Friday, June 8, 2012

Fwd: [Ahlusuna Group] Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya...





Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya...

1:07am Jun 7
Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa Uislamu.

Kwa nini Tunazugumzia Mada hii?
JIBU:
Tuna sababu zifuatazo zinazotufanya tuzungumzie mada hii:

Ni katika kulingania dini yetu kwa Jihadi ya hoja na kuzuia Munkari (Maovu).

﴿فَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَجَاهِدْهُمْ بِهِ جِهَادًا كَبِيرًا﴾(الفرقان:٥٢ قال تعالى:

Amesema Allaah:
"Na wala usiwatii Makafiri na pigana nao Jihadi ya hoja ya (Quraan) Jihadi kubwa". (Surat AlFurqaan: 52).

وقال تعالى:﴿ قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴾(يوسف:١٠٨).

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
"Sema hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah kwa ujuzi mimi na yule aliyenifuata na Ametakasika Allaah na kila upungufu nami si katika washirikina"
(Surat Yuusuf: 108).

وقال صلى الله عليه وسلم:(من رأى منكم منكرا فليغيره بيده فإن لم يستطع فبلسانه فإن لم يستطع فبقلبه وذلك أضعف الإيمان)رواه مسلم.

Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa wa sallam):
"Atakaeona miongoni mwenu ovu lolote aliondoe kwa mkono yake, na kama hataweza basi na kwa ulimi wake na kama hataweza basi na aliondoe kwa moyo wake (alichukie) na hali hii (kulichukia kwa moyo) ni udhaifu mkubwa wa imani" (Imepokewa na Imaam Muslim).

Ni wajibu wetu kutoa Nasaha:

قال تعالى:﴿ وَإِنْ أَحَدٌ مِنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّى يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّهِ (التوبة:٦).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
"Kama mmoja yeyote katika washirikina atakuomba awe karibu nawe basi kuwa karibu nae ili apate kusikia maneno ya Allaah"
(Surat At-Tawbah: 6).

Nini Maana Ya Katiba Ya Nchi? Kwa Mtazamo Usio Wa Kidini.

Katika nchi yoyote msingi wa uendeshaji wa nchi unategemea Katiba. Katiba ni sheria kuu au sheria mama katika nchi yoyote. Sheria nyingine zote zinategemea au zinatungwa kwa mujibu wa katiba, wakati mwingine katiba hutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kijamii kati ya watawala na wananchi (watawaliwa).

Maana ya katiba ya nchi kwa mtazamo wa Kiislamu

Sheria kuu na Sheria Mama katika nchi kwa mujibu wa Uislamu ni Qur-aan na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa sallam).

قال تعالى:﴿ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ﴾.(النساء:٥٩).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
"Ikiwa mkikindana (kukhitalifiana) katika jambo lolote basi lilerejesheni (jambo hilo) kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake"
(Surat An-Nisaa: 59).
View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.

No comments: