"Enyi watu! Mcheni Mola wenu, hakika mtetemeko wa...
To: UTAMU WA NDOA <229408227128973@groups.facebook.com>
Hassan Kibari posted in UTAMU WA NDOA
"Enyi watu! Mcheni Mola wenu, hakika mtetemeko wa Kiama ni jambo kubwa
kabisa. Siku mtakapokiaona hicho kiama kila mwanamke anyonyeshaye
atamsahau amnyonyeshaye na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake (kabla
ya wakati) tena kwa uchungu.Utawaona watu wamelewa hali ya kuwa
hawakulewa. Lakini ni adhabu ya Mwenyezi Mungu tu hiyo iliyo kali
kabisa" (22:1-2).
Siku hii nzito kabisa Allah subuhana wataalah ameipa majina mengi
katika Quran mimi nitayataja machache:-
1. YA UMUL-QIAMA- Siku ya kiama
2.ASSAA - Saa
3.AL-WAQIA -Tukio la uhakika
4.AL-HAAQA - Tukio la kushitukiza
5.AL-QARIA - Msiba wenye kugonga nyoyo
6.ASWAAKHA - Sauti kali yenye kuumiza nyoyo za wanadamu
7.ATWAMMATUL-KUBRA- Balaa iliyo kubwa kabisa
8. YA UMUDDIN - Siku ya malipo
9.YA UMUL-HISAAB - Siku ya kuhesabiwa
10. YA UMUL-JAMII - Siku ya kukusanywa
11. YA UMUL-TAGHAABUN - Siku ya khasara
12. YA UMUL-FASIL - siku ya hukumu
13. YA UMUL- ADHIIM - Siku iliyo nzito kabisa
Inshallah Allah (s.w) atunusuru.
No comments:
Post a Comment