ADABU NA SABABU ZA KUJIBIWA DUA:
Baadhi ya waislamu wengi hudhani dua waziombazo ni ndogo ndio maana
hawajibiwi na hudhani kuna dua kubwa kubwa ambazo mashekh huzificha
kwa ajili yao tu.
Napenda kukuzindua kuwa Allah (s.w) hujibu dua yeyote ile iwapo
itapitia misingi maalum ambayao kwayo M/Mungu hujibu dua.Misingi hiyo
ni kama ifuatayo:-
1. Mwombaji lazima awe na ikhilaswi (unyenyekevu wakati wa kuomba dua)
2.Mwombaji lazima amwombe M/Mungu peeke bila ya kumshilikisha na chochote
3.Kuhudhurisha moyo katika kuomba dua
4. Mwombaji asiwe na sharaka na haraka ya kujibiwa dua yake (awe na subra)
5.Mwombaji lazima ayatambue madhambi yake na kuomba msamaha kwayo
pamoja na kuzitambua neema na kumshukuru M/Mungu kwazo
6.Kurejesha ulichodhulumu na kutubia na kula chakula ambacho ndani
yake hakuna haramu
7.Kuwa na udhu kabla ya dua kama hilo ni jepesi kwako
8.Kuelekea Qibla wakati wa kuomba kama inawezekana
9.Kuanza kwa kumsifu M/Mungu kwa sifa zake na kumswalia Mtume (s.a.w)
mwanzo na mwisho wa dua.
10.Mwombaji lazima awe ni mwenye kuamrisha mema na kukataza mabaya
11.Maombi yasiwe ya maovu au kukata udugu
Inshallah tukizingatia hayo na mengine mengi mazuri yaliyofundishwa
katika uislamu na imaani dua zetu zitajibiwa.
No comments:
Post a Comment