Thursday, June 14, 2012

UMUHIMU WA KUTOA KWA AJILI YA ALLAH

‫Imetoka kwa Abu Hurairjq رضي الله عنه amesema: Mtume صلى الله عليه
وآله وسلم amesema: ((Kila 'amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara
kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba hadi Atakavyo
Allaah…)). [Ahmad].

Na hii ndio maana Anasema Allaah سبحانه وتعالى katika Aayah nyingine
kuwa mtu anapotoa mali yake kwa ajili Yake ni kama mfano amemkopesha
Allaah سبحانه وتعالى mkopo mzuri ambao malipo yake ni kuzidishiwa
zaidi ya hiyo mali aliyoitoa, kisha juu yake ni kupata ujira mwema
kutoka kwa Mola wake Mtukufu. Ni muhimu kujua kuwa Yeye Mwenyewe
Allaah سبحانه وتعالى Ndiye Anayeturuzuku hiyo mali, kisha Anatutaka
tumkopeshe katika hicho alichotupa ili Atulipe zaidi ya Aliyoturuzuku
kabla. Basi nani atakayesita kutoa mkopo kumkopesha Mola wake kwa
kutegemea malipo kama hayo?

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

((مَن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضاً حَسَناً فَيُضَاعِفَهُ لَهُ
وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ))

((Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mwema, ili Amrudishie
maradufu, na apate malipo ya ukarimu)) [Al-Hadiyd: 11]

Kutoa mali kwa fiy Sabili-Allaah ni jambo lenye kutaka kuazimiwa
kikweli kwani hakuna asiyependa kumiliki mali. Na wakati wa kutoa mali
shaytwaan husimama haraka kumtia wasiwasi binaadamu asitoe mali yake.
Unapofika wakati huo basi ndugu Muislamu kumbuka kuwa thawabu zake ni
nyingi mno na nzito mbele ya Allaah na ndio maana tunaona kwamba
Allaah سبحانه وتعالى Ametanguliza mali kabla ya nafsi katika kuhimiza
kufanya jihaad fiy Sabiyli-Allaah:

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَى تِجَارَةٍ
تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ))

((تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ
بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ
تَعْلَمُونَ))

((يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن
تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ
ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))

((Enyi mlioamini! Nikuonyesheni biashara itakayokuokoeni na adhabu
iliyo chungu?))

((Muaminini Allaah na Mtume Wake, na piganeni Jihaad katika Njia ya
Allaah kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi
mnajua))

((Atakusameheni dhambi zenu, na Atakutieni katika Mabustani yapitiwayo
na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele.
Huko ndio kufuzu kukubwa)) [Asw-Swaff: 10-12].

Vile vile:

((إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ
ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي
سَبِيلِ اللَّهِ أُوْلَئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ))

((Hakika Waumini ni wale walio muamini Allaah na Mtume Wake tena
wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihaad katika Njia ya Allaah kwa
mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli)) [Al-Hujuraat: 15].

Kama tunavyoona katika Aayah hizo za juu kwamba Allaah Anatupa nguvu
kutoa mali fiy Sabili-Allaah kwa kutuhakikishia kuwa kutoa ni kufanya
biashara Naye ambayo matokeo yake ni kupata faida nyingi na juu ya
hivyo ni kupata maghfira kutoka Kwake:

((إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ
وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ
تِجَارَةً لَّن تَبُورَ))

((لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ
غَفُورٌ شَكُور))

((Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalah, na
wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika Tulivyowaruzuku, hao hutaraji
biashara isiyododa [isiyoanguka]))
((Ili Yeye Awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na Awazidishie kutokana na
fadhila Zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani))
[Faatwir: 29-30]

No comments: