Wednesday, June 13, 2012

SWALI: Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah?



3:29pm Jun 10
SWALI: Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah?
JIBU: Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى.
(ذلك بأن الله هو الحق وأن مايدعون من دونه الباطل )

Hivi ni kwa sababu hakika Allaah ndiye wa kweli, na hakika wanachokiomba ni cha uongo. (Luqmaan: 30)

(من قال لا إله إلا الله وكفر بما يعبد من دون الله حرم ماله ودمه )

Atakayesema 'Laa ilaaha illa Allaah na akawapinga wanaoabudiwa wasio Allaah italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai(.

SWALI: Nini maana ya Tawhiyd katika sifa za Allaah SWA.?
JIBU: Kuthibitisha alivyojisifu Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى au alivyosifiwa na Mtume wake.

) ليس كمثله شيء وهو السميع البصير)

Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. (Ash-Shuwraa: 11)

(ينزل ربنا تبارك وتعالى في كل ليلة إلى السماء الدنيا)

Mola wetu Huteremka kila usiku katika mbingu ya dunia.

SWALI: Nini faida ya Tawhiyd kwa Muislamu?
JIBU: Kupata Hidaaya duniani na kuwa katika amani Akhera.

(الذين أمنوا ولم يلبسوا إيمانهم بظلم أولئك لهم الأمن وهم مهتدون )

Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakaopata amani na wao ndio walioongoka. (Al-An'aam: 82)

( حق العباد على الله أن لايعذب من لا يشرك به شيئ )

Haki ya mja kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى (Anayomfanyia) kuwa Hamuadhibu yule asiyemshirikisha Yeye na chochote.

View Post on Facebook · Edit Email Settings · Reply to this email to add a comment.

1 comment:

Anonymous said...

HAYA