Friday, June 8, 2012

HISTORIA YA Bilaal Bin Rabaah (R.A)







HISTORIA YA Bilaal Bin Rabaah (Radhiya Allaahu...

11:32pm Jun 4
HISTORIA YA Bilaal Bin Rabaah (Radhiya Allaahu 'Anhu) (Prt 1)

Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa kila linapotajwa jina la Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu) akisema;

"Bwana wetu aliyemkomboa Bwana wetu". Akimkusudia Bilaal bin Rabaah (Radhiya Allaahu 'anhu). Wanasema wanavyuoni kuwa; Unapomsikia 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) akimwita mtu 'Bwana wetu', basi tambua ya kuwa huyo ni mtu adhimu.

Imeandikwa katika Siyar al-A'alaam an-Nubalaa kuwa Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye asili yake ni Mhabeshi (mu-Ethiopia), alikuwa mweusi sana, mwembamba, mrefu na mwenye nywele ndefu.

Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa mtumwa wa kabila la Bani Jumhi, na maisha yake yalikuwa kama mtumwa yeyote wa kawaida pale Makkah, hakuwa na uwezo wala uhuru wowote isipokuwa kuwatumikia mabwana zake watu wa kabila la Al-Jumhi. Baadaye alimilikiwa na Umayyah bin Khalaf peke yake ambaye pia anatokana na kabila hilo la Al-Jumhiy, na mama yake Bilaal na jina lake lilikuwa Hamaamah, naye pia alikuwa mtumwa wa kabila hilo la Al-Jumhi.

Mara baada ya Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) kuanza kuwalingania watu katika dini ya Kiislam kwa jahari, Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) akawa anasikia habari za dini hii mpya na habari za Mtume huyu mpya (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam), na habari hizo zilikuwa zikimfurahisha sana kila anapozisikia hasa kutoka kwa Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu 'anhu) aliyekuwa kila anapopata fursa akimwendea Bilaal na watu wengine pia na kuwahadithia juu ya dini hii.

Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) akasilimu mikononi mwa Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu 'anhu) aliyekuwa akifanya kazi kubwa sana tokea siku ya mwanzo katika kuwalingania watu katika dini hii tukufu.

Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa akiwalingania watu waliokuwa huru na akafanikiwa kuwasilimisha watu watukufu wakiwemo watano katika wale kumi waliobashiriwa Pepo nao ni 'Uthmaan bin 'Affaan, Az-Zubayr bin 'Awaam, 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf, Sa'ad bin Abi Waqaas na Twalha bin 'UbayduLlaah (Radhiya Allaahu 'anhu) na wengi wengineo, na alikuwa pia akiwalingania watu wasiokuwa huru kama vile Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) aliyekuwa rafiki yake Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu) tokea hata kabla ya Uislam, na wengineo pia.

Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) alifuatana na Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu) mpaka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) na kuzitamka shahada mbili mbele yake, na kwa ajili hiyo akawa miongoni mwa watu wa mwanzo kuingia katika dini hii tukufu.
View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.

No comments: