Assalaam Alaykum
Naihusia Nafsi yangu pamoja na kuwahusia Ndugu
Zangu Waislamu Katika Kumcha Mwenyezi Mungu.
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mwezi huu wa Shaabani Ni miongoni Mwa
Miezi Mitukufu wala Tusichoke kwa Kufanya Mema pamoja na Kuomba
Msamaha
kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ili kupata Maghafira toka toka Mola
(S.W.T)
Ndugu zangu Waislamu
Tuzidishe Kufunga katika Mwezi huu Mtukufu kiasi
Tutakavyoweza pamoja na Kuzidisha Kheri.
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga sana katika Mwezi huu wa Shaabani.
Ndugu zangu Katika Imaani. Katika mwezi huu wa Shaabani Mtume
(S.A.W)
Alikuwa Akifanya Ibaada Sana.
Siku moja bwana Usama bin Zaid Mola Amwilie Radhi. Alimuliza Mtume (
S.A.W)
Akasema Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu Mbona Sijakuona Unafunga Katika
Miezi Mingine kama Unavyofunga Katika mwezi huu wa Shaabani?
Mtume (S.A.W)
Akajibu Akasema Huu ni Mwezi Ulio baina ya mwezi wa Rajab na
Ramadhani.
Ni watu Wengi Hughafirika Nao. na huu ni Mwezi Ambao Amali za Waja
HUpelekwa
Kwa Mwenyezi Mungu. Basi napenda Zipelekwe Amali Zangu nikiwa
Nimefunga.
Ndugu Zangu Waislsmu Tujitahidi Nasi Tufanye Ibaada Kwa kufuata
mwendo
wa Kipenzi Chetu Mtume Muhammad (S.A.W)
Ndugu zangu Katika Imaani Tuzidishe Ibaada pamoja na Toba kwa Allah
(S.W.T)
Katika Mwezi huu Mtukufu na Hakuna Njia Ya Mkato ya Kwenda Peponi ila
ni
Kwa Kazi ngumu kujitolea katika njia za kheri.
Ndugu Zangu katika Imaani
Tumtii Mwnyezi Mungu na Mtume wake ili Tupate Kurehemewa.
ALHADITH
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga hata tukafikiria kwamba Hatafungua na
Alikuwa Alikuwa Akifungua hata Tukadhani Hatofunga tena.
Sikumuona Mtume Akitimiza Kufunga Ispokuwa Mwezi wa Ramadhani. na
Sikumuona Mtume Pia Kuzidisha Kufunga Saumu ila katika Mwezi wa
Shabaani-kasma Bibi Aisha.
Wabillahi Toufq
No comments:
Post a Comment