia haja zako kwa vile una Mungu mwingine. Kwa maana hiyo kundi hili linashindwa kufanikiwa pande zote kutokana na hao wanao wategemea hawana ubia.
Inshallah Allah akitupa wasaa tutaongelea nyakati na hali ambazo ndani yake dua hujibiwa moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment