Siku chache baada ya UVCCM kudai kuwa uamsho wamo serikalini, taasisi hiyo ya Uhoams imeibuka na kujibu hoja hizo kama ifuatavyo:
---------
Tunawajibu Stiphen Wasira na UVCC
Jana tulisikia kauli zenu na mkasema Uwamsho wapo Serikali, sisi tunayakubali maneno yenu na tunakiri kuwa ni kweli Muamsho wapo Serikalini.
Nyinyi mmeshindwa kuwataja kwa majina sisi tutawataja kwa majina na vyeo vyao.
...
Muamsho wa kwanza ni Kikwete, yeye ametuamsha na ametwambia wazi Wazanzibar kuwa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba haitoratibu Muungano hivyo ametuamsha na kutueka bayana Wazanzibar kuwa Tume haituhusu, sisi Wazanzibar kinachotuhusu kwenye Katiba ni Muungano hivyo katuamsha kuwa Tume hii ya Katiba si ya Muungano.
Kikwete huyo huyo ametwambia kuwa Muungano ushavunjwa na CCM NEC, na alisema NEC imeshaamuwa kuwa Rais wa Zanzibar asiwe Makamu wa Rais wa Muungano, hivyo ametuamsha kuwa NEC imeenda kivyume na Hati ya Muungano na kwenda kivyume na makubaliano ni kuyavunja makubaliano, hivyo NEC imeuvunja Muungano.
Muamsho Mkubwa ni Pinda nae ametuamsha pakubwa tena akatutowa kwenye usingizi mzito pale alipotwambia kuwa Zanzibar si Nchi na alipoambiwa ni nchi amekosea akasema sijakosea wala sijalewa Zanzibar si nchi, ametuamsha pakubwa Pinda.
Muamsho mwengine ni Nyerere alitwambia amechoka na sisi Wazanzibar na hapa namnukuu "tumechoshwa na Wazanzibar na Uislaam" kama si Muamsho nani?
Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, yey katuachia uswiya na alitwambia Muungano kama koti likikubana livuwe nae pia ni Muamsho.
Muamsho mwengine ni Mansour Yussuf Himid nae katuamsha sihaba pale aliposema ndani ya Baraza la Wawakilishi kuwa Serikali moja hataki kuisikia, mbili ni butu, anataka Serikali tatu au vyenginevyo.
Amani Karume wa Pili nae katuamsha tena haitoshi akatuletea Umoja wa Kitaifa na Mabadiliko ya Katiba ya 10 ya Katiba ya 2010 tena akaifanya iwe shoka la kuvunja Muungano, isomeni vizuri Katiba ya Zanzibar na hapo mtajuwa kuwa ni Muamsho au si Muamsho.
kwa hiyo Stiphen Wasira na UVCCM hamjakosea kusema Muamsho wapo Serikalini, ni kweli, tena wapo serikali ya Chama chenu, wala msimtafute mchawi, wachawi wenyenu.
uvccm-na-steven-wassira.html
No comments:
Post a Comment