Monday, June 25, 2012

MANUFAA KATIKA NDOA

MANUFAA KATIKA NDOA

1. Kupata kizazi ambacho kwanza kitasaidia katika ujengaji wa
jamii, pili kueneza jinsia ya watu wa kila kabila au mataifa mbali
mbali, na kubwa zaidi ni kuongeza idadi ya kizazi cha jamii ya
kiislamu.

2. Kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) na Mtume Wake
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kueneza idadi ya
wafuasi wa dini ya Kiislamu.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika
hadithi sahihi:

"Oeni wake wema muwapendao na wataowapatia kizazi chema, kwani siku
ya Qiyaamah nitajivunia ukubwa wa umati wangu." [Ahmad]

3. Kupata baraka za mtoto mwema ambaye atakayemsomea dua mzee
wake (atakapofariki). Maneno haya yamethibitishwa na Hadiyth maarufu
inayosema kuwa:

"Binaadamu anapokufa, basi 'amali zake nzuri hukatika au
humalizika, isipokuwa mambo matatu makuu nayo ni: Sadaka yenye
kuendelea, Elimu yenye kunufaisha na Mtoto mwema atakayemuombea
du'aa mzee/wazee wake." [Riyadhus-Swaalihiyn]

Faida nyenginezo zipatikanazo katika ndoa ni:

4. Kinga kutokana na Shaytwaan katika mambo yanayopelekea au
yanokaribisha tendo la zinaa.

5. Utulivu wa akili na moyo na kuwa na urafiki ambao hupelekea
mapenzi na huruma baina ya mume na mke.

6. Kunganisha kwa Familia za pande mbili za ukeni na uumeni.

7. Kusaidiana katika kazi za nyumba (sio kumuachia mke kazi zote
za ndani ya nyumba). Hii ni tabia ambayo ingalipo kwa baadhi ya akina
baba. Kwa vile tabia hii imekuzwa na utamaduni wetu wa tunakotoka,
kinyume kabisa na maamrisho ya dini yetu ya Kiislamu yanavyotuagiza.

8. Kuelimishana majukumu ya kifamilia. Pia kuweka bidii na kuwa
tayari kuihami na kuitunza familia. Na vile vile kuishughulikia na
kuitimizia mahitaji yake yakiwa ama ya (kimwili, kimavazi, kisiha,
kimawazo na kiroho) na kustahamiliana pale panapotokea kutoelewana.

Wabillahi Towfiq

No comments: