Monday, June 25, 2012

MANUFAA KATIKA NDOA

MANUFAA KATIKA NDOA

1. Kupata kizazi ambacho kwanza kitasaidia katika ujengaji wa
jamii, pili kueneza jinsia ya watu wa kila kabila au mataifa mbali
mbali, na kubwa zaidi ni kuongeza idadi ya kizazi cha jamii ya
kiislamu.

2. Kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) na Mtume Wake
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kueneza idadi ya
wafuasi wa dini ya Kiislamu.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika
hadithi sahihi:

"Oeni wake wema muwapendao na wataowapatia kizazi chema, kwani siku
ya Qiyaamah nitajivunia ukubwa wa umati wangu." [Ahmad]

3. Kupata baraka za mtoto mwema ambaye atakayemsomea dua mzee
wake (atakapofariki). Maneno haya yamethibitishwa na Hadiyth maarufu
inayosema kuwa:

"Binaadamu anapokufa, basi 'amali zake nzuri hukatika au
humalizika, isipokuwa mambo matatu makuu nayo ni: Sadaka yenye
kuendelea, Elimu yenye kunufaisha na Mtoto mwema atakayemuombea
du'aa mzee/wazee wake." [Riyadhus-Swaalihiyn]

Faida nyenginezo zipatikanazo katika ndoa ni:

4. Kinga kutokana na Shaytwaan katika mambo yanayopelekea au
yanokaribisha tendo la zinaa.

5. Utulivu wa akili na moyo na kuwa na urafiki ambao hupelekea
mapenzi na huruma baina ya mume na mke.

6. Kunganisha kwa Familia za pande mbili za ukeni na uumeni.

7. Kusaidiana katika kazi za nyumba (sio kumuachia mke kazi zote
za ndani ya nyumba). Hii ni tabia ambayo ingalipo kwa baadhi ya akina
baba. Kwa vile tabia hii imekuzwa na utamaduni wetu wa tunakotoka,
kinyume kabisa na maamrisho ya dini yetu ya Kiislamu yanavyotuagiza.

8. Kuelimishana majukumu ya kifamilia. Pia kuweka bidii na kuwa
tayari kuihami na kuitunza familia. Na vile vile kuishughulikia na
kuitimizia mahitaji yake yakiwa ama ya (kimwili, kimavazi, kisiha,
kimawazo na kiroho) na kustahamiliana pale panapotokea kutoelewana.

Wabillahi Towfiq

Sunday, June 24, 2012

Umuhimu wa kusalimiana

Ninamshukuru mwenyenzi mungu(s.w) kama anavyostahiki kushukuriwa sala na salama zimfikie mtume wake Muhamad (s.a.w) pamoja na maswahaba wake na wote wanaofata njia zake

Ndugu zangu waislamu, kusalimiana ni jambo ambalo lipo katika kila
jamii tena lilikuwepo kabla ya hata kuja Uislamu. Ulipokuja Uislamu
haukuliondoa bali ulileta matamshi yake maalumu kwa Waislamu
kusalimiana, matamshi ambayo kama yalivyothibiti katika Hadithi ni
yale yale waliyosalimiana baba yetu Aadam ('Alayhis Salaam) na
Malaika wa Ar-Rahmaan kama yalivyothibiti katika Hadithi:

"Allaah Amemuumba Aadam kwa sura yake urefu wake alikuwa dhiraa
sitini, Alipomuumba Alimwambia: Nenda ukawasalimie kikundi kile pale
miongoni mwa Malaika waliokaa na usikilize watachokuitikia nacho;
kwani hayo maamkizi watayokuitikia nayo ndio maamkizi yako na ya
vizazi vyako; Aadam akawaamkia kwa kusema: Assalaamu 'Alaykum;

Kwa nini mtume alikuwa akifunga mwezi Rajab na Shaaban kuliko miezi mingine ??soma hapa

Assalaam Alaykum
Naihusia Nafsi yangu pamoja na kuwahusia Ndugu
Zangu Waislamu Katika Kumcha Mwenyezi Mungu.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mwezi huu wa Shaabani Ni miongoni Mwa
Miezi Mitukufu wala Tusichoke kwa Kufanya Mema pamoja na Kuomba
Msamaha
kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ili kupata Maghafira toka toka Mola
(S.W.T)
Ndugu zangu Waislamu
Tuzidishe Kufunga katika Mwezi huu Mtukufu kiasi
Tutakavyoweza pamoja na Kuzidisha Kheri.
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga sana katika Mwezi huu wa Shaabani.

Ndugu zangu Katika Imaani. Katika mwezi huu wa Shaabani Mtume
(S.A.W)
Alikuwa Akifanya Ibaada Sana.
Siku moja bwana Usama bin Zaid Mola Amwilie Radhi. Alimuliza Mtume (
S.A.W)
Akasema Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu Mbona Sijakuona Unafunga Katika
Miezi Mingine kama Unavyofunga Katika mwezi huu wa Shaabani?
Mtume (S.A.W)
Akajibu Akasema Huu ni Mwezi Ulio baina ya mwezi wa Rajab na
Ramadhani.
Ni watu Wengi Hughafirika Nao. na huu ni Mwezi Ambao Amali za Waja
HUpelekwa
Kwa Mwenyezi Mungu. Basi napenda Zipelekwe Amali Zangu nikiwa
Nimefunga.

Ndugu Zangu Waislsmu Tujitahidi Nasi Tufanye Ibaada Kwa kufuata
mwendo
wa Kipenzi Chetu Mtume Muhammad (S.A.W)
Ndugu zangu Katika Imaani Tuzidishe Ibaada pamoja na Toba kwa Allah
(S.W.T)
Katika Mwezi huu Mtukufu na Hakuna Njia Ya Mkato ya Kwenda Peponi ila
ni
Kwa Kazi ngumu kujitolea katika njia za kheri.
Ndugu Zangu katika Imaani
Tumtii Mwnyezi Mungu na Mtume wake ili Tupate Kurehemewa.

ALHADITH
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga hata tukafikiria kwamba Hatafungua na
Alikuwa Alikuwa Akifungua hata Tukadhani Hatofunga tena.
Sikumuona Mtume Akitimiza Kufunga Ispokuwa Mwezi wa Ramadhani. na
Sikumuona Mtume Pia Kuzidisha Kufunga Saumu ila katika Mwezi wa
Shabaani-kasma Bibi Aisha.

Wabillahi Toufq

Tuzidishe kumcha Allah mwezi huu wa Shaabani

Assalaam Alaykum
Naihusia Nafsi yangu pamoja na kuwahusia Ndugu
Zangu Waislamu Katika Kumcha Mwenyezi Mungu.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mwezi huu wa Shaabani Ni miongoni Mwa
Miezi Mitukufu wala Tusichoke kwa Kufanya Mema pamoja na Kuomba Msamaha
kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ili kupata Maghafira toka toka Mola (S.W.T)
Ndugu zangu Waislamu
Tuzidishe Kufunga katika Mwezi huu Mtukufu kiasi
Tutakavyoweza pamoja na Kuzidisha Kheri.
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga sana katika Mwezi huu wa Shaabani.

Ndugu zangu Katika Imaani. Katika mwezi huu wa Shaabani Mtume (S.A.W)
Alikuwa Akifanya Ibaada Sana.
Siku moja bwana Usama bin Zaid Mola Amwilie Radhi. Alimuliza Mtume ( S.A.W)
Akasema Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu Mbona Sijakuona Unafunga Katika Miezi Mingine kama Unavyofunga Katika mwezi huu wa Shaabani?
Mtume (S.A.W)
Akajibu Akasema Huu ni Mwezi Ulio baina ya mwezi wa Rajab na Ramadhani.
Ni watu Wengi Hughafirika Nao. na huu ni Mwezi Ambao Amali za Waja HUpelekwa
Kwa Mwenyezi Mungu. Basi napenda Zipelekwe Amali Zangu nikiwa Nimefunga.

Ndugu Zangu Waislsmu Tujitahidi Nasi Tufanye Ibaada Kwa kufuata mwendo
wa Kipenzi Chetu Mtume Muhammad (S.A.W)
Ndugu zangu Katika Imaani Tuzidishe Ibaada pamoja na Toba kwa Allah (S.W.T)
Katika Mwezi huu Mtukufu na Hakuna Njia Ya Mkato ya Kwenda Peponi ila ni
Kwa Kazi ngumu kujitolea katika njia za kheri.
Ndugu Zangu katika Imaani
Tumtii Mwnyezi Mungu na Mtume wake ili Tupate Kurehemewa.

ALHADITH
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga hata tukafikiria kwamba Hatafungua na Alikuwa Alikuwa Akifungua hata Tukadhani Hatofunga tena.
Sikumuona Mtume Akitimiza Kufunga Ispokuwa Mwezi wa Ramadhani. na
Sikumuona Mtume Pia Kuzidisha Kufunga Saumu ila katika Mwezi wa Shabaani-kasma Bibi Aisha.

Wabillahi Toufiq

Tuzidishe kumcha Allah mwezi huu wa Shaabani

Assalaam Alaykum
Naihusia Nafsi yangu pamoja na kuwahusia Ndugu
Zangu Waislamu Katika Kumcha Mwenyezi Mungu.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mwezi huu wa Shaabani Ni miongoni Mwa
Miezi Mitukufu wala Tusichoke kwa Kufanya Mema pamoja na Kuomba Msamaha
kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ili kupata Maghafira toka toka Mola (S.W.T)
Ndugu zangu Waislamu
Tuzidishe Kufunga katika Mwezi huu Mtukufu kiasi
Tutakavyoweza pamoja na Kuzidisha Kheri.
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga sana katika Mwezi huu wa Shaabani.

Ndugu zangu Katika Imaani. Katika mwezi huu wa Shaabani Mtume (S.A.W)
Alikuwa Akifanya Ibaada Sana.
Siku moja bwana Usama bin Zaid Mola Amwilie Radhi. Alimuliza Mtume ( S.A.W)
Akasema Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu Mbona Sijakuona Unafunga Katika Miezi Mingine kama Unavyofunga Katika mwezi huu wa Shaabani?
Mtume (S.A.W)
Akajibu Akasema Huu ni Mwezi Ulio baina ya mwezi wa Rajab na Ramadhani.
Ni watu Wengi Hughafirika Nao. na huu ni Mwezi Ambao Amali za Waja HUpelekwa
Kwa Mwenyezi Mungu. Basi napenda Zipelekwe Amali Zangu nikiwa Nimefunga.

Ndugu Zangu Waislsmu Tujitahidi Nasi Tufanye Ibaada Kwa kufuata mwendo
wa Kipenzi Chetu Mtume Muhammad (S.A.W)
Ndugu zangu Katika Imaani Tuzidishe Ibaada pamoja na Toba kwa Allah (S.W.T)
Katika Mwezi huu Mtukufu na Hakuna Njia Ya Mkato ya Kwenda Peponi ila ni
Kwa Kazi ngumu kujitolea katika njia za kheri.
Ndugu Zangu katika Imaani
Tumtii Mwnyezi Mungu na Mtume wake ili Tupate Kurehemewa.

ALHADITH
Mtume (S.A.W) Alikuwa Akifunga hata tukafikiria kwamba Hatafungua na Alikuwa Alikuwa Akifungua hata Tukadhani Hatofunga tena.
Sikumuona Mtume Akitimiza Kufunga Ispokuwa Mwezi wa Ramadhani. na
Sikumuona Mtume Pia Kuzidisha Kufunga Saumu ila katika Mwezi wa Shabaani-kasma Bibi Aisha.

Wabillahi Toufiq

Thursday, June 14, 2012

KUMTEGEMEA MWENYEEZI MUNGU SUBHAANAHU WA TA'ALA:

KUMTEGEMEA MWENYEEZI MUNGU SUBHAANAHU WA TA'ALA:
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
A/Alleykum,
Kumpenda Mwenyeezi mungu na Mtume wake ni miongoni mwa mambo ya IMANI
ya Lazima, Mtu hawi Muislaam mwenye Imani mpaka atangulize mapenzi ya
Mwenyeezi mungu na mtume wake mbele ya kitu alichonacho, kiwe ni
mali,mtoto,mzazi, au watu woote, kama alivyotueleza Mtume wetu...''Na
kadri ya mapenzi ndio unapatikana UTIIFU na kufuata amri za Allah s.w.
na Mtume wake''.
Na hakika himaya ya kutafuta cha kutosheleza au kutaka utajiri vyote
vipo katika milki ya Mwenyeezi mungu, na kama alivyosema Mtume swalla
allaahu 'alayhi wa sallam ''Isiwapelekee nyinyi uzito wa kupata riziki
mkaingia katika kumuasi Mwenyeezi mungu, hazitapatikana zilizoko kwa
mwenyeezi mungu ila kwa Twaa yake'' , na hadith nyingine imepokewa
toka kwa omar bin khatwab r.a. akisema nimemsikia Mtume swalla allaahu
'alayhi wa sallam akisema ''Lau hakika nyinyi mungalikuwa mnamtegemea
Mwenyeezi mungu haki ya kumtegemea angeliwaruzuku nyinyi kama
anavyowaruzuku ndege, wanatoka asubuhi wakiwa na njaa na wanarudi
jioni wakiwa wameshiba''. Kutokana na hadithi hii inatuonyesha
TUMTEGEMEE ALLAH SUBHAANAHU WA TA'ALA Kikweli na Allah atatupa
tunalolitaka, Na aya nyingi zimekuja za kumtegemea Allah, mfano katika
suratil Huud:123...''Ni vya Mwenyeezi mungu vilivyofichika mbinguni na
ardhini na mambo yote yanarejeshwa kwake na hakuna Mola mwenye
kughafilika na mnayoyatenda''.
Pia katika suratil shuaraa:217..."Na umtegemee Mola wako mwenye nguvu
mwenye Rehema''.
Na suratil Ahzaab:3..''Na umtegemee Mwenyeezi mungu na Mwenyeezi Mungu
atosha kuwa Mlinzi''.
Na Mtume swalla allaahu 'alayhi wa sallam ameeleza kuhusu kumtegemea
Allah s.w. katika hadith aliyoipokea Abu hurarya r.a...''wataingia
peponi watu nyoyo zao ni mfano wa nyoyo za ndege''(muslim), maana yake
wanaomtegemea Mwenyeezi Mungu kwa kuwa nyoyo zao ni laini.
Hakika Allah subhaanahu wa ta'ala amewaahidi wenye kumtegemea watapata
malipo makubwa, Na hakuna kufaulu wala kupata furaha ila kwa kumuabudu
ALLAH subhaanahu wa ta'ala na kumuomba Msaada kwake yeye ndiyo mwenye
kuabudiwa kiukweli, na yeye anastahiki kuombwa msaada pekee yake.
...Inshaalah Allah s.w. atujaalie tuwe wenye KUMTEGEMEA yeye peke
yake, na tusimshirikishe na chochote.
Atujaalie ni Wenye kusikia pamoja na kufuata na atuepushe na Batili,
Na atupe Mema ya ulimwenguni na Akhera...AMIIN:

"MAMBO 10 YA KUZINGATIA KWA MMEO"

"MAMBO 10 YA KUZINGATIA KWA MMEO"

1. Unyenyekee kwake kwa Kukinai.
2. Umsikilize Mmeo na Kumtii.
3. Na uangalie Maeneo ya Macho yake na Pua yake. Yaan macho yake
yasione au Kuangalia yanayochukiza kwako mfano kaenda kizini karudi
kakukuta hujakoga nguo chafu unanuka Moshi na Mikojo ya Watoto. 4.
Hivyo basi Macho ya Mumeo yasione Au Kuangalia Yanayochukiza kwako na
wala mapua yake Yasinuse ila Harufu Nzuri kutoka Kwako.
5. Angalia sana wakati wake wa kulala Mumeo na Umpe chakula chake.
6. Kwani hakika Mbabaiko wa njaa Unaunguza na Kunaghadhibisha.
7. Chunga Mali yake na Ulinde heshima yake na Watoto wake.
8. Na matumizi ya Mali yawe Mazuri na katika kuishi Nae Upange vizuri
Maisha.
9. Usimuasi kwa Jambo lolote na Usitoe Siri Zake Mumeo nje.
10. Kwani wewe Ukikengeuka na Amri yake Utapandisha Shuki na Hasira
katika kifua chake. Na ukitoa siri Zake hutosalimika kwa kumvunjia
ahadi yake. Kisha ole wako na kufurahi hali yakuwa Mmeo hana Raha. Na
kukasirika hali ya kuwa mmeo Amefurahi!
Pia kuwa Kwake mfanyakazi nae Atakuwa ni Mtumwa wako asiyetamani
kukukosa.
Assalaam Alaykum

Photo attachment:
http://www.facebook.com/photo.php?fbid=221488311305869&set=o.229408227128973&type=1

ADABU NA SABABU ZA KUJIBIWA DUA:

ADABU NA SABABU ZA KUJIBIWA DUA:

Baadhi ya waislamu wengi hudhani dua waziombazo ni ndogo ndio maana
hawajibiwi na hudhani kuna dua kubwa kubwa ambazo mashekh huzificha
kwa ajili yao tu.
Napenda kukuzindua kuwa Allah (s.w) hujibu dua yeyote ile iwapo
itapitia misingi maalum ambayao kwayo M/Mungu hujibu dua.Misingi hiyo
ni kama ifuatayo:-
1. Mwombaji lazima awe na ikhilaswi (unyenyekevu wakati wa kuomba dua)
2.Mwombaji lazima amwombe M/Mungu peeke bila ya kumshilikisha na chochote
3.Kuhudhurisha moyo katika kuomba dua
4. Mwombaji asiwe na sharaka na haraka ya kujibiwa dua yake (awe na subra)
5.Mwombaji lazima ayatambue madhambi yake na kuomba msamaha kwayo
pamoja na kuzitambua neema na kumshukuru M/Mungu kwazo
6.Kurejesha ulichodhulumu na kutubia na kula chakula ambacho ndani
yake hakuna haramu
7.Kuwa na udhu kabla ya dua kama hilo ni jepesi kwako
8.Kuelekea Qibla wakati wa kuomba kama inawezekana
9.Kuanza kwa kumsifu M/Mungu kwa sifa zake na kumswalia Mtume (s.a.w)
mwanzo na mwisho wa dua.
10.Mwombaji lazima awe ni mwenye kuamrisha mema na kukataza mabaya
11.Maombi yasiwe ya maovu au kukata udugu
Inshallah tukizingatia hayo na mengine mengi mazuri yaliyofundishwa
katika uislamu na imaani dua zetu zitajibiwa.

Mwenyezi Mungu anasema tujitolee nafsi zetu kwa ajili yake

Mwenyezi Mungu anasema
Na ktk ishara zake Mwenyezi Mungu (kuonyesha hisani yake) amekuumbieni
kutokana na nafsi zenu wanawake ili mpate UTULIVU kwao. Na akaweka
baina yenu mapenzi na huruma kwa hakika katika haya kuna alama kwa
watu wanaotafakari. Wewe vipi umempata mke halafu unautafuta utulivu
kwenye bao? Au unaupata utulivu kwenye kusoma magazeti yalio jaa:-
1. Habari ýa vita
2. Habari za maafa
Umepotea ndugu khazina ya utulivu anayo mkeo
Funguka

Na watu wanafanya mambo kwa kujiona wao ni wabora sana hebu soma hapa kwa maelezo zaidi

اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ
سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن
ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ
أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ
إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ
يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

"Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Aliye hai, Msimamiaji wa
mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee
vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele
yake bila ya idhini Yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma
yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi Wake, ila kwa
atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala
haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye Aliye juu, na ndiye Mkuu."

Al-Baqarah – 255

JE MNAJUA MAANA YA KUMSENGENYA MTU?? soma hapa kwa maelezo zaidi

عَنْ أَبِى هُرَيْرَةَ رَضِىَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُوْلَ اللهِ صَلَّى
اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم قَالَ:أَتَدْرُوْنَ مَاالْغِيبَةُ؟قَالُوا:اللهُ
وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ:قَالَ ذِكْرُكَ أَخَاكَ
بِمَايَكْرَهُ.قَالَ:أَفَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِى أَخِى
مَاأَقُوْلُ.قَالَ:إِنْ كَانَ فِيْهِ مَاتَقُوْلُ فَقَدِ
اُغْتَبْتَهُ,وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيْهِ فَقَدْ بَهَتَّهُ)أَخْرَجَهُ
مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abii huraira Radhwi za M/mungu ziwe juu yake,Amesema Mtume
wa M/mungu rehma na amani ziwe juu yake.
Hivi mnamjua msengenyaji?,wakajibu maswahaba "M/mungu na mtume wake
ndio wenye kujua"
Akasema Mtume,kusengenya ni kumtaja ndugu yako wakati hayupo kwa yale
yanayo mkera.maswahaba wakauliza, "Jee ikiwa yale tunayomzungumzia ni
ya kweli?" akasema tena mtume "hata ikiwa mnayomzungumzia ni ya
kweli mtakuwa mmemsengenya,na hata kama mnayomzungumzia hana basi
utakuwa umemsengemya.
Imepokelewa na imamu muslim

UMUHIMU WA KUTOA KWA AJILI YA ALLAH

‫Imetoka kwa Abu Hurairjq رضي الله عنه amesema: Mtume صلى الله عليه
وآله وسلم amesema: ((Kila 'amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara
kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba hadi Atakavyo
Allaah…)). [Ahmad].

Na hii ndio maana Anasema Allaah سبحانه وتعالى katika Aayah nyingine
kuwa mtu anapotoa mali yake kwa ajili Yake ni kama mfano amemkopesha
Allaah سبحانه وتعالى mkopo mzuri ambao malipo yake ni kuzidishiwa
zaidi ya hiyo mali aliyoitoa, kisha juu yake ni kupata ujira mwema
kutoka kwa Mola wake Mtukufu. Ni muhimu kujua kuwa Yeye Mwenyewe
Allaah سبحانه وتعالى Ndiye Anayeturuzuku hiyo mali, kisha Anatutaka
tumkopeshe katika hicho alichotupa ili Atulipe zaidi ya Aliyoturuzuku
kabla. Basi nani atakayesita kutoa mkopo kumkopesha Mola wake kwa
kutegemea malipo kama hayo?

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

((مَن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضاً حَسَناً فَيُضَاعِفَهُ لَهُ
وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ))

((Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mwema, ili Amrudishie
maradufu, na apate malipo ya ukarimu)) [Al-Hadiyd: 11]

Kutoa mali kwa fiy Sabili-Allaah ni jambo lenye kutaka kuazimiwa
kikweli kwani hakuna asiyependa kumiliki mali. Na wakati wa kutoa mali
shaytwaan husimama haraka kumtia wasiwasi binaadamu asitoe mali yake.
Unapofika wakati huo basi ndugu Muislamu kumbuka kuwa thawabu zake ni
nyingi mno na nzito mbele ya Allaah na ndio maana tunaona kwamba
Allaah سبحانه وتعالى Ametanguliza mali kabla ya nafsi katika kuhimiza
kufanya jihaad fiy Sabiyli-Allaah:

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَى تِجَارَةٍ
تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ))

((تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ
بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ
تَعْلَمُونَ))

((يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن
تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ
ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))

((Enyi mlioamini! Nikuonyesheni biashara itakayokuokoeni na adhabu
iliyo chungu?))

((Muaminini Allaah na Mtume Wake, na piganeni Jihaad katika Njia ya
Allaah kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi
mnajua))

((Atakusameheni dhambi zenu, na Atakutieni katika Mabustani yapitiwayo
na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele.
Huko ndio kufuzu kukubwa)) [Asw-Swaff: 10-12].

Vile vile:

((إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ
ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي
سَبِيلِ اللَّهِ أُوْلَئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ))

((Hakika Waumini ni wale walio muamini Allaah na Mtume Wake tena
wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihaad katika Njia ya Allaah kwa
mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli)) [Al-Hujuraat: 15].

Kama tunavyoona katika Aayah hizo za juu kwamba Allaah Anatupa nguvu
kutoa mali fiy Sabili-Allaah kwa kutuhakikishia kuwa kutoa ni kufanya
biashara Naye ambayo matokeo yake ni kupata faida nyingi na juu ya
hivyo ni kupata maghfira kutoka Kwake:

((إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ
وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ
تِجَارَةً لَّن تَبُورَ))

((لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ
غَفُورٌ شَكُور))

((Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalah, na
wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika Tulivyowaruzuku, hao hutaraji
biashara isiyododa [isiyoanguka]))
((Ili Yeye Awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na Awazidishie kutokana na
fadhila Zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani))
[Faatwir: 29-30]

"Enyi watu! Mcheni Mola wenu, hakika mtetemeko wa...

"Enyi watu! Mcheni Mola wenu, hakika mtetemeko wa...
To: UTAMU WA NDOA <229408227128973@groups.facebook.com>

Hassan Kibari posted in UTAMU WA NDOA

"Enyi watu! Mcheni Mola wenu, hakika mtetemeko wa Kiama ni jambo kubwa
kabisa. Siku mtakapokiaona hicho kiama kila mwanamke anyonyeshaye
atamsahau amnyonyeshaye na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake (kabla
ya wakati) tena kwa uchungu.Utawaona watu wamelewa hali ya kuwa
hawakulewa. Lakini ni adhabu ya Mwenyezi Mungu tu hiyo iliyo kali
kabisa" (22:1-2).
Siku hii nzito kabisa Allah subuhana wataalah ameipa majina mengi
katika Quran mimi nitayataja machache:-
1. YA UMUL-QIAMA- Siku ya kiama
2.ASSAA - Saa
3.AL-WAQIA -Tukio la uhakika
4.AL-HAAQA - Tukio la kushitukiza
5.AL-QARIA - Msiba wenye kugonga nyoyo
6.ASWAAKHA - Sauti kali yenye kuumiza nyoyo za wanadamu
7.ATWAMMATUL-KUBRA- Balaa iliyo kubwa kabisa
8. YA UMUDDIN - Siku ya malipo
9.YA UMUL-HISAAB - Siku ya kuhesabiwa
10. YA UMUL-JAMII - Siku ya kukusanywa
11. YA UMUL-TAGHAABUN - Siku ya khasara
12. YA UMUL-FASIL - siku ya hukumu
13. YA UMUL- ADHIIM - Siku iliyo nzito kabisa

Inshallah Allah (s.w) atunusuru.

Hassan Al-Basriy aliulizwa ameupata vp ucha Mungu...

Hassan Al-Basriy aliulizwa ameupata vp ucha Mungu...
To: UTAMU WA NDOA <229408227128973@groups.facebook.com>

Halima Al-Amin posted in UTAMU WA NDOA

Hassan Al-Basriy aliulizwa ameupata vp ucha Mungu na utulivu wa nafsi
yake? Akajibu kwa kusema:
1. NAJUA kila nifanyalo ALLAH ANANIONA. Hili hunifanya niogope kufanya maasia.
2. Sipapariki moyo kwani NAJUA RIZKI yangu hakuna atakaeichukua ALLAH
keshaniandikia.
3. NAJUA hakuna atakaenifanyia IBADA zangu lazima nifanye mwenyewe.
4. NAJUA ntakutana na KIFO wakati wowote hivyo lazima NIANDAE zawadi
zitumikazo akhera.
Jee sisi tunayazingatia haya??Funguka

SWALI: Je, Shirki ipo kwa Waislamu?

SWALI: Je, Shirki ipo kwa Waislamu?

JIBU: Ndio, ni masikitiko kuwa ipo tena nyingi'

DALILI KUTOKA QUR-AAN:(وما يؤمن أكثرهم بالله إلا وهم مشركون)

Na wengi katika wao hawamuamini Allaah pasina kuwa ni washirikina. (Yuwsuf: 106

DALILI KUTOKA HADIYTH :(لاتقوم الساعة حتى تلحق قبائل من أمتي بالمشركين
وحتى تعبد الأوثان )

Qiyaamah hakitosimama mpaka kutafika wakati watu wa baadhi ya makabila
katika ummah wangu wataungana na washirikina na hadi watakapoabudu
asiye Allaah!

ASSALAAM ALAYKUM SOMA KISA HIKI

ASSALAAM ALAYKUM

KISA:

Swahaba aliyeitwa Julaybiyb alijulikana sana kuwa alikuwa ni mtu duni
asiyemiliki mali na hakuwa ni mzuri kwa sura na umbo, na alikuwa ni
mtu wa kuchekesha watu. Kwa hivyo hakuna aliyetaka kumuozesha binti
yake. Mtume (S.A.W) alimuuliza Julaybib kama anataka kuoa, naye
akamjibu: "Ewe Mjumbe wa Allah, nani atakayekubali nimuoe mimi?

Sina nyumba wala mali wala chochote katika mapambo ya dunia".
Mtume (S.A.W) akamtuma mtu mmoja aende nyumba ya Answaariy fulani
ambao walikuwa ni familia yenye kujulikana kwa kabila lao maarufu
kubwa lenye kujulikana kwa heshima na wenye hali nzuri. Alipopiga
hodi, alifungua mlango mama wa binti huyo. Swahaba akamjulisha kuwa
ametumwa na Mtume kuleta posa kwa binti yake.

Mama huyo alifurahi sana kudhania kwamba Mtume (S.A.W) ndiye anayetaka
kumposa binti yake. Swahaba Alipomjulisha kuwa sio kwa ajili ya Mtume
(S.A.W) bali ni kwa ajili ya Julaybiyb, mama huyo alisema: "Nani?
Julaybib? Hapana! Hatumuozeshi yeye binti yetu!".

Mara yule binti alisikia mazungumzo hayo akaja kuuliza vizuri: "Nani
anayetaka kuniposa?" Mama mtu akamuelezea kuwa Mtume (S.A.W) amemtuma
mtu aje kumposa yeye kwa ajili ya Julaybiyb.

Binti huyo alimwambia mama yake: "Vipi mama unakataa amri ya Mtume
(S.A.W) Fuata amri yake kwani hakuna kitakachonidhuru". (Katika usemi
mmoja ni kwamba hapo hapo Aayah ifuatayo iliteremshwa [Ibnu Kathiyr
7:692-694]) na katika usemi mwingine aliwaambia wazazi wake:
"Hamkusikia kauli ya Allah (S.W)

(وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ
وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ
وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا)

(Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari
katika jambo, Allah na Mtume Wake Wanapokata shauri katika jambo lao.
Na mwenye kumuasi Allah na Mtume Wake basi hakika amepotea upotofu
ulio wazi)[Al-Ahzaab:36]

Ikabidi wamuozeshe binti yao kwa Julaybiyb. Kisha katika vita fulani
alitoka Mtume (S.AW) na Maswahaba miongoni mwao ni Julaybiyb na baada
ya ushindi wa vita hivyo, Mtume (S.A.W) aliwauliza Maswahaba kabla ya
kurudi: (Je, kuna mtu aliyekosekana?)
Wakataja baadhi ya Maswahaba waliokosekana kisha Mtume (S.A.W)
akawauliza tena wakasema: "Hakuna mtu mwingine aliyekosekana: Lakini
Mtume (S.A.W) akasema: (Lakini mimi naona kwamba Julaybiyb
amekosekana) yaani hayupo na sisi.

(Nendeni mkamtafute miongoni mwa waliouliwa). Wakaenda Maswahaba
kumtafuta wakamkuta ameuawa akiwa karibu yake makafiri saba ambao
aliwahi kuwaua yeye Julaybiyb. Maswahaba wakamjulisha Mtume (S.A.W)
ambaye alikwenda na kusimama karibu naye kisha akasema: (Ameua saba
kisha wakamuua. Yeye ni wangu na mimi ni wake).

Alisema hivyo mara mbili au tatu, kisha Mtume (S.A.W) akambeba kwa
mikono yake na kwenda kumzika. Na akamuombea Du'aa mke wake:

(الَّلهُمَّ، صَبَّ عَلَيْهَا [الخير] صَبَّا، وَلاَ تَجْعَل عَيْشَها كَدَّا)

(Ewe Allah, Mjaze kheri (nyingi) zilizojaa na Usimjaaliye maisha yake
kuwa ni ya shida [tabu na mashaka]

Imesemekana kwamba hakuweko mjane aliyekuwa ana maisha mema kama
maisha ya mke wa Julaybiy (R.A)

[Kisa kimesimuliwa na Imaam Ahmad Muslim na An-Nasaaiy]

Ndugu waislamu Kisa Hiki kimetufunza nini? wewe Binafsi. Funguka:

Wednesday, June 13, 2012

SWALI: Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah?



3:29pm Jun 10
SWALI: Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah?
JIBU: Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى.
(ذلك بأن الله هو الحق وأن مايدعون من دونه الباطل )

Hivi ni kwa sababu hakika Allaah ndiye wa kweli, na hakika wanachokiomba ni cha uongo. (Luqmaan: 30)

(من قال لا إله إلا الله وكفر بما يعبد من دون الله حرم ماله ودمه )

Atakayesema 'Laa ilaaha illa Allaah na akawapinga wanaoabudiwa wasio Allaah italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai(.

SWALI: Nini maana ya Tawhiyd katika sifa za Allaah SWA.?
JIBU: Kuthibitisha alivyojisifu Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى au alivyosifiwa na Mtume wake.

) ليس كمثله شيء وهو السميع البصير)

Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. (Ash-Shuwraa: 11)

(ينزل ربنا تبارك وتعالى في كل ليلة إلى السماء الدنيا)

Mola wetu Huteremka kila usiku katika mbingu ya dunia.

SWALI: Nini faida ya Tawhiyd kwa Muislamu?
JIBU: Kupata Hidaaya duniani na kuwa katika amani Akhera.

(الذين أمنوا ولم يلبسوا إيمانهم بظلم أولئك لهم الأمن وهم مهتدون )

Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakaopata amani na wao ndio walioongoka. (Al-An'aam: 82)

( حق العباد على الله أن لايعذب من لا يشرك به شيئ )

Haki ya mja kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى (Anayomfanyia) kuwa Hamuadhibu yule asiyemshirikisha Yeye na chochote.

View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.

Hakika Katika Jambo ambalo ni Muhimu kwa Mme...





Hakika Katika Jambo ambalo ni Muhimu kwa Mme kulichunga na kulilinda ni Kumchezea Chezea mke Wake na Haswa kabla ya Kumingilia,
Hili Linaathari kubwa sana Kati ya WanandoaWawili katika Mahusiano yao ya Kiroho
na Ya Kijinsi.
Katika Kufikia Kilele cha Raha ya Kiwiliwili kunahitaji kwa Mwanamme awe na
Diplomasia ili aweze Kumpa Mke wake Hamu na Matamanio ya Kweli,
na Ushiriki Mzuri ulio kamili na Mapenzi Yaliyokita.

Mke Akiwa Mwenye Hekima ANaweza Kwa Diplomasia aliyokuwa nayo ya
Mapambo yake na Usafi wa Kiwiliwili chake Kumvuta Mume wake na Kumtamanisha.
Hivyo basi kumhimiza katika kuwasiliana kwa Viwili wili vyao kwa Urahisi na Wepesi
Zaidi, Mahaba Siku Zote yanatimiza Furaha,


Pia tendo la kubusu lina Athari Muhimu sana katika Mapenzi ya Mdoa na Hukurubisha zile Hisia za Mapenzi na Mwisho na Mwisho Hupelekea Kugandana kwa Kiwiliwili,
Busu Nalo lina Umuhimu wake Busu nalo Linatakiwa Liwe katika Hali Nzuri lenye Kusisimua. na Hasa Linapokuwa ni
Mdomo kwa Mdomo Hali yakuwa Wanandoa Wanapokuwa Wamefumba Macho
Mawili na Kufungua kidogo kidogo Mara kwa mara.

Wakati huo wakati Huo Inapokuwa
Miili yao Imegandana na Pumzi Kubadilishana hali Zikiwa Moto moto, Ukianzia Kuvuta
Kwa ndani kabisa na Macho yenu yakiwa yanaangaliana kwa Huruma. Yote Haya
Huzipa Raha Nafsi za Wanandoa na ni Vitangulizi vizuri kwa Kutayarisha Mazingira
Mazuri ya Kuanza kwa Jimai.

Busu lilivyo na Umuhimu Hata Mtume S.A.W Alikuwa Akiwabusu Wake zake Na
Alikuwa haachi Kuwabusu Wake Zake Hata kama Amefunga Saumu.
Kwan Alikuwa Akiwabusu na Akiwakumbatia Wake zake Hali Yakuwa Amefunga"
(Bukhari na Muslim) Ummu Salama r.a Amesema Hakika Mtume wa Allah Alikuwa
Akiwabusu Wake zake Hali ya kuwa Amefunga


.


Hakika Katika Jambo ambalo ni Muhimu kwa Mme...

.


2:07am Jun 11
Hakika Katika Jambo ambalo ni Muhimu kwa Mme kulichunga na kulilinda ni Kumchezea Chezea mke Wake na Haswa kabla ya Kumingilia,
Hili Linaathari kubwa sana Kati ya WanandoaWawili katika Mahusiano yao ya Kiroho
na Ya Kijinsi.
Katika Kufikia Kilele cha Raha ya Kiwiliwili kunahitaji kwa Mwanamme awe na
Diplomasia ili aweze Kumpa Mke wake Hamu na Matamanio ya Kweli,
na Ushiriki Mzuri ulio kamili na Mapenzi Yaliyokita.

Mke Akiwa Mwenye Hekima ANaweza Kwa Diplomasia aliyokuwa nayo ya
Mapambo yake na Usafi wa Kiwiliwili chake Kumvuta Mume wake na Kumtamanisha.
Hivyo basi kumhimiza katika kuwasiliana kwa Viwili wili vyao kwa Urahisi na Wepesi
Zaidi, Mahaba Siku Zote yanatimiza Furaha,


Pia tendo la kubusu lina Athari Muhimu sana katika Mapenzi ya Mdoa na Hukurubisha zile Hisia za Mapenzi na Mwisho na Mwisho Hupelekea Kugandana kwa Kiwiliwili,
Busu Nalo lina Umuhimu wake Busu nalo Linatakiwa Liwe katika Hali Nzuri lenye Kusisimua. na Hasa Linapokuwa ni
Mdomo kwa Mdomo Hali yakuwa Wanandoa Wanapokuwa Wamefumba Macho
Mawili na Kufungua kidogo kidogo Mara kwa mara.

Wakati huo wakati Huo Inapokuwa
Miili yao Imegandana na Pumzi Kubadilishana hali Zikiwa Moto moto, Ukianzia Kuvuta
Kwa ndani kabisa na Macho yenu yakiwa yanaangaliana kwa Huruma. Yote Haya
Huzipa Raha Nafsi za Wanandoa na ni Vitangulizi vizuri kwa Kutayarisha Mazingira
Mazuri ya Kuanza kwa Jimai.

Busu lilivyo na Umuhimu Hata Mtume S.A.W Alikuwa Akiwabusu Wake zake Na
Alikuwa haachi Kuwabusu Wake Zake Hata kama Amefunga Saumu.
Kwan Alikuwa Akiwabusu na Akiwakumbatia Wake zake Hali Yakuwa Amefunga"
(Bukhari na Muslim) Ummu Salama r.a Amesema Hakika Mtume wa Allah Alikuwa
Akiwabusu Wake zake Hali ya kuwa Amefunga


.

Swalah Ya Safari:




11:38am Jun 12
Swalah Ya Safari:
Kwa vile Uislamu ndio njia pekee kamili na sahihi ya maisha, basi unawafikiria Waumini na hali zao katika mazingira tofauti. Na kwa vile safari zina mashaka, misukosuko na taabu, Uislamu unamsahilishia mambo msafiri upande wa Swalah na hata Funga. Hivyo ukiwa safarini swali Rakaa mbili badala ya Rakaa nne katika Swalah ya Adhuhuri, Alasiri na Ishaa. Ama Alfajiri na Magharibi hazipunguzwi. Allah Ametuambia:

Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Swalah"

(4: 101).

Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hii (kupunguza Swalah) ni neema ya Allaah kwenu, basi ipokeeni kwa shukrani" (Al-Bukhari).

Mtu akishatoka sehemu anayoishi kwa nia ya kuwa safarini (safari ianyokusudiwa hapa ni safari ya kheri inayoruhusiwa na Uislamu si safari ya maasiya na ufisadi) inakubidi ufupishe Swalah.

((Amehadithia 'Abdillahi bin 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) kuwa alisafiri na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu), 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) na 'Uthmaan (Radhiya Allaahu 'anhu) na kamwe hakuwaona kabisa kuswali zaidi ya Rakaa mbili zile Swalah za Rakaa nne ndani ya safari)) (Al-Bukhariy na Muslim).

Hamna umbali maalumu uliowekwa na Qur-aan au Sunnah. Kuna kauli nyingi na rai tofauti kutoka kwa Maulamaa kuhusu masafa, wengine wamesema ni maili 48 au kilomita 85 kutokana kwamba Ibn 'Umar na Ibn 'Abbaas walikuwa wakifupisha katika masafa hayo, na wengine wameonelea mwendo wa siku tatu kutokana na Hadiyth ya kuwa 'asisafiri mwanamke masafa ya siku tatu bila kuwa na Mahram wake', na wengine kutokana na kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali Rakaa mbili baada tu ya maili tatu. Ama kauli yenye nguvu ni kuwa pale popote panapojulikana katika ada ya jamii ni safari basi hupunguzwa Swalah, japo ni chini ya masafa yaliyotajwa. Na hapa haiangaliwi jinsi ya kusafiri iwe kwa mguu, mnyama, gari, treni, meli au ndege, kinachoangaliwa ni tendo la safari.


"SABABU KUBWA ZA KUWA WANAWAKE WACHACHE PEPONI"







10:00am Jun 11
"SABABU KUBWA ZA KUWA WANAWAKE WACHACHE PEPONI"

Kama inavyojulikana Mtume S.A.W. alipokuwa katika safari yake ya usiku wa Israa alibahatika kuoneshwa Moto wa Jahannam akaona watu walio wengi zaidi ni wanawake. Na wakati alipowaona idadi yao ni kubwa alishangaa na kuuliza sababu yake na akajibiwa kama tutakavyoona katika Hadithi iliyopo hapo chini. Hadithi iliyopokelewa na Abu Said Al-Khudry R.A.A. na iliyotolewa na Muslim, Mtume S.A.W. kasema, "

"Enyi jamii ya wanawake! Toeni sadaka, kwani mimi nimekuoneni nyinyi zaidi watu wa Motoni. Tukasema "Na kwa nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Akajibu akasema "Mnazidisha (kuitamka) laana na mnakanusha fadhila na ihsaani za waume zenu."Pia katika Hadithi nyingine Mtume S.A.W. alipoona Motoni idadi kubwa ya wanawake aliuliza sababu zilizowafanya wawe humo akajibiwa,

"Niliona wengi wa watu wake wanawake nikasema "Wana nini?" Ikasemwa, "Vimewashughulisha vyekundu viwili: Dhahabu na zaafarani (yaani nguo za rangi mbalimbali)." Kama inavyoonesha katika hizo Hadithi mbili zilizopo hapo juu, sababu kubwa ya wanawake wengi kuwa Motoni ni kule kughilibika kwao na dunia kwa kujishughulisha na kupenda mapambo ya aina tofauti na kutaka kuonekana na watu au kuonesha watu ikiwa ni pamoja na kudharau waume zao na kuitamka laana kwa wingi. Hadithi iliyopokelewa na Ibn Abbas R.A.A. na iliyotolewa na Bukhari, Mtume S.A.W. kasema, "

"Nimeoneshwa Moto tahamaki (nikaona) wengi wa watu wake ni wanawake wanaokanusha." Ikaulizwa "Jee, wanamkanusha Mwenyezi Mungu?" Akasema "Wanakanusha waume (zao) na wanakanusha ihsani. Lau ukimfanyia ihsani mmoja wao mwaka mzima kisha akaona kitu kutoka kwako (cha kumchukiza) atasema "Sikuona kwako kheri yoyote ile." Pia Hadithi iliyopokelewa na Ibn Umar R.A.A. na iliyotolewa na Muslim na Ibn Maajah, Mtume S.A.W. kasema, "

"Enyi kundi la wanawake! Toeni sadaka na zidisheni kuomba maghufira (msamaha). Kwa hakika mimi nimekuoneni nyinyi zaidi watu wa Motoni." Mwanamke mmoja mwenye akili miongoni mwao akasema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Na vipi sisi tukawa wengi watu wa Motoni?" Akajibu, "Mnazidisha (kuitamka) laana na mnakufuru fadhila na ihsani za waume zenu. Sikuona waliopungukiwa akili, dini na maarifa zaidi kuliko nyinyi." Akasema (mwanamke) "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kwa nini tukapungukiwa akili na dini? Akajibu (Mtume S.A.W.), "Ama mmepungukiwa akili kwa sababu ushahidi wa wanawake wawili ni sawasawa na ushahidi wa mwanaume mmoja na huko ndiko kupungukiwa akili. Na mnakaa masiku hamsali na mnafungua (mwezi wa) Ramadhani na hii ndio kupungukiwa dini."

Wabilahi Toufiq



‫Anasema Allaah

>





10:34am Jun 11
‫Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

((مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّئَةُ حَبَّةٍ وَاللّهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ وَاللّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ))

((Mfano wa wanaotumia mali zao katika njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye, na Allaah ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua)) [Al-Baqarah: 261].

Hivyo tunaona kwamba kila unapotoa mali yako Allaah سبحانه وتعالى Hukuzidishia hiyo mali. Mfano huo Alioutoa Allaah سبحانه وتعالى katika Aayah hiyo inatupa hesabu ifuatayo:‬


MAFUNGU (MAKUNDI) MATATU YA WAOMBAJI DUA






p

Hass7:46pm Jun 12
MAFUNGU (MAKUNDI) MATATU YA WAOMBAJI DUA NA MATOKEO YAKE.

Ndugu muislamu waomabaji dua wamegawanyika makundi matatu:
i/.Wapo ambao huomba na kujibiwa moja kwa moja
ii/. Wapo ambao huomba na hawajibiwi
iii/.Kundi la tatu limegawanyika sehemu kuumbi:
(a). Moja ni lile lisilofanikiwa kwenye maombi na hufanikiwa kwenye shiriki
(b). Pili ni lile ambalo halifanikiwi kwenye shiriki wala kwenye maombi
Kundi la kwanza hili ni la Wacha-Mungu ambao hawa dua zao hujibiwa haraka kutokana na Ucha-Mungu waliokuwa nao. Hawa M/Mungu hana hasira nao kwa hiyo huwapa waliombalo na Allah (s.w) huwapenda kwani wamemjua na kumpa haki yake sitahiki na wanaitwa Mawalii wa Allah.
" Bila shka rehema za Mwenyezi Mungu ziko karibu sana na wale waja wake wafanyao mema" (Aaraf:56).
Pia katika hadithi iliyopokelewa na Anas (r.a) anasimulia kuwa Mtume (s.a.w) alisema M/Mungu anasema kama mja wangu anisogeleapo kwa kiasi cha futi moja, mimi (Allah) namsongelea kiasi cha yadi moja na anaponisogelea kwa kiasi cha yadi moja mimi (Allah) namsongelea kwa kiasi cha mikono miwili iliyonyooshwa na anisogeleapo akiwa natembea nami (Allah) namsogelea nikiwa nakimbia (Bukhari) .

Kundi la pili ni lile ambalo halijibiwi hata liombe kwa vile limeghadhibikiwa na Allah kutokana na maasi wayatendayo. Ni kama ilivyo kwa mzazi hawezi kuwa na mapenzi na mtoto asiyekuwa mtiifu kwake.
Haya anayathibitisha Allah (s.w) katika kitabu chake kitukufu kuwa:
"Na atakayefanya ubaya, basi hawatalipwa wale wafanyao ubaya ila yale waliokuwa wakiyafanya" (Qasas: 84).
Pia katika surat Ruum Allah (s.w) anaendelea kusema kuwa:
"Anayekufuru madhara ya kufuru yake ni juu yake mwenyewe. Bila shaka yeye hawapendi makafiri" (Ruum:45).

Kundi la tatu ambalo limegawanyika katika sehemu mbili ufananuzi wake ni kama ifuatavyo:
Kundi lifanikiwalo kwenye kufru. Hapa shetani anawacheza shere tu yeye huwapelekea misukosuko nay eye mwenyewe huwaondolea pindi tu wafanyapo kufru ili kumridhisha yeye katika lengo la ke la kuwakufrisha wanadamu kama alivyochukuwa ahadi kwa Allah (s.w) pale alipofukuzwa katika rehhema zake. Mfano mtu aliyerogwa kuaguliwa kwa njia ya uchawi, hata kama uchawi utaondoka itakuwa ni haramu kwa vile uchawi ni amali ya shetani. Haiwezekani uaguliwe kwa njia ya uchawi ni lazima kuwe na makubaliano baina ya uchawi na kiaguzi ( Uchawi ni shetani na kiaguzi ni shetani). Siyo mapambano kama vile tiba ya Ruqya za kisheria (Quran) ndio maana yeyote aliyeaguliwa ucahwi kwa njia ucahwi lazima alazimishwe kuvaa hirizi, kutundika tarasimu na mengine kam hayo.
Katika kundi hili la tatu sehemu ya pili ni wale ambao hawafanikiwi kwa Allah nakwe4nye kufru, Ni kwamba M/Mungu hana ubia na wala shetani hatki ubia. Mwenye kumtegemea M/Mungu pekee Allah (s.w) atamkidhia haja zake lakini kwa mashariti ya kumtegemea yeye pekee. Hachanganywi na chochote katika utendaji wake na akichanganywa na chochote yeye hukaa pembeni. Kwani haki na batili havikai pamoja kama anavyo bainisha Allah (s.w) katika sulatu Baqarah.
"Basi anayemkataa shetani na akamwamini Mwenyezi Mungu, bila shaka yeye ameshikilia kishiko chenye nguvu kisicho vunjika, Na Menyezi Mungu ndiye asikiaye na mjuzi,.Mwenyezi Mungu ni mlinzi wa wale walioamini, lakini waliokufuru walinzi wao ni mashetani huwatoa katika mwangaza na huwaingiza kwenye giza.Hawo ndio watu wa motoni, humo wataka milele" (Baqarah:256-257).

Katika aya nyingine Allah (s.w) anabainisha kuwa shetani hana nguvu zozote za kukusaidia chochote.
" Nani huyo awezaye kuombea mbele ya Allah iba idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na yaliyo nyuma yao. Wala hawo viumbe (mashetani) hawalijui lolote katika yaliyo kwenye ilimu yake Allah ila kwa alipendalo yeye" (Baqarah :255),
Kati ya Allah na shetani, Allah ndiye mwenye mamlaka ya kweli, lakini shetani naye anajipa mamlaka kwa hiyo hawa hawakubaliani hata kidogo kila mmoja ana lake,.Basi ukimshika Allah shetanai anakususia na ukimshika shetan Allah anakususia.
Haiwezekani upatwe na misukusuko kasha utumie njia za kishirikina kuondosha na mara baada ya shetani kutumikia kwa lengo la kukufurisha ili uingie motoni mara unaonekana ukifunga ramadhani na kusali n akufanya mema mengine ambayo shetani hayapendi atakuona unamvurugia lengo lake hivyo hutafanikiwa katika yale uliyoyaomba kwa njia za kishirikina.
Vile vile leo uko kwa shetani kesho uko kwa Mwenyezi Mungu naye hakubali kukukidhia haja zako kwa vile una Mungu mwingine. Kwa maana hiyo kundi hili linashindwa kufanikiwa pande zote kutokana na hao wanao wategemea hawana ubia.

Inshallah Allah akitupa wasaa tutaongelea nyakati na hali ambazo ndani yake dua hujibiwa moja kwa moja.


Kutoa Mali Yako Kwa Ajili Ya Allaah





T
Kutoa Mali Yako Kwa Ajili Ya Allaah Imetoka...
T 12:34pm Jun 13
Kutoa Mali Yako Kwa Ajili Ya Allaah

Imetoka kwa Abu Hurayrah R.anhu amesema: Mtum SAW amesema: Kila 'amali
njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba hadi Atakavyo Allaah…)). [Ahmad].

Na hii ndio maana Anasema Allaah سبحانه وتعالى katika Aayah nyingine kuwa mtu anapotoa mali yake kwa ajili Yake ni kama mfano amemkopesha Allaah سبحانه وتعالى mkopo mzuri ambao malipo yake ni kuzidishiwa zaidi ya hiyo mali aliyoitoa, kisha juu yake ni kupata ujira mwema kutoka kwa Mola wake Mtukufu. Ni muhimu kujua kuwa Yeye Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى Ndiye Anayeturuzuku hiyo mali, kisha Anatutaka tumkopeshe katika hicho alichotupa ili Atulipe zaidi ya Aliyoturuzuku kabla. Basi nani atakayesita kutoa mkopo kumkopesha Mola wake kwa kutegemea malipo kama hayo?

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

((مَن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضاً حَسَناً فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ))

((Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mwema, ili Amrudishie maradufu, na apate malipo ya ukarimu)) [Al-Hadiyd: 11]

Kutoa mali kwa fiy Sabili-Allaah ni jambo lenye kutaka kuazimiwa kikweli kwani hakuna asiyependa kumiliki mali. Na wakati wa kutoa mali shaytwaan husimama haraka kumtia wasiwasi binaadamu asitoe mali yake. Unapofika wakati huo basi ndugu Muislamu kumbuka kuwa thawabu zake ni nyingi mno na nzito mbele ya Allaah na ndio maana tunaona kwamba Allaah سبحانه وتعالى Ametanguliza mali kabla ya nafsi katika kuhimiza kufanya jihaad fiy Sabiyli-Allaah:

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَى تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ))

((تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ))

((يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))

((Enyi mlioamini! Nikuonyesheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iliyo chungu?))

((Muaminini Allaah na Mtume Wake, na piganeni Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua))

((Atakusameheni dhambi zenu, na Atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa)) [Asw-Swaff: 10-12].

Vile vile:

((إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُوْلَئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ))

((Hakika Waumini ni wale walio muamini Allaah na Mtume Wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli)) [Al-Hujuraat: 15].

Kama tunavyoona katika Aayah hizo za juu kwamba Allaah Anatupa nguvu kutoa mali fiy Sabili-Allaah kwa kutuhakikishia kuwa kutoa ni kufanya biashara Naye ambayo matokeo yake ni kupata faida nyingi na juu ya hivyo ni kupata maghfira kutoka Kwake:

((إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ))

((لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُور))

((Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalah, na wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika Tulivyowaruzuku, hao hutaraji biashara isiyododa [isiyoanguka]))
((Ili Yeye Awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani)) [Faatwir: 29-30].



HEBU SOMENI NYINYI WANANDOA








11:56am Jun 13
‫عَنْ أَبِى هُرَيْرَةَ رَضِىَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُوْلَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم قَالَ:أَتَدْرُوْنَ مَاالْغِيبَةُ؟قَالُوا:اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ:قَالَ ذِكْرُكَ أَخَاكَ بِمَايَكْرَهُ.قَالَ:أَفَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِى أَخِى مَاأَقُوْلُ.قَالَ:إِنْ كَانَ فِيْهِ مَاتَقُوْلُ فَقَدِ اُغْتَبْتَهُ,وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيْهِ فَقَدْ بَهَتَّهُ)أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abii huraira Radhwi za M/mungu ziwe juu yake,Amesema Mtume wa M/mungu rehma na amani ziwe juu yake.
Hivi mnamjua msengenyaji?,wakajibu maswahaba "M/mungu na mtume wake ndio wenye kujua"
Akasema Mtume,kusengenya ni kumtaja ndugu yako wakati hayupo kwa yale yanayo mkera.maswahaba wakauliza, "Jee ikiwa yale tunayomzungumzia ni ya kweli?" akasema tena mtume "hata ikiwa mnayomzungumzia ni ya kweli mtakuwa mmemsengenya,na hata kama mnayomzungumzia hana basi utakuwa umemsengemya.
Imepokelewa na imamu muslim‬


Monday, June 11, 2012

SABABU ZA KUFELI KWA WANAFUNZI JAPO KWA UCHACHE

Ninamshuktru Allah(s.w) kama anavyostahiki kushukuriwa sala na salam
zimfikie mtume wake sayyidina Muhamad(s.a.w) pamoja na sahaba zake na
kila anayefuata njia yake

A:SABABU ZA KUFELI
-Sera ya taifa
-Kuondolewa kwa mtihani wa kidato cha pili
-MFUMO KRISTO
-Wazazi

B:SABABU ZA MWANAFUNZI
-Kutokujitambua
-Mahudhurio hafifu
-Matumizi ya lugha
-Nidhamu
-Ushirikiano
-Kuathiriwa na utandawazi
-Kuathiriwa na mitandao ya kijamii km vile facebook,twitter,eskim..
-Mashindano ya urembo(Miss)
-Kupenda anasa na starehe za dunia
-Kutozingatia usomaji wenye tija
-Ujibuji wa maswali
-Uelewa

Friday, June 8, 2012

Fwd: [UTAMU WA NDOA] "STARA NI WAJBU KWA MWANAMKE WA KIISLAMU"...




"STARA NI WAJBU KWA MWANAMKE WA KIISLAMU" Mwanamke mwili wake wote ni 'awrah mbele ya wanaume ambao si Mahram zake (anayeweza kumuoa), na haijuzu kwake kuonekana mbele ya wanaume hata kama atakuwa ni mwenye kujisitiri, kwa kuhofia fitnah kwa kumuangalia na kuona jinsi ni alivyo na jinsi anavyotembea. Kuhusiana na lililosemwa kuhusu 'awrah ya mwanamke mbele ya wanawake wenziwe kuwa ni kutoka kitovu hadi magoti, hii inatumika tu wakati atakuwa kwenye nyumba yake miongoni mwa dada zake na wanawake ambao anaishi nao.
Kanuni za msingi bado zinasisitiza asitiri mwili wake wote ili achukuliwe kama kiigizo bora na haya mazoea maovu yameenea miongoni mwa wanawake. Vile vile, anapaswa kusitiri uzuri wake mbele ya mahram wake na wanawake wageni ili baadhi ya mahram wake wavutiwe (waathirike) nae kitabia na adabu, au ili baadhi ya wanawake wasije kwenda kumuelezea yeye wasifu wake kwa wengine (wanaume). Imeripotiwa katika Hadiyth kuwa Mtume (S.A.W) amesema:

"Haitakiwi mwanamke kumuelezea mwanamke mwengine kwa mume wake, hivyo ni kama (mumewe) anamuona yeye" Kinachomaanishwa ni kuwa uzuri wake, kama vile kifua chake, mabega yake, tumbo lake, nyuma, mikono yake, shingo yake na ndama yake inakuwa wazi, kila mtu anaona kwamba ni jambo lisiloweza kuepukwa, mtu kuwa na hisia yake.
Na ni kawaida wanawake huelezea juu wa waliyoyaona kwa familia zao, sawa wanamume na wanawake. Hivyo mwanamke anaweza kutaja hayo mbele ya watu ambao si Mahram wake, kwa namna ambayo inaweza kuwafanya wao kuvutiwa kwake [huyo mwanamke], au ambayo inaweza kusababisha watu wabaya kutafuta njia kuanzisha uhusiano naye.
Kwa sababu hii, wanawake wanatakiwa kufunika 'awrah [sehemu zisizotokiwa kuonekana katika miili] yao - kama vile vifua vyao, migongo, mikono, ndama, n.k, - vile vile hata mbele ya mahram wake na wanawake wengine.

Kujisitiri huku kunakuwa muhimu zaidi katika sehemu za makundi, maeneo ya sherehe, hospitali, na mashule, hata kama kutakuwepo wanawake tu, kwa sababu baadhi ya wanaume ambao si Mahram na hata vijana wanaweza kuwaona au kuwachukua picha hali ya kuwa hawana stara zao kamili, na hiyo itakuwa ni sababu ya fitnah kwa wale wanaowaona.

Onyo kali imetolewa kwa wale [wanawake] ambao wanajionyesha na wavaao nguo za kuonyesha au za kubana, wakati Mtume (S.A.W) aliposema:

"Aina mbili za watu wa motoni siwaoni... Wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi, wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao (kwa kuwa warahisi). Vichwa vyao kama nundu za ngamia zinazoyumba (aina ya msuko wa nywele wanaosuka wanawake). Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake ingawa harufu yake inaweza kunuswa kutoka masafa kadhaa na kadhaa" [Muslim]

Kinachomaanishwa ni kwamba wamevaa nguo za kuonyesha au nguo za kubana ambazo zinaonyesha maumbile yao, au kunapokuwepo fursa ya ajira kwenye kampuni ambayo [mavazi yao] huonyesha vifua vyao, matiti yao na sehemu zingine zisizofaa kabisa kuonekana. Hili limeenea katika makundi na katika mikusanyiko ya ujumla yote. Na Allaah Anajua zaidi. Assalaam Alaykum!


View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.

HISTORIA YA Bilaal Bin Rabaah (R.A)







HISTORIA YA Bilaal Bin Rabaah (Radhiya Allaahu...

11:32pm Jun 4
HISTORIA YA Bilaal Bin Rabaah (Radhiya Allaahu 'Anhu) (Prt 1)

Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa kila linapotajwa jina la Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu) akisema;

"Bwana wetu aliyemkomboa Bwana wetu". Akimkusudia Bilaal bin Rabaah (Radhiya Allaahu 'anhu). Wanasema wanavyuoni kuwa; Unapomsikia 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) akimwita mtu 'Bwana wetu', basi tambua ya kuwa huyo ni mtu adhimu.

