Ninamshukuru mwenyenzi mungu(s.w) kama anavyostahiki kushukuriwa sala na salama zimfikie mtume wake Muhamad (s.a.w) pamoja na maswahaba wake na wote wanaofata njia zake
Ndugu zangu waislamu, kusalimiana ni jambo ambalo lipo katika kila
jamii tena lilikuwepo kabla ya hata kuja Uislamu. Ulipokuja Uislamu
haukuliondoa bali ulileta matamshi yake maalumu kwa Waislamu
kusalimiana, matamshi ambayo kama yalivyothibiti katika Hadithi ni
yale yale waliyosalimiana baba yetu Aadam ('Alayhis Salaam) na
Malaika wa Ar-Rahmaan kama yalivyothibiti katika Hadithi:
"Allaah Amemuumba Aadam kwa sura yake urefu wake alikuwa dhiraa
sitini, Alipomuumba Alimwambia: Nenda ukawasalimie kikundi kile pale
miongoni mwa Malaika waliokaa na usikilize watachokuitikia nacho;
kwani hayo maamkizi watayokuitikia nayo ndio maamkizi yako na ya
vizazi vyako; Aadam akawaamkia kwa kusema: Assalaamu 'Alaykum;
No comments:
Post a Comment