Imeandikwa katika Siyar al-A'alaam an-Nubalaa kuwa Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye asili yake ni Mhabeshi (mu-Ethiopia), alikuwa mweusi sana, mwembamba, mrefu na mwenye nywele ndefu.

Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa mtumwa wa kabila la Bani Jumhi, na maisha yake yalikuwa kama mtumwa yeyote wa kawaida pale Makkah, hakuwa na uwezo wala uhuru wowote isipokuwa kuwatumikia mabwana zake watu wa kabila la Al-Jumhi. Baadaye alimilikiwa na Umayyah bin Khalaf peke yake ambaye pia anatokana na kabila hilo la Al-Jumhiy, na mama yake Bilaal na jina lake lilikuwa Hamaamah, naye pia alikuwa mtumwa wa kabila hilo la Al-Jumhi.

Mara baada ya Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) kuanza kuwalingania watu katika dini ya Kiislam kwa jahari, Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) akawa anasikia habari za dini hii mpya na habari za Mtume huyu mpya (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam), na habari hizo zilikuwa zikimfurahisha sana kila anapozisikia hasa kutoka kwa Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu 'anhu) aliyekuwa kila anapopata fursa akimwendea Bilaal na watu wengine pia na kuwahadithia juu ya dini hii.

Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) akasilimu mikononi mwa Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu 'anhu) aliyekuwa akifanya kazi kubwa sana tokea siku ya mwanzo katika kuwalingania watu katika dini hii tukufu.

Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa akiwalingania watu waliokuwa huru na akafanikiwa kuwasilimisha watu watukufu wakiwemo watano katika wale kumi waliobashiriwa Pepo nao ni 'Uthmaan bin 'Affaan, Az-Zubayr bin 'Awaam, 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf, Sa'ad bin Abi Waqaas na Twalha bin 'UbayduLlaah (Radhiya Allaahu 'anhu) na wengi wengineo, na alikuwa pia akiwalingania watu wasiokuwa huru kama vile Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) aliyekuwa rafiki yake Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu) tokea hata kabla ya Uislam, na wengineo pia.

Bilaal (Radhiya Allaahu 'anhu) alifuatana na Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu) mpaka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) na kuzitamka shahada mbili mbele yake, na kwa ajili hiyo akawa miongoni mwa watu wa mwanzo kuingia katika dini hii tukufu.
View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.

Siku chache baada ya UVCCM kudai kuwa uamsho WAPO SERIKALINI wamo serikalini


Uislamu Afrika posted in RADIO IMAAN
Siku chache baada ya UVCCM kudai kuwa uamsho...
Uislamu Afrika 6:31am Jun 6
Siku chache baada ya UVCCM kudai kuwa uamsho wamo serikalini, taasisi hiyo ya Uhoams imeibuka na kujibu hoja hizo kama ifuatavyo:
---------
Tunawajibu Stiphen Wasira na UVCC

Jana tulisikia kauli zenu na mkasema Uwamsho wapo Serikali, sisi tunayakubali maneno yenu na tunakiri kuwa ni kweli Muamsho wapo Serikalini.

Nyinyi mmeshindwa kuwataja kwa majina sisi tutawataja kwa majina na vyeo vyao.
...
Muamsho wa kwanza ni Kikwete, yeye ametuamsha na ametwambia wazi Wazanzibar kuwa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba haitoratibu Muungano hivyo ametuamsha na kutueka bayana Wazanzibar kuwa Tume haituhusu, sisi Wazanzibar kinachotuhusu kwenye Katiba ni Muungano hivyo katuamsha kuwa Tume hii ya Katiba si ya Muungano.

Kikwete huyo huyo ametwambia kuwa Muungano ushavunjwa na CCM NEC, na alisema NEC imeshaamuwa kuwa Rais wa Zanzibar asiwe Makamu wa Rais wa Muungano, hivyo ametuamsha kuwa NEC imeenda kivyume na Hati ya Muungano na kwenda kivyume na makubaliano ni kuyavunja makubaliano, hivyo NEC imeuvunja Muungano.

Muamsho Mkubwa ni Pinda nae ametuamsha pakubwa tena akatutowa kwenye usingizi mzito pale alipotwambia kuwa Zanzibar si Nchi na alipoambiwa ni nchi amekosea akasema sijakosea wala sijalewa Zanzibar si nchi, ametuamsha pakubwa Pinda.

Muamsho mwengine ni Nyerere alitwambia amechoka na sisi Wazanzibar na hapa namnukuu "tumechoshwa na Wazanzibar na Uislaam" kama si Muamsho nani?

Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, yey katuachia uswiya na alitwambia Muungano kama koti likikubana livuwe nae pia ni Muamsho.

Muamsho mwengine ni Mansour Yussuf Himid nae katuamsha sihaba pale aliposema ndani ya Baraza la Wawakilishi kuwa Serikali moja hataki kuisikia, mbili ni butu, anataka Serikali tatu au vyenginevyo.

Amani Karume wa Pili nae katuamsha tena haitoshi akatuletea Umoja wa Kitaifa na Mabadiliko ya Katiba ya 10 ya Katiba ya 2010 tena akaifanya iwe shoka la kuvunja Muungano, isomeni vizuri Katiba ya Zanzibar na hapo mtajuwa kuwa ni Muamsho au si Muamsho.

kwa hiyo Stiphen Wasira na UVCCM hamjakosea kusema Muamsho wapo Serikalini, ni kweli, tena wapo serikali ya Chama chenu, wala msimtafute mchawi, wachawi wenyenu.
uvccm-na-steven-wassira.html


Siku chache baada ya UVCCM kudai kuwa uamsho wamo serikalini, taasisi hiyo ya Uamsho imeibuka na kuj...
View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.

Fwd: [Ahlusuna Group] Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya...





Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya...

1:07am Jun 7
Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa Uislamu.

Kwa nini Tunazugumzia Mada hii?
JIBU:
Tuna sababu zifuatazo zinazotufanya tuzungumzie mada hii:

Ni katika kulingania dini yetu kwa Jihadi ya hoja na kuzuia Munkari (Maovu).

﴿فَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَجَاهِدْهُمْ بِهِ جِهَادًا كَبِيرًا﴾(الفرقان:٥٢ قال تعالى:

Amesema Allaah:
"Na wala usiwatii Makafiri na pigana nao Jihadi ya hoja ya (Quraan) Jihadi kubwa". (Surat AlFurqaan: 52).

وقال تعالى:﴿ قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴾(يوسف:١٠٨).

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
"Sema hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah kwa ujuzi mimi na yule aliyenifuata na Ametakasika Allaah na kila upungufu nami si katika washirikina"
(Surat Yuusuf: 108).

وقال صلى الله عليه وسلم:(من رأى منكم منكرا فليغيره بيده فإن لم يستطع فبلسانه فإن لم يستطع فبقلبه وذلك أضعف الإيمان)رواه مسلم.

Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa wa sallam):
"Atakaeona miongoni mwenu ovu lolote aliondoe kwa mkono yake, na kama hataweza basi na kwa ulimi wake na kama hataweza basi na aliondoe kwa moyo wake (alichukie) na hali hii (kulichukia kwa moyo) ni udhaifu mkubwa wa imani" (Imepokewa na Imaam Muslim).

Ni wajibu wetu kutoa Nasaha:

قال تعالى:﴿ وَإِنْ أَحَدٌ مِنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّى يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّهِ (التوبة:٦).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
"Kama mmoja yeyote katika washirikina atakuomba awe karibu nawe basi kuwa karibu nae ili apate kusikia maneno ya Allaah"
(Surat At-Tawbah: 6).

Nini Maana Ya Katiba Ya Nchi? Kwa Mtazamo Usio Wa Kidini.

Katika nchi yoyote msingi wa uendeshaji wa nchi unategemea Katiba. Katiba ni sheria kuu au sheria mama katika nchi yoyote. Sheria nyingine zote zinategemea au zinatungwa kwa mujibu wa katiba, wakati mwingine katiba hutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kijamii kati ya watawala na wananchi (watawaliwa).

Maana ya katiba ya nchi kwa mtazamo wa Kiislamu

Sheria kuu na Sheria Mama katika nchi kwa mujibu wa Uislamu ni Qur-aan na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa sallam).

قال تعالى:﴿ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ﴾.(النساء:٥٩).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
"Ikiwa mkikindana (kukhitalifiana) katika jambo lolote basi lilerejesheni (jambo hilo) kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake"
(Surat An-Nisaa: 59).
View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.

Tuesday, June 5, 2012

CHANGAMOTO KATIKA KUUSIMAMISHA UISLAM KATIKA JAMII

Assalaam aleykum ,katika suala hili la kuusimamisha uislam ktk jamii
waislam wamegawanyika katika makundi matatu na makundi hayo ni:
1-Walioridhika na sasa jinsi tulivyo
2-Wale wanaochukizwa na maisha na tawala ya sasa
3-Ambao wanaona hakuna haja ya kusimamisha dola ya kiislam
Quran 33-1:3,Allah!hata badili watu bila kujibadili wenyewe

Inshaallah muweze kuchangia na coment yako ni muhimu sana